Angalia huyu house girl wa mzungu alichokifanya na anachokisema
Updated at: 2024-05-25 17:11:31 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani. Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza 'what happened to my plate? House girl akajbu: 'The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjee……the pasuka paaaaaaaa 😂😂😂😂hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
Kilichompata huyu anayependa kusoma SMS za watu kwenye daladala
Updated at: 2024-05-25 17:01:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati…
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyu…. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext: "Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomu💣 lilipuke… najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sana…" Yule jamaa akajirusha dirishani……😂😅
Updated at: 2024-05-25 17:17:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda kisha halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa Google?". Dada: "hapana, kwanini umedhani naitwa hivyo?". Jamaa: "Una kila kitu nnachokitafuta "😅😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
Updated at: 2024-05-25 18:02:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.