Updated at: 2024-05-25 17:05:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, "naomba leseni yako." Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2 Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu! Haya nenda Ulevi sio mzuri 😄😄😄😄
Updated at: 2023-04-29 22:53:40 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..
Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
Updated at: 2024-05-25 17:05:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
……… Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamaha… Ndugu yangu….. Msamehe…. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoa…. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yao…… Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKA…..
Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti
Updated at: 2024-05-25 17:16:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike? MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala MKE: Na lipstiki kwenye shati? MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali? MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani MUME: Umesema nini wewe? MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. 😄😄
Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?
Updated at: 2024-05-25 16:56:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukiona hivyo ujue ndio hivi
Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmh😨😨 hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tu "Huyu.mkaka hapana kwa kweli"🤣🤣🤣🤣🤣🤣