Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Featured Image

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, mawasiliano ni muhimu katika kuboresha uzoefu wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, mawasiliano ni muhimu katika kuboresha uzoefu wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, wewe na mwenzi wako mnahisi kama hamjawai kufurahia tendo la ndoa? Kila wakati mnafikiri kuwa... Read More

Kwa nini watu wengine wanaamua kutoa mimba?

Kwa nini watu wengine wanaamua kutoa mimba?

Hapa Tanzania utoaji wa mimba hauruhusiwi kisheria. Hata hivyo watu wengine wanaamua kutoa mimba ... Read More

Albino anaweza kuwa na maisha ya kawaida na yenye mafanikio katika maisha?

Albino anaweza kuwa na maisha ya kawaida na yenye mafanikio katika maisha?

Imani iliyojengeka kwenye jamii kuwa Albino wana uwezo
mdogo si ya kweli. Ipo mifano mingi y... Read More

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Hivi karibuni, wanaume wengi wamekuwa wakikosa jinsi ya kuonyesha shukrani kwa msichana wao. Hata... Read More

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kwanza kabisa, watu ni kweli wawe wamedhamiria kuacha. Hii inataka uamuzi wa wazi na nia imara kwa s... Read More
Kwa nini pombe na sigara bado zinatangazwa wakati zina madhara?

Kwa nini pombe na sigara bado zinatangazwa wakati zina madhara?

Serikali inatakiwa iamue kuwepo kwa matangazo ya biashara
ya pombe na sigara au la? Serikali... Read More

Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii ... Read More

Kwa nini mara nyingi mvulana ni mwepesi sana katika kuanzisha kufanya mapenzi? Na kwa nini mwanaume mara nyingi anafikia mshindo kabla ya mwanamke? Mwanaume anawahi kufika kileleni kwa nini?

Kwa nini mara nyingi mvulana ni mwepesi sana katika kuanzisha kufanya mapenzi? Na kwa nini mwanaume mara nyingi anafikia mshindo kabla ya mwanamke? Mwanaume anawahi kufika kileleni kwa nini?

Kwa kawaida i inakubalika kuwa wavulana ndiyo waaanze kuonyesha ishara za kujamiaana na tafiti zi... Read More

Ukeketaji ni nini?

Ukeketaji ni nini?

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndan... Read More

Nini maana ya neno Albino?

Nini maana ya neno Albino?

Neno Albino linamaanisha mtu mweupe, linatokana na neno la lugha ya Kilatini - albus-linamaanisha β€... Read More
Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kipekee na Ya Kusisimua na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kipekee na Ya Kusisimua na Msichana

Kila mwanaume anataka kuwa na tarehe ya kipekee na ya kusisimua na msichana. Lakini, wakati mwing... Read More

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Kama unavyohusisha rafiki zako katika mihemuko mingine, inaeleweka kama utataka kuwashirikisha ka... Read More