Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Featured Image

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtoto aliye tumboni. Mtoto aliye
tumboni hurutubishwa kupitia damu ya mama. Kama mama atavuta
sigara au kunywa pombe, sumu illiyopo katika sigara au pombe
inapoingia kwenye damu yake itamfikia mtoto pia. Pombe hushambulia
moyo uendeleao kukua na ubongo wa mtoto aliye tumboni.
Akina mama wanaokunywa kupita kiasi wakiwa wajawazito
wanaweza kupata watoto wenye magonjwa ya moyo au mtindio
wa akili, kwa sababu chembechembe za ubongo hazikui vizuri.
Mara nyingi watoto huzaliwa na upungufu katika mwonekano
wa sura. Kwa mtoto pombe ni sumu kali, hata kama ni kwa kiasi
kidogo, itamdhuru.

Mama anaekunywa pombe anaweza kuwa hajali au kusahau
kujilinda mwili wake na mtoto anayekua.
Kama akipata maambukizo ya VVU na mtoto pia anaweza
akapata virusi vya UKIMWI.
Wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito wana
uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto ambao hufariki ghafla bila
sababu ya kueleweka katika mwaka wao wa kwanza wa maisha.
Watoto wa akina mama wanaovuta sigara mara nyingi huzaliwa
na umbo dogo kuliko wengine kwa sababu watoto walipata
chakula kidogo walipokuwa bado tumboni mwa mama zao.
Ujumbe upo wazi: Wanawake wanaotaka watoto wenye afya
wasivute kabisa sigara wala kunywa pombe wakiwa wajawazito.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, nini imani ya watu katika kuzungumza waziwazi juu ya ngono/kufanya mapenzi na kutokuwa na aibu?

Je, nini imani ya watu katika kuzungumza waziwazi juu ya ngono/kufanya mapenzi na kutokuwa na aibu?

Habari rafiki yangu! Leo tutaongea kuhusu umuhimu wa kuzungumza waziwazi juu ya ngono na kufanya ... Read More

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni mpangilio wa mwili kujikinga na maradhi. Chembechembe nyeupe zilizopo katika damu ... Read More
Kumaliza ashiki au hamu ya kufanya mapenzi

Kumaliza ashiki au hamu ya kufanya mapenzi

Kwa vijana mara nyingine siyo rahisi kufahamu afanye nini mara anapopata ashiki (hamu) ya kutaka ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Kama una nia ya kuimarisha uhusiano wako na msichana, ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri ya sim... Read More

Je, watu wanapenda ngono/kufanya mapenzi ya haraka au ngono/kufanya mapenzi ya muda mrefu?

Je, watu wanapenda ngono/kufanya mapenzi ya haraka au ngono/kufanya mapenzi ya muda mrefu?

Kama mtaalamu wa masuala ya mahusiano, swali la iwapo watu wanapenda ngono ya muda mfupi au muda ... Read More

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na k... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu kwenye ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu kwenye ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu kwenye ngono/kufanya mapenzi? B... Read More

Je, kuna dawa zozote za kutibu magonjwa ya zinaa?

Je, kuna dawa zozote za kutibu magonjwa ya zinaa?

Magonjwa mengi ya zinaa yana dawa za kutibu, kwa mfano: kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi au... Read More

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Kuwa na uhusiano wa mbali sio rahisi... Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Uoga kabla ya Kufanya Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Uoga kabla ya Kufanya Ngono?

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Uoga Kabla ya Kufanya Ngono 🌟

Karibu kwenye makala hii... Read More

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Hakuna madhara yoyote ya msingi anayopata mtu asipooga baada ya kujamiiana. Isipokuwa kwa ajili y... Read More