Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali
Kama wewe ni mtu ambaye anatafuta mapenzi ya muda mrefu, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi! Leo tutakufundisha jinsi ya kupata msichana wa kuwa na uhusiano wa mbali. Soma zaidi!
Updated at: 2024-05-25 16:21:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali
Kuwa na uhusiano wa mbali sio rahisi kwa wengi wetu, lakini kama unataka kumpata msichana wa kuwa na uhusiano wa mbali, hapa ni baadhi ya mambo ya kuzingatia.
Kuwa Mtandao wa Kijamii
Kuwa mtandao wa kijamii ni muhimu sana kwa kupata msichana wa kuwa na uhusiano wa mbali. Tumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Twitter, WhatsApp, na Snapchat kumtafuta msichana. Weka picha zako za hivi karibuni na maelezo yako ya kibinafsi.
Kuwa Mtu wa Kuvutia
Msichana atakuwa na hamu ya kukujua vyema zaidi ikiwa utakuwa mtu wa kuvutia. Kwa hiyo, hakikisha unapata muda wa kujifunza mambo mapya mara kwa mara. Fanya mazoezi ya kujenga mwili wako, pata shughuli zinazokufurahisha, tembelea sehemu mpya na ujifunze mambo mapya.
Mwonyeshe Upendo na Kuwajali
Mwonyeshe msichana kwamba unamjali kwa kumtumia ujumbe wa upendo mara kwa mara. Hata kama hamtumii muda mwingi pamoja, hii itamsaidia kujua kwamba wewe unajali kuhusu uhusiano wenu. Kuwa na mazungumzo ya kina na msichana na msikilize kwa makini.
Kuwa Na Mawasiliano Mema
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika uhusiano wa mbali. Hakikisha kuwa una mawasiliano ya kutosha na msichana, weka ratiba ya maongezi yenu, na ushirikiane katika mambo mbalimbali yatakayowakutanisha. Hii itawawezesha kushirikiana katika mambo mbalimbali na kutambua mawazo ya kila mmoja.
Kuwa Mstahimilivu
Uhusiano wa mbali unahitaji uvumilivu na uelewano. Hakikisha kuwa umeelewana na msichana wako kuhusu mambo muhimu yatakayowezesha uhusiano wenu kuendelea. Kumbuka kuwa wewe ni sehemu ya uhusiano huu na unapaswa kutoa nafasi kwa msichana kushiriki katika uhusiano huu.
Kuwa Mkakamavu
Usikate tamaa kwa haraka. Uhusiano wa mbali unaweza kuwa mgumu, lakini unaweza kufanikiwa ikiwa utakuwa mkakamavu. Hakikisha unafanya bidii na kutumia muda wako kuimarisha uhusiano wenu. Mwishowe, usisahau kuwa kuwa na msichana wa kuwa na uhusiano wa mbali ni jambo la kuvutia na litaweka mapenzi yenu kwa kiwango cha juu.
Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?
Updated at: 2024-05-25 16:22:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mvulana hawezi kuthibitisha ubikira wa msichana kwa njia ya kumwangalia wala kwa njia ya kumwingilia kimwili. Hii ni kwa sababu ubikira ni kutowahi kujamii ana na hautegemei kuwepo kwa kizinda ndani ya uke. Yaani msichana ambaye hajawahi kujamii ana, lakini ambaye kizinda chake kimepasuliwa kwa sababu nyingine, bado ni bikira. Njia pekee ya kufahamu kama msichana ni bikira ni kufahamu kile alichofanya maishani, na hii , kwa kweli haiwezekani. Msichana anaweza kujifahamu kuwa bikira kama hajawahi kujamii ana, yaani kuingiliwa kimwili na mwanaume au mvulana. Jamii nyingi hutilia mkazo kuhusu ubikira wa wasichana wakati wa kuolewa. Lakini suala la kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa au kuoa ni muhimu kwa wote, wasichana na wavulana. Kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa kuna maana ya kujiepusha na shida zinazoweza kutokea, kama mimba isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa na hata maambukizi ya VVU na UKIMWI. Iwapo huwezi kustahimili ashiki ya kujamii ana, basi huna budi kuhakikisha kuwa unajikinga wewe na mpenzi wako asipate ujauzito na magonjwa kwa kutumia kondomu.
Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?
Updated at: 2024-05-25 16:23:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupanga kuzaa aina fulani ya mtoto. Tulivyoona juu ni mwanaume ndiye aliye na aina mbili za mbegu. Aina moja husababisha kutokea mtoto wa kike na aina nyingine mtoto wa kiume. Mwanaume hana uwezo wa kuhakikisha achangie aina ya mbegu gani. Kwa hiyo, hata kama ni mwanaume anayeyakinisha jinsia ya mtoto, hana kosa, kwa sababu hana uwezo wa kuamua achangie mbegu ya aina gani.
Je, ni lazima kumeza vidonge vya kuzuia mimba siku zote, hata zile siku nisipojamiiana?
Updated at: 2024-05-25 16:23:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, vidonge vya kuzuia mimba ni lazima vimezwe kila siku hata kama hufanyi ngono siku hiyo. Kuna aina ya vidonge vya kuzuia mimba inayokuja katika pakiti yenye vidonge 21 na kuna inayokuja katika pakiti ya vidonge 28. Iwapo utapewa ile ya vidonge 21 utapumzika kunywa siku 7 katika mwezi. Iwapo utapewa ile ya vidonge 28, itabidi kumeza kidonge kimoja kila siku, hata siku za hedhi. Ili kuhakikisha vidonge vya kuzuia mimba vinafanya kazi sawasawa, mwulize yule aliyekushauri kutumia vidonge hivyo jinsi ya kuvimeza. Kama mwanamke akisahau kunywa kidonge hata kama ni siku moja kuna uwezekano wa kupata mimba. Anaposahau kumeza vidonge, ni vizuri zaidi watumie kondom wakati wa kujamiiana kwa kuhakikisha kutopata mimba. Hii inahusika vilevile kama mwanamke ameharisha au ametapika katika kipindi cha saa 4 tangu ameze vidonge. Kama mwanamke anashindwa kukumbuka kunywa vidonge mara kwa mara, ni vizuri zaidi apate ushauri kutoka kwenye kliniki ya uzazi wa mpango kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba.
Updated at: 2024-05-25 16:23:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, mtu yoyote anayelazimishwa kujamiina atakuwa amebakwa, haijalishi kama mtu huyu ni mwanamke/ msichana, mwanaume au mvulana.
Wavulana na wanaume wanaweza kubakwa na wanaume wenzao au wanaweza kulazimishwa na mwanamke kujihusisha na tendo la kujamiiana. Wanaume wanaweza kulazimisha wavulana kujamiiana kwa njia ya mdomo au njia ya haja kubwa. Kisheria hapa Tanzania tukio kama hili linajulikana kama kulawiti. Matatizo/matokeo ya kulawiti kwa wavulana ni sawa na yale yanayopatikana kwa wasichana. Wavulana wanaweza kuumizwa vibaya zaidi wakati wa kujamiiana na pia kuchanganyikiwa, kiwewe, na kwa wavulana wanapata madhara zaidi. Sheria hapa Tanzania12 haziko wazi juu ya ubakaji kwa wavulana hata hivyo wanatambua mahusiano ya ushoga/ubasha kuwa ni kosa la jinai.
Kwa nini watu wanakuwa wagomvi na wakali wanapokuwa wamelewa?
Updated at: 2024-05-25 16:24:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Madhara ya pombe husababisha watu walioolewa kugombana. Kutokana na ushawishi wa pombe watu hupoteza tabia zao za kawaida na kuona vigumu kuhimili mihemko na kushindwa kufanya maamumzi katika hali hiyo. Matokeo yake, mlevi huyachukulia tofauti mazingira na maneno. Watu waliolewa hukasirishwa haraka na vitu ambavyo wangevipuuza kama wasingekuwa wamelewa. Mara nyingi huwapiga watu wakati wangetatua hali hiyo kwa njia tofauti kama wasingelewa. Kama jambo hili litatokea miongoni mwa rafiki zako au familia, jaribu kuwa mbali na uepuke ulevi. Usijaribu kujadiliana na mtu aliyelewa kwa sababu kwa vyovyote hatakuelewa.
Kufikia mshindo au kufika kileleni kwa mwanamke na mwanamme wakati wa kufanya mapenzi
Updated at: 2024-05-25 16:22:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo?
Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Dalili ya mwanamke kufikia mshindo katika kujamiiana ni ile hali ya pekee ya kujisikia vizuri kimwili. Tofauti na mwanaume, anapofikia mshindo mwanamke hakojoi kitu chochote.
Kwa kawaida mwanaume anakojoa manii wakati wa kujamii ana anapofikia mshindo. Kwa sababu dalili hii ni rahisi kuona baadhi ya watu wanadhani kwamba ni wanaume tu wanaofikia mshindo wakati wa kujamii ana. Lakini hii siyo kweli. Mwanamke pia hufikia mshindo, ingawa siyo rahisi kuuona.
The ListPages module does not work recursively.
Je, kwa nini mwanamke akigongwa na uume kwenye uke yaani juu hutoa majimaji kupitia ukeni?
Kugusana kwa kutumia viungo vya uzazi ni njia mojawapo ya kuamsha hisia ya kujamii ana. Kama mwanamke anatoa majimaji baada ya kugusana na uume kwenye uke, i ina maana kwamba ameshikwa na ashiki kubwa. Majimaji hayo yanarahisisha uume kupenya ukeni. Chanzo cha majimaji hayo ni vifuko maalumu vilivyomo ndani ya uke.
Njia zipi zinaweza kumletea mwanamke mshindo haraka, na zipi zinamletea mwanaume mshindo haraka?
Jambo la msingi kabisa ni kwamba wote wawili kuwa tayari kwa kujamii ana. Yaani kupendana na kujaliana sana, halafu kuwa tayari kwa tendo hilo kimwili, kimawazo na kiakili. Kutokuwa tayari kwa kufanya mapenzi, kwa mfano kwa sababu ya kuogopa ujauzito, inamzuia mtu yeyote kufikia mshindo.
Kama wote wawili mpo tayari, kufikia mshindo au kutofikia kunategemea maandalizi ya awali ya mapenzi.
Mnatakiwa kukubaliana jinsi mtakavyofanya mapenzi i i ili kila mmoja wenu aweze kufurahia na kuridhika. Kwa uhakika, kila mwanamke na mwanaume anazo sehemu maalumu ambazo ukigusa basi ni rahisi sana kufikia mshindo.
Upeo wa hali ya kujamiiana pia unaweza kufikia kwa kupiga punyeto. Kwa mfano, mwanaume anaweza kugusa uume wake au mwanamke anaweza kusugua taratibu kinembe mpaka anafikia mshindo. Kupiga punyeto ni njia i iliyo salama ya kumaliza hamu ya kutaka kufanya mapenzi na haina athari mbaya kiafya.
The ListPages module does not work recursively.
Kwa nini mara nyingi mvulana ni mwepesi sana katika kuanzisha kufanya mapenzi? Na kwa nini mwanaume mara nyingi anafikia mshindo kabla ya mwanamke?
Kwa kawaida i inakubalika kuwa wavulana ndiyo waaanze kuonyesha ishara za kujamiaana na tafiti zimeonyesha kwamba mara nyingi mwanaume anafikia mshindo kabla ya mwanamke. Hii ni ukweli katika sehemu nyingi za dunia.
Baadhi ya wavulana wanatumia vibaya uwezo wao wa kufanya mapenzi. Wanafuatafuata wasichana na kuwatongoza i ili wafanye mapenzi katika umri mdogo. Hata hivyo kujamii ana katika umri mdogo kunaweza kusababisha athari nyingi kama vile mimba isiyotarajiwa au kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Kwa hiyo, wavulana wanashauriwa kuwa wavumilivu licha ya mivuto hiyo ya kutaka kujamii ana, kwa sababu kwa njia ya kujamii ana ovyo mnahatarisha maisha yenu ya baadaye. Kuna njia nyingine za kuonyesha mapenzi, kama vile kubusu, kukumbatia, kushikana mikono na hata kupiga punyeto.
Kimaumbile, mara nyingi mwanaume anafikia mshindo haraka zaidi kuliko mwanamke. Lakini, mkihakikisha kwamba mwanamke ni tayari kwa kujamii ana na kama mmechukua muda wa kutosha kujiaanda vizuri, mnaweza kufikia mshindo pamoja. Hivyo kuwaletea raha na starehe wote wawili.
Updated at: 2024-05-25 16:23:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ya kuvunja ungo (yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza) msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Siku ya kwanza ya hedhi huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka i ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija
wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai. Ina maana kwamba endapo atajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka na kutoka kwenye kokwa, linarutubishwa wakati linaelekea kwenye mji wa mimba, na linapofika hapo kwenye mji wa mimba linatulia kwenye utando wa mji wa mimba. Mtoto anahifadhiwa na kukua ndani ya mji wa uzazi mpaka siku ya kuzaliwa. Kama yai halikurutubishwa, basi yai hufa na hutoka pamoja na utando wa mfuko wa uzazi na hutoka nje ya mwili wa mwanamke kama damu ya hedhi. Yaani, mwanamke atapata hedhi kama kawaida na atafahamu kwamba hajashika mimba.
Updated at: 2024-05-25 16:23:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kike. Ile mbegu inayofika kwenye yai kwanza, inarutubisha yai na ni wakati uleule, jinsia ya mtoto i inatokea. Uwezekano wa kumpata mtoto wa kike au wa kiume unafanana, na hii ni kweli katika nchi zote duniani.
Kwa nini Albino tunaonekana kama mzigo katika familia zetu?
Updated at: 2024-05-25 16:24:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wanaohitaji kupewa uangalizi maalumu wanaweza kuonekana ni mzigo kwa kuwa wanaweza wakawa wanaomba kupewa mahitaji au msaada maalumu tofauti na watu wengine wa kawaida. Wazazi na wanafamilia wengine wanaweza kuchukizwa na matamshi wanaotoa watu wengine pamoja na kulazimika kuvumilia utani na matusi. Ndugu wanapaswa kujua kwa nini ndugu yao Albino ni tofauti na kwa nini anahitaji uangalizi maalumu. Familia ndiyo msingi wa kumwezesha mtoto Albino kujitambua na kukubali hali aliyo nayo. Familia inayoweza kumkubali mtoto wao Albino inaneemeka na kuwa yenye furaha kwa sababu mtoto Albino anakuwa kiungo maalumu katika familia, yaani inaipa familia hali ya kuwa na nguvu yao iliyoungana.