Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Watu wanasema kuwa unaweza kupona UKIMWI kwa kujamiiana na Albino. Hii ni kweli?

Featured Image

Watu wanaweza kuvumisha uongo wowote ili kupotosha
ukweli na kufanya mambo yao maovu wanayoyapenda. Wapo
wanaosema kuwa unaweza kupona UKIMWI kwa kujamiiana na
bikira, mtu mlemavu au Albino, hizi ni imani potofu na hazina
msingi wowote.

Imani hii kuwa kwa kujamiiana na Albino mtu anaweza kupona
VVU / UKIMWI siyo kweli kabisa. Mpaka sasa hakuna tiba
ya UKIMWI ingawa kuna maendeleo makubwa yanayotokana
na dawa za kufubaza VVU (Anti-retrovirals kwa kifupi ARVs).
ARVs zimesaidia watu wengi wanaoishi na VVU kuishi maisha
bora kiafya lakini ARVs haziponyi UKIMWI. Mtu akisha athirika
na VVU ataendelea kuwa na maambukizo kwa maisha yake yote
na hakuna uponyaji wowote unapatikana kwa kujamiiana na
Albino.
Imani hizi potofu pia zinaathiri makundi mengine katika jamii
yetu, kwa mfano; kujamiiana na bikira kunaweza kuponya
UKIMWI, hii imepelekea kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji
wa watoto. Ni muhimu kwa vijana Albino kufahamu ukweli
kuhusu VVU/UKIMWI na pia mila hizi potofu ili waweze
kujikinga.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kumaliza ashiki au hamu ya kufanya mapenzi

Kumaliza ashiki au hamu ya kufanya mapenzi

Kwa vijana mara nyingine siyo rahisi kufahamu afanye nini mara anapopata ashiki (hamu) ya kutaka ... Read More

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha.... Read More

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria ya msingi ya ndoa nchini Tanzania ni Sheria ya ndoa ya
Bunge, iliyopitishwa mwaka 197... Read More

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, ni sahihi kufanya mapenzi na mpenzi wangu wa shule? πŸ€”

Habari vyote vijana! Leo tuta... Read More

Mafuta kwenye kondomu

Mafuta kwenye kondomu

Mafuta yanayowekwa kwenye pakiti ya kondomu ni mafuta maalum na yana kazi ya kuhifadhi kondomu mp... Read More

Je, unajiamini wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, unajiamini wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

  1. Je, unajiamini wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi? Swali hili limewahi kuulizwa ma... Read More

Ubikira ni nini?

Ubikira ni nini?

Maana halisi ya neno β€œbikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj... Read More

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Wakati mwingine ni vigumu kusema hapana ukiwa na
maana ya hapana. Jaribu kuwa mpole na usiwe... Read More

Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Si rahisi kusema ni kitendo kipi kilicho cha kawaida na kisicho cha kawaida. Kulamba ni jambo linalo... Read More
Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Aibu Kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Aibu Kuhusu Ngono?

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Aibu Kuhusu Ngono 🌟

Karibu vijana wenzangu! Leo, tutaj... Read More

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu san... Read More

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Ukitafuta vidokezo vya kukabiliana na ubaguzi katika uhusiano wako na msichana, basi umefika maha... Read More