Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ugumba wa mwanamke unasababishwa na nini?

Featured Image

Ugumba wa mwanamke ni hali ya mwanamke kushindwa kupata mimba. Kama kwa wanaume kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha ugumba wa wanawake.
Ili mwanamke aweze kupata mimba, vitu vingi lazima vitokee. Lazima yai lipevushwe, lazima yai lii ngie kwenye mrija wa kupitisha yai ambapo mimba hutungwa, tena lazima yai lililorutubishwa lifikie kwenye mfuko wa mimba na mwishoni lazima utando ndani ya mfuko wa uzazi uandaliwe. Endapo yoyote kati ya hali hizi hazitafikiwa kwa sababu fulani, mimba haiwezi kutunga. Sababu za kutopevuka yai mara nyingi ni mfadhaiko wa kiakili na kisaikologia na sababu za kuziba mrija wa kupitisha yai mara nyingi ni magonjwa ya zinaa. Wanawake wengine wamepata ugumba kutokana na kujaribu kutoa mimba, matokeo yake wameziharibu kabisa sehemu za ndani za viungo vya uzazi. Bahati mbaya, hali nyingi katika hizi haziwezi kurekebishwa na wanawake wanabaki wagumba wa kudumu.
Kuna mambo mengine yanayosababisha ugumba wa muda. Mambo hayo ni pamoja na ugonjwa, ulevi, matumizi ya dawa za kulevya, lishe duni, mshituko na majonzi. Vingi vya vyanzo hivi vinaweza kutibwa, kwa mfano, kutumia madawa ya kulevya. Mara vikitibiwa, mwanamke ataweza kupata mimba.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu tena kwenye blogu yetu ya mapenzi. Leo tutaangazia swali linaloulizwa mara kwa mara kuhusu... Read More

Kwa nini pombe za kienyeji ni hatari kuliko pombe za viwandani?

Kwa nini pombe za kienyeji ni hatari kuliko pombe za viwandani?

Pombe zinazotengenezwa kiwandani zinafuata viwango
ambavyo ubora wake umethibitishwa kihalal... Read More

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu san... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono/Kufanya mapenzi

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono/Kufanya mapenzi

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono/Kufanya Mapenzi 😊πŸ”₯

... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

Kwani Albino hawatakiwi kuishi duniani?

Kwani Albino hawatakiwi kuishi duniani?

Albino ni binadamu kama alivyo binadamu mwingine na ana haki
sawa za kuishi na kufaidi kuwep... Read More

Kwa nini Albino tunaonekana kama mzigo katika familia zetu?

Kwa nini Albino tunaonekana kama mzigo katika familia zetu?

Watu wanaohitaji kupewa uangalizi maalumu wanaweza
kuonekana ni mzigo kwa kuwa wanaweza waka... Read More

Je, kuharibika mimba kunasababishwa na nini?

Je, kuharibika mimba kunasababishwa na nini?

Asimilia kumi hadi i i ishirini ya mimba huharibika. Mimba nyingi zinaharibika katika kipindi cha wi... Read More
Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa? πŸ€”

Kuna wakati maish... Read More

Kwa nini Albino wanawekwa katika kundi la watu wenye ulemavu?

Kwa nini Albino wanawekwa katika kundi la watu wenye ulemavu?

Ulemavu maana yake ni hitilafu katika mwili au akili inayomwekea
mipaka mtu asiweze kufaniki... Read More

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More

Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki? Natumaini uko salama na unafurahia siku yako. Leo nitazungumzia suala linaloh... Read More