Updated at: 2024-05-25 17:08:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:09:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa: Mambo honey, upo ok? Mrembo: Sipo ok my dear Jamaa: Una tatizo gani baby? Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba. Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga? Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu,
Updated at: 2024-05-25 18:01:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza "Hii pete bei gani?" . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu "Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?"
Updated at: 2024-05-25 18:00:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto: Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.
Baba: Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwanangu…..
Updated at: 2024-05-25 17:57:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI
1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati. 2.Inbox na sending items hufutwa kila wakati. 3.Ukimuomba simu yake ghafla lazima akwambie hebu kwanza……. 4. Kamwe haiiti always vaibration. 5. Namba nyingi ha save. 6. Kuna simu hapokei hata iweje….anapenda sms zaidi 7.Majina mengi kwenye simu yameseviwa kwa majina ya kufikirika. 8.Muda mwingi ni mtu wakujihami. 9.Anapenda password na anabadili mara kwa mara. 10.Akiazima simu yako, akitumia tu anafuta dial no haraka. 11.Always yuko na simu…..hadi bafuni ikibidi. 12. Anajazba ukimuuliza chochote kuhusu simu….anajishtukia. 13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa mara kiwiziwizi 14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture na akikuweka humalizi masaa anakudampu huko Hapa kuna ukweli asilimia millioni moja kabisa Share na washikaji zako😜😜😜😜😜