Kwa nini hairuhususiwi kuotesha au kuvuta bangi, iwapo kupanda na kuvuta tumbaku kunaruhusiwa?
Updated at: 2024-05-25 16:24:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali. Tumbaku imekubalika na jamii kwa muda mrefu, na ni katika miaka kama hamsini iliyopita ndipo madhara yatakanayo na nikotini iliyomo kwenye tumbaku yalipoanza kukubalika. Hata hivyo, hadi sasa tumbaku ni halali, lakini ni bangi kwa upande mwingine si halali kisheria Tanzania. Kwa hivyo, kutokana na kwamba nikotini kwenye sigara ina madhara, basi serikali ilichukua hatua ya kuanza kuwatahadhadharisha wavutaji na kuwazuia vijana kuvuta sigara. Kuna sheria mpya Tanzania ambayo inawalazimisha watengenezaji wa bidhaa za tumbaku kuandika tahadhari ya afya kwenye bidhaa wanazotengeneza na kuuza. Kuanzia mwaka 2000 bidhaa za tumbaku zote zililazimika kuwa na onyo kwamba “Uvutuaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.”
Updated at: 2024-05-25 16:24:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wenye ualbino hawana uwezo kabisa au wana uwezo mdogo
wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele na macho. Rangi hii
huitwa “melanini”. Rangi ya ngozi itategemeana na kiasi cha
melanini kilichopo. Hali ya kuzalisha melanini imekaa katika
vinasaba vyetu. Kama vinasaba vya kutoa melanini havipo au
vimebadilishwa madhara yake ni ukosefu au upungufu wa rangi.
Kwa hiyo hali ya ualbino ni ya kurithi. Inaweza kurithishwa
kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto.
Je, kuwa kuna mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono/kufanya mapenzi?
Mapenzi ni raha tele, lakini kuna mambo ambayo ni bora kutofikiria kabisa! Je, umewahi kusikia juu ya kiharusi cha ngono? Hapana! Hapa kuna mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono/kufanya mapenzi.
Updated at: 2024-05-25 16:18:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Habari yako, mpenzi! Katika mada ya leo, tunajadili kuhusu mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono au kufanya mapenzi. Ingawa ngono ni sehemu muhimu ya maisha ya kimapenzi, kuna mambo ambayo ni bora kuyaelewa na kuyaelezea kwa uwazi na waziwazi. Kwa hiyo, hebu tuanze!
Upungufu wa nguvu za kiume
Hii ni mojawapo ya mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono. Kama mpenzi wako ana upungufu wa nguvu za kiume, ni bora kumshawishi kumwona daktari badala ya kuzungumza naye kwa dharau au kumhukumu. Ni muhimu kwa watu wote kuelewa kwamba upungufu wa nguvu za kiume siyo kitu cha kudhalilisha na kwamba linaweza kusababishwa na mambo mengi ya kiafya.
Mawasiliano ya simu
Wakati wa tendo la ndoa, ni muhimu kuwa na mawasiliano ya kina na mpenzi wako, lakini ni bora kuacha mawasiliano ya simu wakati huo. Ni bora kuacha simu zako pembeni na kujitolea kikamilifu kwa mpenzi wako. Wakati wa tendo la ndoa, hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kujitolea kwa kila mmoja na kufurahia kila wakati wa kushiriki.
Mipaka ya kibinafsi
Kuna mambo ambayo huwa hayafai kuzungumziwa kati ya wapenzi. Ni muhimu kuheshimu mipaka ya kibinafsi ya kila mmoja wenu. Kila mtu ana mipaka tofauti, hivyo ni muhimu kuongea pamoja na kujua mipaka ya kila mmoja.
Mambo ya kibinafsi
Mambo ya kibinafsi kama vile matatizo ya uzazi, historia ya kimapenzi, na masuala mengine ya kibinafsi hayafai kuzungumziwa hadharani. Ni muhimu kwa wapenzi kufahamu mipaka ya kibinafsi na kuzungumzia mambo kwa uwazi pekee wakati wamejipanga vizuri.
Fadhila za kimapenzi
Kufanya mapenzi ni suala la kibinafsi kabisa, hivyo ni muhimu kuacha kuzungumza kuhusu fadhila za kimapenzi na wengine. Ni muhimu kuwa na mawasiliano bora kati ya wapenzi na kushiriki vitu vya kibinafsi na mpenzi wako.
Maslahi ya kifedha
Ngono ni sehemu muhimu ya maisha ya kimapenzi, lakini maslahi ya kifedha hayafai kutajwa. Mambo kama kulipa au kupokea pesa kwa ajili ya ngono ni mambo ambayo yanapaswa kukwepwa. Kupata pesa kwa ajili ya ngono ni ukahaba na hukualeta madhara kwa pande zote mbili.
Kuzungumza kwa dharau
Kuzungumza kwa dharau na kupuuza hisia za mpenzi wako kunaweza kuharibu uhusiano wenu. Kila mmoja anapaswa kuzungumza kwa uwazi na kwa kujali maoni ya mwenzi wako. Inapasa kuwa na majadiliano yatakayosaidia kuboresha uhusiano wenu.
Ngono na afya
Ingawa ngono ni sehemu muhimu ya maisha ya kimapenzi, ni bora kuzingatia afya na usalama. Ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya mipira ya kiume na kujua afya yako kwa ujumla. Mipira ya kiume inasaidia kuepuka magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.
Kujadili kuhusu wapenzi wa zamani
Ni bora kuepuka kuzungumza kuhusu wapenzi wa zamani wa mpenzi wako. Hii inaweza kusababisha kutoaminiana na kutokuelewana. Kila mmoja anapaswa kuzingatia sifa na tabia za mwenzi wako kwa wakati huu na kujenga uhusiano bora bila kizingiti cha zamani.
Kuzungumza kwa uwazi
Ni muhimu kuzungumza kwa uwazi na mpenzi wako kuhusu mambo yanayohusu ngono au kufanya mapenzi. Ni vizuri kuwa na mawasiliano bora kwa kila mmoja ili kuelewa hisia, mipaka na matarajio ya mpenzi wako. Kuzungumza kwa uwazi ni hatua muhimu katika kujenga uhusiano bora na wenye nguvu.
Kwa kumalizia, mambo yoyote kuhusu ngono hayafai kuzungumziwa hadharani au kwa watu wengine. Ni bora kuwa na mawasiliano bora na mpenzi wako, kuheshimiana na kuelewa mipaka ya kila mmoja. Tambua kwamba ngono ni sehemu muhimu ya maisha ya kimapenzi, lakini afya na usalama kwanza. Hivyo, endelea kufurahia tendo la ndoa na mpenzi wako kwa njia salama na yenye furaha. Je, unasemaje kuhusu mada hii? Nipe maoni yako!
Updated at: 2024-05-25 16:22:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au kutokana na madhara ya muda mrefu katika viungo vya ndani ya mwili kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Watu wengi hufa katika ajali pale wanapokuwa wana kiasi kikubwa cha kilevi katika damu, kwani wanashindwa kutambua mazingira ya hatari. Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza akafa ghafla kwa kile kinachoitwa kuzidisha dawa, pale mtu atakapotumia dawa za kulevya zaidi ya uwezo wa mwili. Kifo cha ghafla kinaweza kutokea au kutokana na matumizi ya kokaini na vifukishi kama petroli bila hata ya kuzidisha kiwango. Watumiaji wa vifukishi kama petroli mara nyingi hutumia mifuko ya plastiki i i ili kuongeza kiwango cha mvuke wanaovuta. Katika mazingira haya ni rahisi kupoteza fahamu kutokana na kukoseshwa hewa na mifuko hiyo. Kuchanganya baadhi ya dawa za kulevya kama vile heroini na dawa zingine hasa dawa za kutuliza maumivu (mfano valium) au pombe pia huweza kusababisha kifo.
Updated at: 2024-05-25 16:23:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo. Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi. Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni. Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo. Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.
Je, ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokananyo na kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji?
Updated at: 2024-05-25 16:24:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Uvutaji wa aina zote una madhara. Kama utavuta sigara na kuvuta moshi kwa kutumia mdomo hadi kwenye mapafu yako utapata madhara moja kwa moja kwenye viungo vyako. Kama nitasimama karibu na mvutaji na kuvuta moshi, kuna madhara ambayo siyo ya moja kwa moja. Kwa upande mwingine kama jirani wa mvutaji unaweza kuvuta sumu nyingi itokanayo na tumbaku kwa sababu hakuna kitu cha kuichuja. Sigara za viwandani zina kishungi ambacho huchuja tindikali mbalimbali zenye sumu, kama vile kaboni na asidi ya magamba ya miti, ambazo zina madhara kwa mapafu.
Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?
Updated at: 2024-05-25 16:22:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwanaume. Zamani, watu walimtambua msichana bikira kwa njia ya kuhakikisha kwamba kile kiwambo chembamba ndani ya uke kipo. Lakini kwa sababu ngozi hii huweza kuchanika kwa njia nyingine zaidi ya kujamii ana, siyo kipimo kizuri cha kumtambua msichana ambaye hajajamii ana kabisa (yaani bikira). Katika jamii nyingi ni kawaida kuwaita `bikira` wanawake ambao hawajawahi kujamii ana. Pia, jamii nyingi wanasisitiza umuhimu wa mwanamke kuwa bikira mpaka siku ya kuolewa. Hata hivyo, neno “bikira” hutumiwa kwa wanawake na wanaume.
Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?
Updated at: 2024-05-25 16:24:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo msichana anaweza kupata mimba kwa kujamiiana mara moja tu bila kujali ana rangi gani ya ngozi. Wasichana weupe, weusi na wanaoishi na ualbino au wasio na ulemavu wa ngozi wanafanana wote inapokuja kwenye suala la uwezekano wa kupata mimba. Kinachobainisha/ kinachosababisha upatikanaji wa mimba ni wakati tendo la kujamiiana linapofanywa na hatua ya mzunguko wa hedhi. Kama yai lililopevuka kwa ajili ya kurutubishwa litakuwa tayari basi ujauzito utatokea mara tu baada ya mbegu ya mwanaume kuingia, (wakati wa kujamiiana). Ujauzito unaweza kutokea hata kama msichana alikuwa bado bikira na ni mara yake ya kwanza kujamiiana.
Nikitumia nyembe kali au sindano pamoja na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI ninaweza kupata Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?
Updated at: 2024-05-25 16:22:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, unaweza kuambukizwa ukitumia nyembe kali au sindano kwa kuchangia pamoja na mtu mwenye virusi i vya UKIMWI. Matumizi ya vyombo vyenye makali, kama sindano, visu au nyembe yana hatari. Kama baada ya kutumika damu husalia katika vyombo hivi, na endapo vitatumika bila kutakaswa au kuchemshwa, matumizi yake yanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali, pamoja na UKIMWI. Kwa hiyo ni muhimu sana kutochangia vifaa vyenye makali na watu wengine au lazima kuvitakasa na kuchemsha kila baada ya kuvitumia.
Je, mtu anaweza kuambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI iwapo atavaliana nguo na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?
Updated at: 2024-05-25 16:22:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapana, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI hauambukizwi kwa kuvaliana nguo na mgonjwa, kwa sababu vijidudu vya UKIMWI vinakufa baada ya muda mfupi vikiwa hewani. Hata hivyo, kufuatana na kanuni za usafi, ni vizuri zaidi kuvaa nguo zilizofuliwa na kupigwa pasi.