Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kidali cha kuku 1 kikubwa Swaum,tangawizi 1 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Curry powder 1/2 kijiko Paprika 1/2 kijiko cha chai Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Kitunguu 1/2 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Katakata kuku ktk vipande vya mishkaki ya kawaida kisha vimarinate na vitu vyote, kasoro hoho na kitunguu.Ni vizuri kuziacha either usiku mzima au kwa masaa machache ili spice ziingie vizuri. Baada ya hapo katakata hoho na vitunguu vipande vya wastani kiasi. Baada ya hapo Taarisha vijiti vya mishkaki kisha tunga nyama pamoja na hoho na vitunguu kisha nyunyuzia mafuta na kisha uzichome kama mishkaki ya kawaida. Itakapoiva itakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama ndizi za kuchoma, viazi na n.k.
Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2
Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo - 2 vikombe
Nazi iliyokunwa - ½ Kikombe
Chokoleti vipande vipande - 1 Kikombe
Njugu vipande vipande - ½ Kikombe
Siagi - 227 g
MAPISHI
Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti. Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ºC kwa dakika 20. Katakata tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maini ya kuku 1/2 kilo Vitunguu vikubwa 2 Hoho 1 Pilipil 1 Limao 1/2 Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai Curry powder 1/2 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai) Hamira (yeast kijiko 1 cha chai) Sukari (sugar 2 vikombe vya chai) Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji kikombe1 na 1/2 Mafuta
Matayarisho
Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO VYA SAMAKI
Samaki wa sea bass vipande - 1 1/2 LB (Ratili) Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai Bizari ya manjano au ya pilau - 1/2 Kijiko cha chai Paprika ya unga au pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai Chumvi - Kiasi Ndimu Mafuta - 3 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
Washa oven moto wa 400F. Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri. Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA
Gwaru (green beans) - 1 LB Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu Karoti - 4-5 Chumvi - Kiasi Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai Pilipili manga - 1/4 kijiko cha chai Mafuta ya zaituni - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika. Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga. Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.
Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga kikombe 1 ½
Siagi ½ kikombe
Sukari ½ kikombe
Yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Jam ya peach na raspberry
MAANDALIZI
Wash oven moto wa takriban 180 – 190 Deg F Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla. Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon). Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam. Panga katika treya uliyopakaza siagi. Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light. Epua vikiwa tayari
Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Wali:
Mchele mpunga - 4 Vikombe
Tui la nazi - 6 vikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando. Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi. Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.
Maharage Ya Nazi
Maharage - 3 vikombe
Tui la nazi zito - 1 kikombe
Tui la nazi jepesi - 1 kikombe
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa -1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha maharage mpaka yaive. Katiakatia kitunguu maji na tia thomu, tia na tui jepesi kikombe kimoja. Tia tui zito endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi yakaribie kukauka yakiwa tayari.
Samaki Nguru Wa Kukaanga
Samaki Wa Nguru - 4 vipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) & tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 4
Ndimu - 2 kamua
Bizari ya samaki -1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki. Mwache akolee viungo kwa muda kidogo. Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Hoho la kiajani 1/2 Njegere 1 kikombe cha chai Carrot 1 kubwa Broccoli kidogo Cauliflower kidogo Kitunguu 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry power 1 kijiko cha chakula Coriander powder 1 kijiko cha chai Tarmaric 1/2 kijiko cha chai Olive oil Chumvi 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele 2 vikombe vya chai Choroko kikombe 1 na 1/2 Nazi kopo 1 Swaum 1 kijiko cha chakula Kitunguu 1 kikubwa Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai Chumvi Mafuta
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima, pindi ukianza kupika loweka mchele nusu saa kisha katika sufuria kubwa, kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia swaum na binzari nyembamba kisha tia choroko, mchele, chumvi,nazi na maji mengi kiasi yakuivisha choroko pamoja na mchele. Pika mpaka vitu vyote viive na viwe vilaini kisha upondeponde kiasi.Baada ya mseto wako kuiva utakuwa unaonekana kama uji wa mchele vile. Na Baada ya hapo mseto wako utakuwa tayari kwa kuliwa na mboga yoyote uipendayo.Inapendeza zaidi kuliwa vile tu ukishamalizwa kupikwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 4 Vikombe vya chai Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai Baking powder - 2 Vijiko vya chai Mayai - 2 Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai Vanilla -1 Kijiko cha chai Maziwa ya kuchanganyia - kiasi Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe
MAANDALIZI
Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika. Vumbika (bake) moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.