Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo
Updated at: 2024-05-25 10:35:04 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili. Tatizo hili hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu kama mbuzi hilo ni tatizo kwako. Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha kama atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo.Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria.
Updated at: 2024-05-25 10:35:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nichukue wasaa huu kukuarika rasmi ewe mpenzi na mfuatiliaji wa blog hii ya Muungwana blog, naomba nichukue walau dakika zako chache niweze kukueleza kinagaubaga ni kwa jinsi gani unaweza kupunguza mwili wako kwa kutumia hatua zifuatavyo:
Updated at: 2024-05-25 10:35:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.
Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.
·Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
·Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.
·Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
·Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote
·Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri
Updated at: 2024-05-25 10:35:25 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuwa watoto wazazi wao walivuta sigara mbele yao,wana hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na maradhi ya mapafu.
Watafiti wanasema kati ya watu laki moja ,watu saba hufa kila mwaka kutokana na madhara ya sigara waliyoyapata wakiwa watoto.
Watalamu wanasema kinga bora zaidi ya kuzuia watoto kutoathirika na sigara ni wazazi kuacha kuvutaji sigara kabisa.
Aidha utafiti huo umebainisha kwamba sio watoto peke yake ndio wanaweza kuathiriwa na sigara bali hata mtu mzima ambaye havuti sigara lakini anaishi au anakuwa karibu na mtu anayevuta sigara.
Moshi wa sigara wa saa 10 au zaidi kwa kila wiki unaongeza hatari ya vifo vya ugonjwa wa moyo kwa asilimia 27,kupooza kwa asilimia 23 na madhara katika mapafu kwa asilimia 42 ukilinganisha na wale ambao wanaishi na watu wasiovuta sigara.
Utafitit huu ambao umechapishwa kwenye jarida la ' Preventive Medicine' uliwauliza watu kuhusu uvutaji sigara katika maisha yao na wanayaangaliaje maisha yao baada ya miaka 22.
Kumekuwa na kampeni ya kuwazuia watu kuvuta sigara katika maeneo ya ndani ili watoto au watu wasiovuta wasiathirike lakini maeneo maalum ya kuvuta sigara yanaonekana kuwa ni machace bado na njia pekee inayoweza kusaidia madhara yasiwepo ni watu kuacha kabisa uvutwaji sigara.
Dr Nick Hopkinson ambaye ni mshauri wa masuala ya afya kutoka taasisi ya mapafu nchini Uingereza 'the British Lung Foundation, agreed, saying' anasema kuwa kuna madhara makubwa ambayo mtoto anaweza kuyapata anapovuta moshi wa sigara.
Ni vyema kwa wazazi ambao wana watoto wadogo au wanawake wajawazito kupata msaada wa kuacha kuvuta sigara.
Sigara ina madhara yanayohatarisha Maisha
Watoto ambao wazazi wao wanavuta sigara wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata mangojwa kama ya pumu na athari katika mapafu. Utafiti unaonesha kuwa madhara ya uvutaji wa sigara kwa watoto uonekana pale anapokuwa mtu mzima.
Vilevile madhara ya sigara yanaweza kusababisha ongezeko la magonjwa sugu na maisha ya utegemezi hapo badae.
Updated at: 2024-05-25 10:35:01 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Updated at: 2024-05-25 10:35:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu. Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer
Updated at: 2024-05-25 10:35:00 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume.
Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebaini kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kina mama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.
“Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kina baba… vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenzi wao,” mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es Salam aliiambia Nipashe.
Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni, alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuiamrisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana, na hasa Zinc.
Alisema ni kwa sababu hiyo, anaamini ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa ni kina mama.
“Kuna uvumi mwingi kuhusu faida za mihogo mibichi na nazi kavu kwa wanaume. Wengi huhusisha na masuala ya tendo la ndoa…ukweli ni kwamba wanaozungumzia suala hilo wako sahihi ingawa wanaweza kuwa siyo wataalamu.
Vitu hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu,” alisema Mgeni.
Alisema zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho.
MUUJIZA ZAIDI
Dokta John Kimai wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam alisema ni kweli mihogo mibichi na nazi mbata husaidia kuiamrisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.
Aidha, alisema faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho ‘lauric acid’.
Alisema faida nyingine ya nazi mbata ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides – MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.
Aidha, kwa mujibu wa Dk. Kimai, mbata husaidia pia kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kutokana na uthibitisho wa tafiti mbalimbali kuthibitisha kuwa ‘lauric acid’ hubadilishwa kuwa acid inayojulikana kama ‘monolaurin’. Aidha, nazi kavu husaidia pia kuzisisimua seli na shughuli za ubongo na kwa kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya akili (dementia) na upotezaji wa kumbukumbu (Alzheimer).
Akielezea kuhusu faida za mihogo mibichi, daktari mwingine alisema kuwa ina madini mengi pia yakiwamo ya calcium, phosphorus, chuma na potassium ambayo kwa pamoja husaidia ukuaji wa tishu za mwili wa binadamu.
“Kwa mfano, calcium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno kwa mwanadamu na hivyo mtu anayekula kwa wingi mihogo mibichi huimarisha meno yake na kuyafanya kuwa na nguvu,”alisema.
Katika mbata, baadhi ya virutubisho vingine vilivyomo ni Folates, Niacin, Pantothenic acid,
Pyridoxine, Riboflavin, Thiamin, Sodium na Copper
Updated at: 2024-05-25 10:35:28 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda midomo au sehemu nyeti. Yafuatayo ni mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu Ugonjwa wa Kaswende.
Updated at: 2024-05-25 10:35:29 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Kupooza ubongo kitaalamu ni Cerebral plasy (CP), ni hali ya kupooza ya moja kwa moja ya viungo vya mwili inayotokana na sehemu ya ubongo (seli) inayotawala viungo hivyo kufa katika kipindi cha mwanzo cha maisha (Utototni).
Mtindio wa Ubongo ni aina ya tatizo la mishipa ya fahamu inayoathiri misuli ya mwili inayotokana na selli za ubongo wa mtoto kufa au kutengenezeka vibaya katika kipindi cha mwisho wa ujauzito (3rd trimester), kipindi cha kuzaliwa au kipindi cha miaka miwili ya mwanzo wa mtoto.
Hii inatoka na sehemu ya ubongo kukosa oksijeni na virutubisho vya kutosha inayopelekea celli hizo kufa. Tunajua kuwa ubongo una kazi mbalimbali mfano kufikilia,kufanya maamuzi(decion making) pia inatawala sehemu mbalimbali ya viungo vya mwanadamu,mfano ubungo wa nyuma unahusika na kuona kama wakati mtoto akichelewa kulia cell za ubongo wa nyuma (occipital) zikafa mtoto huyu baadae atakuwa na matatizo ya kuona.
Vitu vingi vinaweza kusababisha ubongo kupooza, navyo ni katika kipindi cha ujauzito (mtoto akiwa tumboni), wakati wa kujifungua(80%) na kuugua mtoto kipindi cha mwanzo kabla ya miaka miwili.
Zaidi ya 67% ya watoto wote wenye tatizo la ubongo kupooza(CP) Tanzania inatokana na kuchelewa kulia baada ya kuzaliwa(birth asphyxia) ambayo inatokana na mama mjamzito kukaa na uchungu kwa muda mrefu(prolonged labour).
Ikifatiwa na manjano (severe neonatal jaundice) na degedege baada ya kuzaliwa inayopelekea celli za ubongo kufa.
Kabla ya miaka 2, mtoto akipata homa ya uti wa mgongo(meningitis) mtoto kuanguka(head trauma), malaria kali, matatizo haya yanaweza kuathiri seli za ubongo za mtoto ambazo haujakomaa.
Katika kipindi cha awali ujauzito(1st trimester) mama akipata mashambulizi ya magonjwa na kipindi cha miezi ya mwisho ya ujauzito (3rd trimester) shinikizo la damu kuwa juu (Pregnancy Induced Hypertension) na kifafa cha mimba/eclampsia kinaweza sababisha usafirishaji wa damu yenye oksijeni na virutubisho kupitia kondo la nyuma kushindikana vizuri hii inaweza pelekea baadhi ya cell kwenye mwili wa mtoto aliye tumboni kufa.
Kwa utafiti uliofanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mwaka 2013 kuhusiana na sababu za watoto waliopooza ubongo, inaonesha zaidi ya 80% ya watoto wenye tatizo hilo linatokana na matatizo katika kipindi cha kujifungua.
Madhala ya ubongo kupooza huwa yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwasababu inategemeana na sehemu ipi ya ubongo iliyoathiriwa zaidi.
Kupooza ubongo(CP) kunaleta matokeo mabaya ya moja kwa moja(permanent) katika mwili wa mtoto, Kila mfumo katika mwili wa mtoto unaweza athiriwa mfano mfumo wa chakula, wa hewa, mkojo,fahamu, na wa misuli ,athari zenyewe ni kupata degedege, Kifafa, mtoto kuwa na kichwa kikubwa(macrocephaly), mtoto kuwa na kichwa kidogo sana(microcephaly), tatizo la kusikia, kuona, kuongea,kumeza pia kushindwa kutembea na kupata choo ngumu (constipation) , Pia utahila (mental retardation).
Tatizo la ubongo kupooza hakuna matibabu yake, kinachotibiwa ni matokeo ya tatizo hili yanayosaidia kubolesha maisha yao na kuwa na hali ya kujitegemea.
Katika matibabu kuna aina mbili nayo ni medical (dawa) na mazoezi(therapy).
Dawa zinazotumika mfano phenobarbitone na Carbamazepine kwa degedege na kifafa na kukakamaa (contracture,spasticity) hupewa BOTOX inayosaidia kupunguza tatizo.
Kuna therapy mbalimbali kwa watoto wenye CP, nazo ni Physiotherapy, Occupational therapy, Speech therapy n.k.
Kwa tatizo la kutoweza kutembea, watoto hawa wanaweza pata faida katika kitengo cha mazoezi(physiotherapy) mzazi anaweza kufundishwa ili kumsaidia , misuli ya mwili kupata nguvu,hupunguza kukakamaa na pia inasaidia kupata ujuzi wa kutembea n.k. Pia kuna Occupational therapy inamsaidia mtoto apate uwezo wa kula mwenyewe na kukaa.Speech therapy/kuongea, watoto wengi wenye CP huwa na tatizo la kuongea hii inatikana na misuli inayosaidia katika kuongea kuathiriwa, kuna vifaa vinavyotumika kumsaidia mtoto mwenye tatizo hili ili aweze kuongea vizuri.
Sio watoto wote wenye kupooza ubongo wana utahila (mental retardation), 36% ya watoto wenye ubongo kupooza wana utahila(mental retardation). Mtoto anaweza kuwa na tatizo la viungo ila ana uwezo mkubwa wa kufikilia.
Jamii:Kwa utafiti uliofanyika katika hospitali ya Muhimbili, inaonesha zaidi ya asilimia 30 ya wazazi wanahusisha tatizo hili na mambo ya kishirikina(superstition) Wazazi wengi wenye watoto hawa wanafanya maamuzi ya kuwaficha watoto wao vyumbani kutokana na mtazamo wa jamii husika .
Familia:Pia imegundulika kuwa ndoa nyingi huvunjika mara baada ya kuzaliwa watoto wenye CP, kati ya wanawake 100 wenye watoto hawa waliohojiwa katika hospitali ya Muhimbili 16 wanaishi peke yao baada ya kupata watoto hao, wengi wao wanadai kuwa waume zao wanawalahumu kuwa wenyewe ndio chanzo cha hao watoto.
Pia wanawake wengi hupata changamoto katika malezi ya watoto hawa, wengi wao huwatekeleza katika vyumba inayopelekea kuharibika kisaikolojia.Hii inatokana na hali ya uchumi wa familia, mama na wanafamilia wote kuondoka nyumbani kwenda kufanya ujasiliamari ili kujikimu na maisha.
Familia :upendo unahitajika wa hali ya juu kwa watoto hawa, ili wasiharibike kisaikolojia. Kuna watoto wameweza kufanya vizuri katika masomo ambao wana tatizo hili, sio wote wanapata utahila, mtoto anaweza kushindwa kutembea lakini akawa na IQ kubwa, katika watoto waliokuwa wanahudhulia clinic ya watoto wa CP na kifafa Muhimbili, alikuwepo mmoja aliyekuwa anaongoza katika darasa analosoma na pia anamipango wa kusoma ili kuwasaidia watoto wenye tatizo hili, pia kuna madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu kwa watoto walioko marekani(Paediatric neurologist) ambao wana matatizo hayo.
Wazazi wasikate tama kwa watoto hawa kwa sababu kwa therapi mbalimbali watoto wanaweza rudi katika hali kama watoto wengine, pia wakiendelea kutumia dawa na kuhuzulia clinic kama watu wenye sukari na presha.
Uongozi: Kupitia vyombo vya Habari na vipeperushi , jamii ya Tanzania katika miji na vijiji, elimu itolewe kuhusiana na sababu ya tatizo ili kuweza ziepuka. Pia kuna vituo vichache sana vya mazoezi (physiotherapy na occupational therapy) wazazi wanapata changamoto nyingi, katika jiji la Dar, wengi wao huenda katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya mazoezi, kutokana na hali ya uchumi, nauli inakuwa changamoto wanaamua kuacha kuhudhulia kliniki.
Fursa ya kufungua vituo vya mazoezi(physiotherapy) na shule katika kila wilaya kwa sekta binafsi na serikali itasaidia watoto wenye CP. Pia shule za watoto wenye CP katika nchi ya Tanzania hazipo, kuna shule chache za watoto wenye utahila, watoto wenye CP sio wote wenye utahila.
Updated at: 2024-05-25 10:34:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Yafuatayo ni madhara ya shisha; 1.Kansa Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu. 2.Matatizo ya Moyo Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake. 3.Huharibu Fizi (periodontal disease) Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno. 4. Fangasi na Kifua kikuu (TB) Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria. 5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo) Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji. 6. “Nicotine Addiction” Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara. 7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana. Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume. 8.Kuchakaa kwa ngozi. Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia. 9.Asthma na Allergy Zingine Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma. 10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!