Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufa...
Read More
Mshubiri au Aloe Vera kama ilivyozoeleka na namna nzuri kwa wale wote wanaotaka kubaki na ngozi ...
Read More
Nimekutana na hiki kitabu japo nimekipitia juu juu nikaona nisiwe mchoyo Wa kukushirikisha wewe u...
Read More
Mwili wa binadamu unafanya mambo
mengi ya kibaiolojia ambayo mara
nyingi ni vigumu kuya...
Read More
Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya as...
Read More
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni...
Read More
- Mafuta ya zeituni
- Mafuta ya nazi
- Samaki
- Binzari
- Mayai
Read More
Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapan...
Read More
BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaout...
Read More
Vyakula hivyo ni;
- Maharage
- Nyanya
- Samaki
- Mboga za majani zenye...
Read More
Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal can...
Read More
Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’en...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!