Biashara – Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti

Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-

Hiyo ina maana mahindi 50 ananunua kwa shilingi 5000/- akichoma na kuuza anapata sh.30,000/-. Akitoa pesa ya mtaji (5000/- ya mahindi na 1500/- ya mkaa) anabakiwa na sh.23,500/- kwa siku.

Hivyo kwa mwezi huyu mchoma mahindi atakuwa ameingiza kiasi cha sh.705,000/-

Mwalimu mwenye Degree anayeanza kazi analipwa 584,000/- akikatwa kodi pamoja na makato mengene ya mifuko ya jamii anabakiwa na sh.425,000/.

Tofauti ya Mwalimu wa degree na Muuza mahindi ni kuwa Mwalimu kaajiriwa, muuza mahindi kajiajiri. Mwalimu anafanya kazi masaa 9 kwa siku, muuza mahindi anafanya kazi masaa matatu kwa siku (saa 12 jioni hadi 2 usiku). Mwalimu anatumia muda wake wa ziada kusahihisha mitihani na homework, mchoma mahindi anatumia muda wake wa ziada kutafuta fursa nyingine za kupata hela.

Uoga wako ndio umaskini wako.
KAMA HUNA FURAHA NA UNACHOKIFANYA BADILI MTAZAMO NA SIKUSHAURI UKAUZE MAHINDI NO HUO NI MF. KAMA SWALA NI KIPATO TU BASI KUNA FURSA NYINGI SANA KIPINDI HIKI NA WAWEZA BILA HATA YA KUWA NA MTAJI CHA MSINGI NI WEWE KUAMUA KUWAONA WATAALAMU WAKUSHAURI NI NINI CHA KUFANYA.

mafanikio yanaanza nawewe

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.

Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.

Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda yake yanaweza kuwa fedha, lakini katu fedha haiwezi kuzaa ndoto. Kwa hiyo bais, ndoto ni kubwa kuliko fedha.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, mtu maskini kuliko wote duniani ni yule asiyekuwa na ndoto!

Hivyo utakubaliana naye kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si maskini, maana ana kitu cha thamani, cha pekee na cha tofauti ambacho hakuna mwenye nacho isipokua wewe mwenyewe.

Tatizo kubwa ni kwamba, watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini wanashindwa kutambua kwamba hakuna fedha inayozidi ndoto isipokuwa ndoto inazidi fedha.

Tatizo lingine ni kwamba, watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na kila nyanja.

Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka ama unachokihitaji – iwe fedha, utajiri, umaarufu, familia nzuri, mume mzuri, mke mzuri, watoto wazuri, kazi nzuri, afya nzuri – hivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo.

Lakini tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitimie na zikuzalie mafanikio. Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama hutaitimiza ikaja kwenye uhalisia tambua kwamba utakufa maskini ukiwa na utajiri wa ndoto, jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaoishi maisha ya chini tofauti na walivyopaswa wawe.

Ndoto yako ndiyo imebeba kusudi la maisha yako. Kama hutaishi katika ndoto yako maana yake utakuwa hujaishi maisha yako ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kwenye ndoto zako.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, watu wengi duniani hawaishi, bali wapo tu. Kuna tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Kuishi ni kutimiza ndoto zako na ndani ya kusudi la maisha yako, lakini kama hutimizi ndoto hizo uko nje ya kusudi la maisha yako. Wewe utakuwa hauishi bali upo upo tu.

Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka. Ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka! Hana sababu za msingi. Kataa kuishi bila agenda, bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.

Kila kitu kipo kwenye ndoto zako, tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha kwa sababu fedha ni moja kati ya bidhaa iliyomo ndani ya ndoto zako.

Sisemi watu wasitafute fedha, la hasha. Wazitafute, tena kwa bidi, ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia fedha kama moja kati ya nyenzo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Ukweli ni kwamba, fedha daima huwa hazitoshi, hata kama ni nyingi kiasi gani. Kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika. Lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi fulani (satisfaction) hata kama si kwa asilimia 100.

Mwandishi mashuhuri wa vitabu, Myles Munroe, aliwahi kusema kuwa β€œWatu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia, zinawasumbua.”

Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwa sababu hujatimiza ndoto zako, maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia, inampa mahangaiko, mfadhaiko wa kutaifuta.

Kila mtu anapaswa azae, ndoto yako izae, uwezo ulionao uzae. Unaweza kukuzalia mafanikio makubwa, hivyo usikubali kufa na kitu cha thamani kilichoko ndani yako.

Hakuna ndoto kubwa wala ndogo. Fikiria mtu aliyegundua lipstick, leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick, si jambo dogo tena.

Hukuja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha, inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe, ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha.

Tengeneza miundombinu ya fedha na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako, maono yako, kipaji

Angalia utofauti wa mawazo ya maskini na tajiri

MASKINI NA TAJIRI WANA MAWAZO TOFAUTI.
Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo.
Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo.

Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi.
Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.

Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa.
Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.

Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda.
Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.

Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana.
Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.

Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliopita.
Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.

Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani.
Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.

Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa.
Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.

Maskini ana woga.
Tajiri hana woga.

Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha.
Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.

Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi.
Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.

Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa.
Tajiri hutumia pesa kupata pesa.

Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.

Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.

Maskini ana wivu wa chuki.
Tajiri ana wivu wa maendeleo.

Fikiri kama anavyofikiri tajiri.
Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.

#Badilika#
#Shtuka#

Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri

1. Tafuta fursa kila kona.
2. Tumia kipaji chako.
3. Kuwa na nidhamu katika fedha – matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
4. Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote – kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

5. Usipoteze muda – jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.

6. Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.

7. Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

8. Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani – soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

9. Jenga urafiki na taasisi za kifedha – mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha – tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

10. Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.

11. Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo.

12. Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali.

13. Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa – angalia fursa hapo ulipo na wekeza.

14. Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako.

15. Chunguza jamii yako wanakosa bidhaa gani kisha dili na bidhaa hiyo nawe utakuwa milionea.

16. Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

17. Fanya vitu wewe mwenyewe – acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu.

18. Kuwa na malengo – kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.

19. Kuwa na moyo wa ujasiri – usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.

20. Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

21. Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

22. Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

23. Acha woga – jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

24. Kuwa na mtazamo chanya – usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.

25. Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

26. Kuwa na mipaka katika mambo yako – usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu.

27. Dili na watu wenye kipato kidogo na kati katika biashara zako; mamilionea wengi hulenga mahitaji ya watu wa hali ya chini ambao ndio wengi hapa duniani. Baadhi ya mahitaji ya watu wa hali ya chini ni;

(a) Vyakula na vinywaji.
(b) Vifaa vya ujenzi.
(c) Vifaa vya umeme.

28.Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

29. Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako – waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.

30. Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

31. Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe.

32. Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja.

33. Ubunifu ni muhimu sana – fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini – kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

35. Nunua hisa katika mabenki, makampuni mbalimbali: Mamilionea wengi hununua hisa hivyo humiliki mabenki na makampuni mbalimbali.

36. Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli.

37. Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea.

38. Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea – kila binadamu anaweza kuwa milionea.

39. Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa – kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk.

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka🐈,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka🐈 mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka🐈, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao.

Afu wiki
mnayofuatia Mchina anasema bado anataka
Paka🐈, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji
macho yamewatoka, hawana tena paka🐈.
Mchina anasema basi ntaftieni kwa Laki na
Nusu. Keshoake inasikika kuwa kuna Mchagga
anauza Paka kijiji cha pili, anauza kwa
100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta
wanaenda nunua Paka🐈🐈🐈🐈 wote wa kijiji cha
pili. Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana
Mapaka 🐈🐈🐈 wakijua watamuuzia mchina fasta kwa
laki na nusu, Mchina hatokei Ng’oooo!!!!
Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu
na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja
wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji
hiki.
This is what called business strategy.πŸ˜ƒ

Shopping Cart