Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
Dalili
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
· Kushindwa kupumua vizuri
· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
· Kucha kuwa dhaifu
· Kusikia hasira na kuhamasika haraka
· Kuchoka sana kuliko kawaida
· Maumivu makali ya kichwa
· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
· Uchovu wa mara kwa mara
Matibabu.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubong...
Read More
Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unao...
Read More
Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa k...
Read More
Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua u...
Read More
Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuz...
Read More
Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu k...
Read More
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki ...
Read More
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak...
Read More
Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana...
Read More
Mwili wa binadamu unafanya mambo
mengi ya kibaiolojia ambayo mara
nyingi ni vigumu kuya...
Read More
Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asub...
Read More
Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni ...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!