Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Featured Image

Mimi Nimecheka sana
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZAπŸ˜€πŸ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, β€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, β€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, β€œSalama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka β€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Charles Mboje (Guest) on March 21, 2022

πŸ€£πŸ˜†πŸ˜ŠπŸ˜‚

Joseph Mallya (Guest) on March 6, 2022

Hii imenifurahisha hadi nacheka kwa sauti! πŸ€£πŸ˜‚

Stephen Kangethe (Guest) on March 6, 2022

Nimecheka hadi mbavu zinauma πŸ˜‚πŸ˜‚

Christopher Oloo (Guest) on March 4, 2022

πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜Š

Lydia Mutheu (Guest) on February 14, 2022

Nimecheka hadi nimepata furaha! πŸ˜ŠπŸ˜†

Charles Mboje (Guest) on January 30, 2022

🀣 Sikutarajia hiyo!

Athumani (Guest) on December 6, 2021

Hii ni kichekesho kali sana, ninashiriki na kila mtu! πŸ˜‚

Robert Ndunguru (Guest) on November 14, 2021

Hizi jokes zinanifanya nicheke kila siku! πŸ˜„πŸ˜†

Ibrahim (Guest) on October 30, 2021

🀣 Hii kichekesho ni nzuri sana!

Salma (Guest) on October 25, 2021

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hiki, asante!

Lydia Wanyama (Guest) on October 22, 2021

Hii imenichekesha sana! πŸ˜„πŸ˜‚

Sharifa (Guest) on October 7, 2021

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hicho!

Mariam Kawawa (Guest) on September 1, 2021

Hii ni joke ya ukweli kabisa! πŸ˜‚πŸ€£

Dorothy Mwakalindile (Guest) on August 4, 2021

πŸ˜… Bado nacheka!

Nyota (Guest) on August 2, 2021

πŸ˜† Naihifadhi hii!

Ann Awino (Guest) on July 1, 2021

Hii imenikuna! πŸ˜†πŸ˜Š

Andrew Mchome (Guest) on June 24, 2021

🀣 Hii imewaka moto!

Rose Kiwanga (Guest) on June 20, 2021

πŸ˜†πŸ˜‚πŸ‘

Janet Wambura (Guest) on May 17, 2021

Hii imenichekesha sana! πŸ€£πŸ˜†

Ann Wambui (Guest) on May 15, 2021

🀣 Hii kichekesho ni nzuri sana!

Elijah Mutua (Guest) on May 1, 2021

Kweli mna kipaji cha ucheshi! πŸ‘πŸ˜†

Nicholas Wanjohi (Guest) on April 29, 2021

πŸ˜„ Kichekesho gani!

Stephen Amollo (Guest) on April 26, 2021

Hii joke ni ya kufurahisha! 🀣🀣

Isaac Kiptoo (Guest) on April 4, 2021

Kweli mnajua kuchekesha watu! πŸ€£πŸ˜‚

Edwin Ndambuki (Guest) on February 26, 2021

Hii imenikumbusha enzi zile! πŸ˜…πŸ˜‚

James Malima (Guest) on January 23, 2021

πŸ˜ƒ Hii imenichekesha kwa sauti kweli!

Dorothy Mwakalindile (Guest) on January 19, 2021

Hii imenipa kicheko cha siku! πŸ˜‚πŸ€£

Thomas Mtaki (Guest) on January 15, 2021

πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜ŠπŸ˜…

Margaret Anyango (Guest) on December 30, 2020

Siwezi kusubiri kuieleza kwenye sherehe yangu inayofuata! πŸŽ‰

Mgeni (Guest) on December 19, 2020

Hii imenigonga vizuri, punchline gani! πŸ˜†

Nahida (Guest) on December 16, 2020

πŸ˜‚ Hii kichekesho imenifurahisha siku nzima!

Joseph Njoroge (Guest) on November 25, 2020

πŸ˜„ Kichekesho kamili!

Dorothy Majaliwa (Guest) on November 22, 2020

πŸ€£πŸ˜­πŸ˜†

Daniel Obura (Guest) on November 5, 2020

πŸ˜…πŸ˜ŠπŸ˜‚πŸ‘

Sekela (Guest) on October 21, 2020

πŸ˜† Naihifadhi hii!

John Lissu (Guest) on October 9, 2020

Nimecheka hadi machozi 🀣😭

Henry Mollel (Guest) on August 28, 2020

πŸ˜… Bado ninacheka!

Salma (Guest) on August 9, 2020

πŸ˜‚ Nimeipenda kabisa hii!

Chris Okello (Guest) on August 4, 2020

πŸ€£πŸ˜„πŸ˜Š

Mary Kendi (Guest) on July 28, 2020

🀣 Nalia kwa kicheko kweli!

Andrew Mchome (Guest) on July 24, 2020

Hii ni joke ya kipekee! πŸ€£πŸ‘Œ

Anna Sumari (Guest) on June 30, 2020

πŸ˜ƒ Hali imeboreshwa papo hapo!

Alex Nakitare (Guest) on April 29, 2020

😁 Hii imenifanya siku yangu iwe bora!

Andrew Mahiga (Guest) on April 10, 2020

Hizi jokes ni za kipekee sana! πŸ˜†πŸ˜Š

Nancy Kawawa (Guest) on April 8, 2020

πŸ˜† Hii imenigonga kweli!

Alice Jebet (Guest) on April 4, 2020

Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ€£πŸ˜†

James Mduma (Guest) on March 28, 2020

Kila siku napenda jokes zenu! πŸ˜†πŸ˜‚

Andrew Mchome (Guest) on March 24, 2020

Ucheshi wenu unanifurahisha kila siku! πŸ˜†πŸ˜‚

Chris Okello (Guest) on March 10, 2020

πŸ˜‚πŸ€£

Emily Chepngeno (Guest) on March 3, 2020

Kweli mna ucheshi wa kipekee! πŸ˜‚πŸ€£

Issack (Guest) on February 29, 2020

πŸ˜ƒ Hali imeboreshwa papo hapo!

Elizabeth Malima (Guest) on January 18, 2020

Huu ucheshi hauna kifani! 🀣πŸ”₯

Linda Karimi (Guest) on January 17, 2020

Nimefurahia sana hii joke! πŸ˜…πŸ˜‚

Mary Sokoine (Guest) on December 7, 2019

Wow, hizi kichekesho ni dhahabu kabisa! πŸ’°

Joyce Aoko (Guest) on November 11, 2019

😊🀣πŸ”₯

Joyce Nkya (Guest) on October 24, 2019

Nimefurahia hii sana! πŸ˜†πŸ˜Š

Lydia Mutheu (Guest) on October 17, 2019

πŸ˜† Nacheka hadi chini!

Daniel Obura (Guest) on September 29, 2019

Nitaeleza hii kwa marafiki zangu bila shaka! πŸ˜„

Andrew Mchome (Guest) on September 29, 2019

πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜„

Linda Karimi (Guest) on September 25, 2019

Ucheshi wenu unanifurahisha! πŸ˜ŠπŸ˜‚

Related Posts

Pale umapofanya interview huku ukijua hutapata kazi

Pale umapofanya interview huku ukijua hutapata kazi

Pale unaitwa kufanya interview na unajua tuu hutapata kazi tuu…..
Interviewer: where were ... Read More

Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake

Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake

Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu
akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lo... Read More

Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi

Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi

Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kush... Read More

Duh! Wanaume jamani…

Duh! Wanaume jamani…

Lakini sisi wanaume hatuko fair … Yani demu anang'ng'ana kujipodoa uso na sisi tunaang... Read More

Ungekua wewe ndio baba wa Huyu mtoto ungemjibu nini?

Ungekua wewe ndio baba wa Huyu mtoto ungemjibu nini?

MTOTO: Hivi Baba wewe umezaliwa wapi?????
BABA: Mbeya

<... Read More
Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama

Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama

Leo nimeiogopa pombe.

Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muzik... Read More

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, in... Read More
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki; MCHUNGAJI: Kijana, ... Read More
Unakumbuka hizi Sheria zetu za mpira utotoni?

Unakumbuka hizi Sheria zetu za mpira utotoni?

1.Mwenye mpira Lazima acheze ata kama hajui mpira
2.Dogo mnene Lazima aw... Read More

Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli

Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli

Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma bar... Read More

Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani

Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani

Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile... Read More

Mshahara usiobadilika

Mshahara usiobadilika

PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA ... Read More