Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Tunda asili yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linaj...
Read More
Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba...
Read More
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki,...
Read More
Tafadhali chukua walau dk 2 kusoma hii:
1. Chukulia ni muda wa saa 1:25 jion unarudi nyumba...
Read More
Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila sik...
Read More
Mwili wa binadamu umeundwa kwa organs na mifumo mbalimbali ili kuuwezesha kufanya kazi sawia. Mfa...
Read More
Unahitaji:
a)Kijiko kimoja cha asali
b)Parachichi 1
Hatua kwa hatua namna ya ...
Read More
Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina k...
Read More
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi...
Read More
Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:
Huondoa sumu Mwilini
Chanzo kizuri cha viua ...
Read More
Dawa ya mswaki au dawa ya meno ni dawa nyingine ya asili unayoweza kutumia kujitibu chunusi. Hii...
Read More
Asthma /pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!