SALA KWA MT. YOSEFU KWA AJILI YA KULIOMBEA KANISA LA MAHUJAJI
Ee Mtukufu Mt. Yosefu, ulichaguliwa na Mungu kuwa Baba Mlishi wa Yesu, mchumba safi kabisa wa Maria Bikira Milele, na mkubwa wa Familia Takatifu. Umechaguliwa na Mwakilishi wa Kristu kama Msimamizi wa kimbingu na mlinzi wa Kanisa alilolianzisha Kristu. Ndiyo maana ninakuomba kwa matumaini makuu usaidizi wako wenye nguvu kwa ajili ya Kanisa zima duniani.
Updated at: 2024-05-27 07:14:02 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mtukufu Mt. Yosefu, ulichaguliwa na Mungu kuwa Baba Mlishi wa Yesu, mchumba safi kabisa wa Maria Bikira Milele, na mkubwa wa Familia Takatifu. Umechaguliwa na Mwakilishi wa Kristu kama Msimamizi wa kimbingu na mlinzi wa Kanisa alilolianzisha Kristu. Ndiyo maana ninakuomba kwa matumaini makuu usaidizi wako wenye nguvu kwa ajili ya Kanisa zima duniani.
Mlinde kwa namna ya pekee, kwa upendo wa kikweli wa ki-baba, Baba Mtakatifu na Maaskofu wote na Mapadre wenye ushirika na Kiti cha Petro. Uwe mlinzi wao wote wanaotumikia wokovu wa wanadamu kati ya majaribu na mahangaiko ya maisha haya, na utujalie kwamba watu wote wa dunia hii wamfuate Kristu na Kanisa alilolianzisha.
Mpendwa Mtakatifu Yosefu, ukubali majitoleo ya nafsi yangu ambayo sasa ninafanya. Ninajiweka wakfu kwako kwa ajili ya utumishi wako, ili daima wewe uwe baba yangu, mlinzi wangu, na kiongozi wangu katika njia ya wokovu. Unijalie usafi mkuu wa moyo na matamanio makuu ya maisha ya kiroho. Unijalie ili matendo yangu yote, kwa mfano wako, yawe kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu, pamoja na Moyo wa kimungu wa Yesu, moyo safi wa Maria, na moyo wako wa ki-baba. Uniombee, nami nishiriki kifo chako cha furaha na kitakatifu. Amina.
Sali Atukuzwe 7 kwa heshima ya Malaika 7 wateule ujipatie neema ya kuepa dhambi mbaya saba na kutujaza mapaji saba ya Roho Mtakatifu.
Updated at: 2024-05-27 07:14:25 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Sali Atukuzwe 7 kwa heshima ya Malaika 7 wateule ujipatie neema ya kuepa dhambi mbaya saba na kutujaza mapaji saba ya Roho Mtakatifu.
TUOMBE Ee Mungu Mwenyezi wa milele, kwa wema na huruma yako ya ajabu, umetaka watu wako waokoke, ukamweka Malaika Mkuu Mikaeli kuwa Mkuu wa Kanisa lako, Utukinge na adui zetu, wasitusmbue saa ya kufa kwetu, bali tuongozwe naye kwenye utukufu wako Mkuu. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana Wetu Yesu Kristo. Amina.
Utuombee Ee Mtukufu Mtakatifu Mikaeli Mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo, tujaliwe ahadi za Kristo. Amina.
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu.
Updated at: 2024-05-27 07:13:57 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. Nakuomba, ee Mama, uniombee daima kwa Mwana wako, najua hawezi kukuvyima wewe kitu chochote. Basi, ufanye, Moyo wa Mwanao ukubali kunijalia ombi langu hili …………………(taja ombi lako). Maana nitamkimbilia nani katika mahitaji na misiba yangu isipokuwa kwako, ee Mama wa huruma? Wewe hasa unaweza kutusaidia sisi tulio bado katika bonde la machozi kwa sababu ulishiriki mateso ya Mwanao kutukomboa. Umtolee Yesu tone moja la Damu yake takatifu. Umkumbushe ya kuwa wewe ni matumaini, furaha na maisha yetu ukanipatie jambo ninalokuomba kwa Yesu Kristo, bwana wetu. Amina.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma; Kwani ndiwe uliyefundisha hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina
Updated at: 2024-05-27 07:13:46 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu wangu,
nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma;
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako. Ee Mlinzi amini wa Jamaa Takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo, ee Baba uliyetupenda mno, utuepusha na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji,utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwokoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi, ulikinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote, mtunze daima kila mmoja wetu, tupate mfano wako, tusaidie kwa msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupokelewa mbinguni makao ya raha milele. Amina
SALA YA KUUABUDU MOYO MTAKATIFU WA YESU KATIKA EKARISTI TAKATIFU
Kwa nguvu zangu zote za moyo wangu/ ninakuabudu ee Moyo Mtakatifu/ na Mwabudiwa sana,/ Moyo Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristu/ ambao ninataka kumpenda/ na kukusalimu kwa usikivu unaoendelea./ Kamwe nisikuudhi tena/ kwa sababu Wewe ni Mwema sana;/ Ee Mwema sana./ Ee Moyo Mtakatifu sana/ ninakupenda/ na ninataka kukupenda zaidi ya vitu vyote,/ kwa
Updated at: 2024-05-27 07:13:58 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa nguvu zangu zote za moyo wangu/ ninakuabudu ee Moyo Mtakatifu/ na Mwabudiwa sana,/ Moyo Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristu/ ambao ninataka kumpenda/ na kukusalimu kwa usikivu unaoendelea./ Kamwe nisikuudhi tena/ kwa sababu Wewe ni Mwema sana;/ Ee Mwema sana./ Ee Moyo Mtakatifu sana/ ninakupenda/ na ninataka kukupenda zaidi ya vitu vyote,/ kwa nguvu zangu zote/ na kwa uwezo wangu wote,/ ninatamani kuwa mali yako/ Wewe uliyejitoa Msalabani kwa ajili yangu/ kwa mateso makali./ Unionee huruma na udhaifu wangu/ na usiniruhusu kupotea./
Ninajitoa kabisa kwako/ ee moyo wa mapendo,/ kwa makusudi kuwa utu wangu,/ maisha na mateso yangu/ yalipie kukupenda,/ kukuheshimu/ na kukutukuza Wewe sasa na milele./ Ninakupenda ee Moyo Mwabudiwa wa Mwokozi wangu,/ ninakuomba kwako/ uamuru moyo wangu na kila kitu ndani yangu/ kikutukuze sasa na milele./ Amina.
Roho ya Kristo unitakase Mwili wa Kristo uniokoe Damu ya Kristo unifurahishe Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie Ee Yesu mwema unisikilize
Updated at: 2024-05-27 07:13:49 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Roho ya Kristo unitakase Mwili wa Kristo uniokoe Damu ya Kristo unifurahishe Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie Ee Yesu mwema unisikilize Katika madonda yako unifiche Usikubali nitengwe nawe Na adui mwovu unikinge Saa ya kufa kwangu uniite Uniamuru kwako nije Na watakatifu wako nikutukuze Milele na milele. Amina.
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”
Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au; “Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……” Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Baba yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe Ufalme wako ufike Utakalo lifanyike Duniani kama mbinguni Utupe leo mkate wetu wa kila siku Utusamehe makosa yetu Kama tunavyowasamehe Na sisi waliotukosea Usitutie katika kishawishi Lakini utuopoe maovuni. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:24 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Baba yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe Ufalme wako ufike Utakalo lifanyike Duniani kama mbinguni Utupe leo mkate wetu wa kila siku Utusamehe makosa yetu Kama tunavyowasamehe Na sisi waliotukosea Usitutie katika kishawishi Lakini utuopoe maovuni. Amina.