Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?
Updated at: 2024-05-25 16:24:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Matumizi mabaya ya pombe ndiyo yanayosababisha kuenea kwa VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana. Tabia ya ulevi ya kupindukia huwaweka watu katika hatari kubwa ya kupata na kueneza magonjwa haya. Pombe husababisha watu kusahau hatari ya kuwa na wapenzi wengi na pia kufanya mapenzi na watu ambao hawafahamu hali za afya zao. Husahau kujilinda wao wenyewe na wapenzi wao, kwa kutumia kondomu na kusahau majukumu yao ya familia.
Watu wanaokunywa pombe kupita kiasi hudhoofisha mfumo wa kinga mwilini, hivyo basi, virusi huingia miilini mwao kirahisi. Kumbuka, bado hakuna tiba ya UKIMWI. Njia pekee ya kinga ni kubadili tabia.
Je, Albino abadili/ageuze nywele rangi (die) au avae nywele bandia (wigi)?
Updated at: 2024-05-25 16:24:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Suala hili litatagemea na kila mtu anavyopendelea. Baadhi ya watu hupendelea kuacha nywele zao katika hali asilia kama walivyozaliwa, wengine wanapendelea kuzigeuza rangi kuwa nyeupe au nyeusi na wengine wanapendelea kuvaa nywele bandia zenye rangi nyeusi, kahawia au nyeupe. Jambo la msingi ni wewe kujisikia vizuri. Kwa kadri unavyojisikia vizuri ni ndivyo utakavyojiamini na ukijipenda na wengine watakupenda.
Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?
Updated at: 2024-05-25 16:22:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madhara yatakayokutokea kwenye sehemu zako za siri au katika sehemu nyingine ya mwili wako. Mwanaume au mwanamke akianza kujamii ana baada ya kukaa muda mrefu, atapata raha na starehe.
Watu wengine wanasema kwamba kutofanya mapenzi kunasababisha kuwa na chunusi usoni au sehemu za siri, au hata kuchanganyikiwa kiakili. Siyo kweli kwamba hali hizi zinasababishwa kwa kutojamii ana, vyanzo vya hali hizi ni tofauti. Uwe na uhakika kwamba kutojamii ana ni salama kabisa kwako na huwezi kupata madhara yoyote. Lakini kama tulivyosema awali, kujamii ana kunaweza kukaleta matatizo mengi kama mimba i isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI.
Updated at: 2024-05-25 16:22:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna aina mbalimbali za ulemavu na kuna sababu mbalimbali za kuzaa mtoto mlemavu. Ulemavu wa mtoto unaweza kuwa wa kurithi au ukatokea katika hatua tofauti wakati mimba inakuwa, kama vile , wakati wa utungaji mimba, wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaa.
Baadhi ya ulemavu ni kwa sababau ya hitilafu ya kinasaba (jenetiki) ambayo tayari i i inajulikana kwenye familia, au inayojitokeza ghafla. Hii ni aina ya ulemavu ambao hauwezi kuzuilika. Ili mimba i iweze kutungwa, kuna mlolongo wa mambo mengi ambayo yanatakiwa yatokee wakati mwafaka. Ule mwenendo wa kujiunga yai lililopevuka likutane na mbegu ya kiume siyo kitu rahisi na i inawezekana yakatokea makosa. Makosa kama hayo siyo rahisi kuyazuia na mara nyingi kutokea kwake ni kwa bahati mbaya. Sababu mojawapo ni mwanamke kuumwa wakati wa ujauzito. Kama mwanamke mjamzito anaumwa kwa mfano, malaria na anakunywa madawa makali, ugonjwa wenyewe au matumizi ya dawa yanaweza kuleta madhara kwa mimba i inayokua tumboni. Malaria ni ugonjwa mmojawapo unaosababisha mimba kutoka na ulemavu kwa watoto wanaozaliwa. Wanawake wanashauriwa kuwa wangalifu sana wasiugue malaria wakati wa ujauzito. Sababu nyingine ni matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na sigara au pombe wakati wa ujauzito. Vitu hivi sio vizuri kwa mwili wa binadamu, hasa kwa mimba. Wakati mwingine, ulemavu wa mtoto unatokea wakati wa kuzaliwa. Kwa hiyo ni muhimu sana mwanamke ahakikishe anahudumiwa na mhudumu mwenye ujuzi wa kutosha ambaye anayajua madhara na namna ya kukabiliana nayo.
Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?
Updated at: 2024-05-25 16:22:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni. Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini sana na uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamii ana ni mkubwa, kwa sababu hakuna majimaji kama ukeni yanoyorahisisha uume kuingia. Kwahiyo virusi vya UKIMWI ni rahisi sana kuingia mwilini mwa mwanamke kupitia kwenye michubuko hii .. Pia ngono kwa njia ya mdomoni ( โkula koni, chumvi chumvi , kulamba ukeni) hatari sana kama mwanamke ana vidonda au michubuko mdomoni na mwanaume au vidonda au michubuko uumeni, wanaweza kuambukizana. Watu wote wanashauriwa kutumia kondomu i ili kuzuia maambukizi.