Updated at: 2024-05-25 17:08:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kusaidia Mtoto wa Nursery Homework ni Ngumu. Unamuuliza "Nina Pipi Tano, nikiwagawia Watoto Watatu, kila mmoja Pipi Mojamoja nabakiwa na ngapi? Anakwambia, "toa Kwanza nizione.."ππππππππππππππππ
*Mdukuzi:* _nikikuuliza swali unaakili ya kujibu?_ *Massai:* _ulisa acha maneno yako._ *Mdukuzi:* _nitajie wanyama kumi wa porini_ *Massai:* _swala watatu na tembo saba_ππππππππΏ
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Updated at: 2024-05-25 17:07:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuβ¦.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:09:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema hataki tena kujiunga fb!
ππππππππππππππ Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Wale wa kupenda kupewa pewa namba za simu soma hii
Updated at: 2024-05-25 17:14:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unaomba namba ya simu ya mdada af anakunyima ila unalazimisha akupe anaona kuliko muendelee kuongea bora tu akupe anakutajia 071112016 unafuraahi unaondoka unafika nyumbani unajaribu kuipiga but kabla hujapiga unagundua alikutajia tarehe ya leoΒ Wadada acheni hizoΒ ππππποΏ½ποΏ½ποΏ½π
Updated at: 2024-05-25 17:09:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake: MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake) MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba) MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa manyani mwanzo?Au wanidanganya? BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπππΆπΌπΆπΌπΆπΌ