Tatizo la maumivu wakati na baada ya kufanya mapenzi
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia,
Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu za maumivu
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano “vaginal agenesis na imperforate hymen.”
Magonjwa ya kizazi kama “endometriosis, PID,fibroids.”
Sababu za kisaikolojia;
Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubis...
Read More
Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sa...
Read More
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi...
Read More
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.
Lakini inaweza pia kutumika...
Read More
Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binada...
Read More
Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza k...
Read More
Uyoga una vitamini na aina nyingi na madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga n...
Read More
Ugumba ni nini ?
Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito. Ugumba unaweza kua...
Read More
Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana...
Read More
Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mri...
Read More
Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu k...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!