Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Featured Image

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Upendo kwa Msichana Wako kila Siku

Jinsi ya Kuonyesha Upendo kwa Msichana Wako kila Siku

Wewe ni mpenzi mzuri na unapenda msichana wako kwa dhati. Lakini je, unamwonyesha upendo kila sik... Read More

Umri unaofaa kuoa

Umri unaofaa kuoa

Kuoana maana yake ni kuwajibika kwa maisha yako na mke au mume wako. Mara nyingi kuoana kunaambatana... Read More
Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Kumwonyesha shukrani msichana wako ni njia moja ya kumfanya ajisikie muhimu na kupendwa. Kwa hiyo... Read More

Njia za Kufanya Msichana Amevutiwa na Wewe kwa Muda Mrefu

Njia za Kufanya Msichana Amevutiwa na Wewe kwa Muda Mrefu

Habari wapendwa, leo tutazungumzia njia za kufanya msichana amevutiwa na wewe kwa muda mrefu. Kun... Read More

Kwa nini jamii inatuchukia sisi Albino?

Kwa nini jamii inatuchukia sisi Albino?

Siyo watu wote katika jamii wanawachukia au kuwatenga Albino.
Wazazi, ndugu zenu, rafiki zen... Read More

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Ipo njia moja ya kuhakikisha kama umeambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au hapana. Njia hii ni... Read More

Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?

Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?

Ndiyo msichana anaweza kupata mimba kwa kujamiiana mara
moja tu bila kujali ana rangi gani y... Read More

Jinsi ya Kutambua Ishara za Upendo kutoka kwa Msichana

Jinsi ya Kutambua Ishara za Upendo kutoka kwa Msichana

Upendo ni hisia ambazo zinafanya maisha kuwa na maana zaidi. Kila mtu anapaswa kupata upendo, na ... Read More

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu san... Read More

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake... Read More

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria ya msingi ya ndoa nchini Tanzania ni Sheria ya ndoa ya
Bunge, iliyopitishwa mwaka 197... Read More