Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Featured Image

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madha... Read More

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

  1. Kuwasiliana kwa Ukaribu Ha... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuelewa tamaa na mahitaji ya ngono/kufanya mapenzi ya mwenza wako?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa tamaa na mahitaji ya ngono/kufanya mapenzi ya mwenza wako?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa tamaa na mahitaji ya ngono/kufanya mapenzi ya mwenza wako? Ndio! Ni m... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi kuna umuhimu mkubwa sana katika kuha... Read More

Kwa nini siku hizi kuna tofauti ya wanaume katika jamii kuwa wazi/tayari kuwa na uhusiano na wanawake Albino?

Kwa nini siku hizi kuna tofauti ya wanaume katika jamii kuwa wazi/tayari kuwa na uhusiano na wanawake Albino?

Mapenzi ya kweli hayabagui dini, kabila wala rangi. Kwa
kawaida, mapenzi ni matokeo ya hisia... Read More

Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Kila mwanamume anapenda kukutana na msichana ambaye anaweza kuwa rafiki wa karibu na kuwa na uhus... Read More

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Siyo haki kwa mtoa huduma wa afya kukataa kumtibu.
Kama kijana, una haki sawa ya kutibiwa ka... Read More

Magonjwa yatokanayo na sigara

Magonjwa yatokanayo na sigara

Kuna matatizo na magonjwa mengi na ya aina mbalimbali
unayoweza kuyapata kutokana na utuvaji... Read More

Jinsi ya kufanya wazazi wamkubali mchumba

Jinsi ya kufanya wazazi wamkubali mchumba

Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika m... Read More
Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini. Mara nyingine i inasaidia kama utakuwa ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Kama wapenzi wapya au wapenzi wa muda mrefu, ni muhimu sana kujadili matarajio ya ngono/kufanya m... Read More

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Ukitafuta vidokezo vya kukabiliana na ubaguzi katika uhusiano wako na msichana, basi umefika maha... Read More