Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Featured Image

Athari za pombe kwa mtu anayeishi na ualbino ni sawa na zile
zinazowapata watu wengine.
Mtu akiwa katika hali ya ulevi anaweza kuzembea katika
kufanya uamuzi sahihi kwa mfano kuhatarisha maisha yake
kwa kuendesha baiskeli yake kimchoromchoro, kujamiiana
bila kuvaa kondomu na kadhalika. Mbali na hayo, watu wenye
matatizo ya kunywa pombe husahau kujiweka katika hali nzuri
kwa maana hawajali kula chakula. Tabia hii inamuweka katika
hatari ya kuandamwa na maradhi.
Pombe zinaweza pia kuingiliana na maisha/uhusiano wa kimwili.
Mwanzo kabisa pombe inaweza kukusisimua na kukufanya
mchangamfu (kutoona aibu), lakini kadiri unavyoendelea
kunywa unaanza kusinzia na kwa upande wa wanaume wengine,
uume kukosa nguvu. Unaweza kushawishika kutoa aibu uliyo
nayo kwa kunywa pombe lakini mara nyingi hii haileti mvuto
kutoka kwa wenzi wako.

Kunywa pombe pia kunaleta uharibifu wa kudumu kwenye ubongo
ambao unamfanya mtu kupata matatizo ya kumbukumbu.
Pombe imewekwa kwenye kundi la vilevi tegemezi. Mwili
ukishazoea pombe, ni rahisi sana watu kutumia pesa zote
kwa ajili ya pombe na kusahau kufanya mambo mengine
yatakayomletea maendeleo katika maisha yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu ha... Read More

Njia za Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Msichana

Njia za Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Msichana

Njia za Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Msichana

Mawasiliano ni muhimu katika kila uhusia... Read More

Je, Ni Vipi Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono?

Je, Ni Vipi Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono?

Je, ni vipi kuepuka shinikizo la kufanya ngono? Hii ni swali ambalo vijana wengi hujikuta wakijiu... Read More

Kama sitaki kujamiiana kabla ya ndoa, nifanye nini ili kuondokana na adha ya vishawishi vya hao ambao ameshaanza kujamiiana?

Kama sitaki kujamiiana kabla ya ndoa, nifanye nini ili kuondokana na adha ya vishawishi vya hao ambao ameshaanza kujamiiana?

Kama umeamua kutojamiiana kabla ya ndoa, huo ni uamuzi mzuri na ni haki yako. Kutojamiiana kabla ... Read More

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati wa kumnyonyesha?
Ndiyo, mama mwenye vi... Read More

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali ... Read More
Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la β€žcareβ€œ na β€œLady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatika... Read More

Kwa nini inapendekezwa Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu?

Kwa nini inapendekezwa Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu?

Kwa nini inapendekezwa Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu? 🌟

Karibu vijana wenzangu! Leo tut... Read More

Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuing... Read More
Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madha... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Kuwa na uhusiano wenye furaha na msichana ni jambo ambalo kila mwanaume anatamani. Lakini mara ny... Read More

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Kwa Ufanisi

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Kwa Ufanisi

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Kwa Ufanisi 🌟

Karibu vijana wenzangu! Leo, tutajadili njia ... Read More