Author name: SW - Melkisedeck Shine

Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga:

Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati:

Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma:

Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.

Mwanamke kuamka mapema asubuhi kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti

Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti.

Kulingana na shirika la habari la BBC,wataalamu wa chuo kikuu cha Bristol nchini Uingereza wamewafanyia tathmini wanawake 400,000 na kutambua kuwa sio rahisi kwa mwanamke anaeamka asubuhi na mapema kupata saratani ya matiti.

Utafiti huo umeoneysha kuwa wanawake wanaoamka wamechelewa wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ukilinganisha na wale wanaoamka wamechelewa.

Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa kufanya kazi mpaka usiku wa manane kunaongeza hatari ya kupata saratani.

Matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa kwenye Mkutano wa Taifa wa Taasisi ya Utafiti wa Saratani huko Glasgow.

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi. Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule.

Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.

Vifuatavyo ndivyo vyakula vinavyosaidia kupunguza uzito:

Mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi yanapanda chati kwa haraka kabisa na kufanya kuwa mojawapo ya vyakula bora kabisa kwa afya ya binadamu.

Mojawapo ya vitu muhimu kabisa katika mafuta haya ni uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili.

Mafuta ya nazi ni yana kemikali yenye mlolongo wa kati wa mafuta (“Medium Fatty Chain Acids”) ambayo humeng’enywa tofauti na yale yenye mlolongo mrefu wa mafuta (“Long Fatty Chain Acids”)

Kemikali zenye mlolongo mrefu wa mafuta(“Long Fatty Chain Acids”) hupatikana kwa wingi katika vyakula vingi vya mafuta kaa vile nyama, chips n.k.

Kemikali zenye mlolongo wa kati wa mafuta hutumiwa na mwili kwa ajili ya nishati badala ya kuhifadhiwa kama mafuta katika mwili.

Hii ndio sababu mafuta ya nazi ni moja ya vyakula vyenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kusaidia kupungua uzito.

Siki ya Apple (Apple Cider Vinegar)

Siki ya Apple ina kiwango kikubwa cha kemikali za amino (amino acids) ,kemikali za kumeng’enya chakula na madini na vitamini. Utafiti unaonyesha kwamba kutumia Siki ya Apple kabla ya kula vyakula vya wanga inasaidia kupunguza kupanda kwa insulin hivyo kusaidia kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Ndimu na Limao

Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha vitamini C mwilini kinahusiana na uzito wa mwili.

Watu wenye viwango vya kutosha wa vitamini C wana uwezo wa uwezo wa kuvunja asilimia 30 zaidi ya mafuta wakati wa mwili unapofanya shughuli za nguvu kama kazi za nyumbani,shambani na mazoezi kama kutembea, kuliko wale walio na kiwango cha chini cha vitamini C.

Kama una dhamira ya kupungua uzito, basi fikiria kuanza siku yako kwa kunywa glasi moja ya maji yenye ndimu au limao au anza kutumia siki(vinegar) kwenye kachumbali au saladi unapokula chakula.

Balungi

Balungi yana kiasi kidogo cha kalori , kiwango cha juu cha tindikali za kumeng’enya chakula na inaweza kukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu.

Watafiti wamegundua kwamba kula nusu ya balungi kabla ya mlo ni inachangia sana kupoteza uzito . Pia kula nusu tu ya balungi kabla ya mlo inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha glucose-insulin katika muda wa masaa mawili tu.

Kama wewe unahitaji kupungua uzito zingatia kula vyakula vinavyo kata mafuta na ongeza vyakula hivi vilivyotajwa katika mlo wako.

Kwa mafanikio ya muda mrefu , kazania kula vyakula kamili (vyakula visivyo kobolewa au kusindikwa) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka.

Vyakula hivi japo tunavipenda sana lakini vina athari mbaya kwa miili yetu na muhimu kujenga tabia ya kuviacha katika milo yetu. Kama si rahisi kuacha kabisa basi angalau kupunguza matumizi yake.

Vifuatavyo ni vyakula 7 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako:

1. Nyama Nyekundu
Mojawapo ya vyakula vinavyozeesha ngozi ni nyama hasa nyama nyekundu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa nyama nyekundu inayotokana na wanyama kama ng’ombe,mbuzi,kondoo,nguruwe n.k ni mbaya kwa afya njema ya binadamu na hivyo kwa ngozi pia. Nyama nyekundu ina kemikali aina ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi.

Hivyo nyama nyekundu ni mojawapo ya vyakula vibaya kwa afya ya binadamu na vya kuvizuia.

2. Chumvi

Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

3. Sukari

Sukari japo tunaipenda sana ni adui mkubwa wa afya ya binadamu. Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matengenezo ya ngozi kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

Sukari nyingi inasababisha mwili kukosa nguvu ya kupambana na bacteria wabaya. Ongezeko la bacteria hawa kunafanya utengenezwaji wa kemikali mbaya ambazo husababisha uchakavu wa ngozi.

Watu wanashauriwa kutumia sukari asilia kama ya matunda na asali kuliko zile zinazopatikana katika vinywaji kama soda na pipi , jojo,biskuti au vitafunwa vingine vyenye sukari ya kuongeza.

4. Vyakula vya Kukaangwa

Vyakula vya kukaangwa kama chipsi,nyama za kukaanga vinasababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini. Mafuta haya yenye vitu vinavyoitwa “Free Radicals” yanasababisha uzibaji wa vijitundu katika ngozi. Ukiachia ngozi mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

5. Mkate Mweupe,Tambi na Keki

Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa ambayo inaleta madhara ya magonjwa ya ngozi (Ugonjwa wa madoa katika ngozi)

6. Pombe

Unywaji wa pombe unasababhisha kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

7. Kahawa (Caffeine)

Kemikali ya caffeine iliyomo katika kahawa na vinywaji vingine inasababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia uzeekaji wa ngozi.

Badilisha Tabia Yako ya Ulaji

Vyakula hivi ni baadhi ya vingi ambayo vimo katika ulaji wetu wa kila siku na una madhara makubwa kwenye ngozi zetu. Wanawake wanaathirika sana na ngozi ukilinganisha na wanaume. Au niseme wanajali sana ngozi zao kuwa zenye afya na kuvutia kuliko wanaume hivyo wanaweza kufaidika sana kwa kupunguza au kutotumia kabisa hivi vyakula vinavyozeesha ngozi.

Fahamu kuwa afya yako ni mtaji mkubwa hivyo ni kitu muhimu kuipa afya ya mwili wako kipaumbele na hivyo zingatia ulaji wako.

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Yafuatayo ni mambo ya msingi kujua kuhusu uotaji wa meno.

¡Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.

¡Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.

¡Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.

¡Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

¡Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri

Shopping Cart