Biashara – Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANGU

Duna Lawrence (78) ni raia wa Togo ambaye alijitosa kwenda nchini Ujerumani kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya 80. Baada ya kufika huko, alipata kazi, akawa muaminifu kwa Bosi wake ili aweze kupata mafanikio.

Baada ya miaka mingi kupita, Duna alirudi nchini mwake kwa mara ya kwanza na akaoa, kisha kurejea tena Ujerumani. Bwana Duna aliendelea kufanya kazi kwa bidii huku mafanikio yake kimaisha yakizidi
kushuka chini, akaomba kuongezewa mshahara ili kukidhi mahitaji yake, lakini hiyo haikumpa unafuu.

Jamaa huyu bado hakuona mafanikio yoyote, kazi zikaendelea kuwa nyingi, familia yake nayo ikawa kwenye wakati mgumu. Bwana Duna umri ulizidi kumtupa mkono, huku akijiona hana chochote cha kujivunia katika kazi anayofanya.

Duna akawa mzee, nguvu nazo zikamuisha, ufanisi kazini ukapungua na magonjwa ya kiutu uzima yakaanza kumwandama, akamweleza Bosi wake hali halisi ya kiafya, akaomba alipwe stahiki zake ili arudi nyumbani. Bosi wake alimwonea huruma Mzee Duna, ila hakuwa na namna nyingine ya kumsaidia zaidi ya kumpa stahiki zake zote. Mzee Duna alirejea nchini Togo.

Mzee Duna akiwa anapekua begi lake wakati wa usiku, alikutana na barua ikiwa na dola 2000 na kuandikwa maneno haya:

“… Duna umefanya kazi kwa muda mrefu lakini ulishindwa kuniuliza jinsi ya kuwa tajiri kama mimi, hilo hukuliona kuwa na maana kwako, ukang’ang’ania kuongezwa mshahara na kudai malimbikizo yako, halikuwa jambo baya, ni haki yako. Ulikuwa kama mfungwa kwangu kwa sababu ya kufanya kazi ukitegemea kupata pesa, uliitumikia pesa kwa muda mrefu na haikuweza kukuondolea umasikini. Ninachokushauri, licha ya umri kuwa mkubwa ila anza kujali mambo yako, Mind Your Own Business, Not Another One’s. Tumia pesa niliyokupatia kujali mambo yako, umejali mambo yangu kwa muda mrefu sana, jifunze kujali shughuli zako… “

Mzee Duna alisikitika sana, akatoa machozi kwa uchungu, hakujali suala la umri kumtupa mkono, akajitosa kutafuta fursa mbalimbali ndani ya nchi yake akiwa na mtizamo tofauti kuhusu pesa. Mzee Duna alifungua mgahawa, akaajiri vijana kadhaa kwa ajili ya kumsaidia kuwahudumia wateja. Biashara ikawa nzuri, akazidi kutanua biashara yake, akaongeza eneo ili kuwahudumia wateja wengi zaidi. Mzee Duna alipata maeneo kadhaa, akafungua migahawa mikubwa na kuipa jina la “MIND YOUR OWN BUSINESS RESTAURANT”.

Nini tunajifunza?

Ifikie wakati kila mtu aanze kujali mambo yake katika kuamua hatima ya maisha yake kiuchumi. Kuendelea kuomba nyongeza ya mshahara, malipo ya ziada, na malupulupu mbalimbali hayatakufanya ujitegemee kiuchumi, bali kuwa tegemezi. Una miaka zaidi ya kumi kazini lakini bado huna uchumi imara, jaribu kujiuliza unamtajirisha nani, nani ananufaika kupitia jasho lako. Lazima ukumbuke kuwa maisha yako yote hayataishia kwenye kazi tu, kuna kipindi hutaweza kufanya kazi kabisa. Je, utaishi kwa njia gani? Anza kufikiria kuhusu maisha yako, timiza ndoto yako na si ya mtu mwingine. Anza kutengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya kujiajiri, usiache kazi kwa papara.

1.Tafadhali fuata hatua makini ili uanze kujali mambo yako.

2.Usifikiri kile wanachofikiri wengi ndicho sahihi.
Fikiri kile kinachokunufaisha wewe ndicho sahihi.

2.Jua maana ya mafanikio!Je, ni kumiliki pesa, vipi kuhusu afya?

Je, mafanikio ni afya, kula vizuri, kuvaa na kula vizuri?Vipi kuhusu mahusiano mazuri ya kijamii na Mungu wako?

Je, maisha ni mahusiano mazuri na Jamii na Mungu?Vipi kuhusu ubinafsi uchoyo na fitna moyoni mwako?

Penda wenzako kwa dhati!Mjue Mwenyezi Mungu wa kweli, Simama imara katika matendo na akili yako.Heshimu na waheshimu wenye mamlaka ama amali za kijamii.

Furahi, ona mbali,fanya kazi, zingatia afya, Mjue Mungu wa Kweli. pumzika vizuri!

Mungu akubariki!

Nia yako isishindwe

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni “NIA”.
Nimemtazama mwendesha pikipiki anaiwasha pikipiki kwa muda mrefu kwa kupiga kiki kwa kurudia rudia, akiamini lazima iwake ili aende anakotaka kwenda. Anajaribu kuwasha kwa kiki ikikataa anajaribu kwa starter, ikigoma anajaribu kuchomoa plug na kuangalia kama kuna tatizo, anajaribu tena na tena mpaka inawaka, anaanza safari yake.

Ingawa ametumia muda mwingi kuhangaika kuiwasha pikipiki yake lakini hakuzimia moyo na kuamua kuitelekeza ili atembee kwa miguu, ila alikua na “NIA” isiyozimika haraka mpaka atakapoona imewaka kwakua anaamini jana iliwaka, lazima na leo iwake hata kama imelala kwenye hali ya hewa ya namna gani.

Ikiwa tunakua na “NIA” ya kufanya mambo madogo madogo yatokee, na tunayasimamia kwa “IMANI” kabisa mpaka yanakua kweli, kwanini tunaogopa kusimamia mambo makubwa yatokee maishani mwetu?. Kwanini unadiriki kusema kwenu hakuna aliyewahi kufanikiwa, hakuna anae miliki gari ya thamanani, hakuna aliyejenga nyumba ya kifahari, hakuna…hakuna….

Kwanini “NIA” yako uilinganishe na kushindwa kwa hao wengine kwenu? Wewe ni mmoja wa tofauti, na ukiamua kujitenga kifikra mbali nao, na kufanya mambo makubwa kwa bidii bila kuzimia moyo, hakika utakua wewe kama wewe kuitwa MABADILIKO ya mafanikio katika hao wengi walioshindwa.

“NIA YAKO ISISHINDWE”

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho unalala masaa manane tena.. Ujue unashabikia mafanikio.

Ukiona Bill Gates anasoma kitabu kimoja kwa wiki. Na wewe unasoma kimoja kwa miezi sita ujue nod maana kuna tofauti ya Bill Gates na wewe.

Ukiona unasema utakuwa successful siku moja afu huna DAILY GOALS. Yani hujui ukiamka ufanye nini na jioni utapimaje kama kweli umekifanya ujue hujaelewa vizuri maana ya kuwa successful.

Hard Work beats talent.

You must sleep less and work harder until you get what you want.

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha – matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote – kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

Usipoteze muda – jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani – soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

Jenga urafiki na taasisi za kifedha – mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha – tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA

Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.

Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU

Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa – angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA

Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA

Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

Fanya vitu wewe mwenyewe – acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu

Kuwa na malengo – kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT

Kuwa na moyo wa ujasiri – usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA

Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

Acha woga – jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

Kuwa na mtazamo chanya – usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

Kuwa na mipaka katika mambo yako – usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu

Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako – waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe

Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja

Ubunifu ni muhimu sana – fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini – kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli
PIGA KAZI

Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea

Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea – kila binadamu anaweza kuwa milionea

Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa – kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Ila kuthubutu ndo hatua ya kwanza.

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa vya mpira.
7.Misumari midogo.
8.Jiko.

MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.
2.Caustic soda
3.Mshumaa.

KAZI ZAKE:

1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

JINSI YA KUTENGENEZA.

(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c)KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.

Shopping Cart