Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
Dalili
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
· Kushindwa kupumua vizuri
· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
· Kucha kuwa dhaifu
· Kusikia hasira na kuhamasika haraka
· Kuchoka sana kuliko kawaida
· Maumivu makali ya kichwa
· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
· Uchovu wa mara kwa mara
Matibabu.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binada...
Read More
Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.
Unahitaji:
...
Read More
Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mba...
Read More
Barafu inaweza kuzipunguza chunusi zionekane ni ndogo na kupunguza madhara yatokanayo na chunusi....
Read More
BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaout...
Read More
Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vya...
Read More
Nimekutana na hiki kitabu japo nimekipitia juu juu nikaona nisiwe mchoyo Wa kukushirikisha wewe u...
Read More
Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku wat...
Read More
Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua...
Read More
Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata ...
Read More
Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.
Chemsha maji k...
Read More
UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha k...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!