Updated at: 2024-05-25 10:22:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mapishi ni kitu ambacho kinaweza kuwa raha na pia kuwa na manufaa kwa afya yetu. Na leo, kama AckySHINE, ningependa kuzungumzia kuhusu mapishi ya viazi vitamu na jinsi yanavyokuwa vitamu na vyenye lishe. Viazi vitamu ni chakula chenye lishe kubwa na ladha tamu ambacho kinaweza kuboresha mlo wako na kukupa nguvu na virutubisho muhimu.
Hapa chini nimeorodhesha pointi 15 ambazo zinaonyesha umuhimu wa kula viazi vitamu:
Viazi vitamu ni chanzo kikubwa cha wanga ambacho kinaweza kukupa nishati ya kutosha kwa siku nzima. π₯
Pia, viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi ambazo zinaweza kuboresha umeng'enyaji wa chakula na kusaidia katika mmeng'enyo wa chakula. π
Viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini A ambayo inasaidia kuimarisha afya ya macho. π
Pia, viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo inasaidia kuimarisha kinga ya mwili. π
Kwa kuwa viazi vitamu ni chanzo cha wanga, yanaweza kuwa chaguo bora kwa watu wenye kisukari, kwani wanga wao hutolewa taratibu na kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. πͺπ½
Viazi vitamu ni chakula chenye kalori chache ambacho kinaweza kusaidia katika kupunguza uzito. Kwa mfano, unaweza kuandaa chips za viazi vitamu zilizopikwa kwa kutumia mafuta kidogo badala ya kuzipika kwa kuzama kwenye mafuta. π
Pia, viazi vitamu vina kiwango cha juu cha potasiamu ambayo inasaidia kudumisha afya ya moyo na shinikizo la damu. π
Kwa kuwa viazi vitamu vina nyuzinyuzi nyingi, yanaweza kusaidia katika kusawazisha viwango vya kolesterolini mwilini na kusaidia katika afya ya moyo. πΏ
Viazi vitamu ni chanzo kizuri cha madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa afya ya damu na inaweza kusaidia katika kuzuia upungufu wa damu. π
Akishine anashauri kutumia viazi vitamu katika mapishi mbalimbali kama vile maini ya viazi vitamu, supu ya viazi vitamu au hata keki ya viazi vitamu. Unaweza kuchanganya na viungo mbalimbali kwa ladha tofauti. π²
Viazi vitamu vinaweza kuwa chaguo bora kwa watoto, kwani ni chakula chenye ladha tamu ambacho kinaweza kuwafanya kuwa na hamu ya kula. Unaweza kuwafundisha watoto kula viazi vitamu kwa njia ya kuvutia kama kuandaa chips za viazi vitamu ambazo zimepikwa kwa njia ya afya. π
Pia, viazi vitamu ni chanzo kizuri cha asidi folic ambayo ni muhimu kwa afya ya wanawake wajawazito na inaweza kusaidia kuzuia kasoro za kuzaliwa kwa watoto. π€°π½
Viazi vitamu ni chakula chenye mchango mkubwa kwa afya ya utumbo, kwani nyuzinyuzi zake zinasaidia katika kuimarisha utendaji kazi wa utumbo na kuzuia matatizo kama vile kuvimbiwa. π½
Kwa kuwa viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini E, vinaweza kusaidia katika kudumisha afya ya ngozi na kusaidia katika kupunguza madhara ya kuzeeka. πΊ
Na mwisho kabisa, viazi vitamu vinaweza kuwa chaguo bora kwa watu wenye mlo wa mboga, kwani ni chakula chenye ladha nzuri na kinaweza kufanywa kuwa chakula kamili kwa kuongeza viungo mbalimbali kama vile mboga za majani, nyanya au hata kuku wa kukaanga. π₯
Kwa ufupi, viazi vitamu ni chakula chenye ladha tamu na muhimu kwa afya yetu. Kama AckySHINE, nakushauri kuwapa kipaumbele kwenye mlo wako na kujumuisha katika mapishi yako. Unaweza kujaribu mapishi mbalimbali na kubuni ladha tofauti kwa kutumia viazi vitamu. Je, unapenda viazi vitamu? Ni mapishi gani unayopenda kufanya na viazi vitamu? Napenda kusikia maoni yako! π½οΈπ
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ΒΎ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ΒΎ Kikombe
Vanila Β½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Jinsi ya kupika na kuandaa
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Β· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula Β· Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula Β· Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula Β· Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga ngano vikombc 3 Unga mbegu za mchicha kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Maziwa kikombe 1 Sukari kikombe 1 Blue band kikombe Β½ Mayai 10-12
Hatua
β’ Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike. β’ Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa. β’ Ongeza sukari na changanya. β’ Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike. β’ Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga. β’ Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo. β’ Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo. β’ Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:34:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Maziwa ya unga 2 vikombe
Sukari 3 vikombe
Maji 3 vikombe
Unga wa ngano Β½ kikombe
Mafuta Β½ kikombe
Iliki kiasi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2
Siagi - 4 Vijiko vya supu
Maziwa (condensed) 300Ml
Lozi zilizokatwakatwa - 1 kikombe
Zabibu kavu - 1 Kikombe
Arki (essence) - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Weka karai kwenye moto kiasi Tia siagi Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu. Weka lozi na zabibu huku unakoroga Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono. Tia arki Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze. Kipindue kwenye sahani utoe kileja. Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Jinsi ya kupika Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Viazi - 3
Nyama ya Kusaga - 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu - 1 Mug
(Frozen vegetable)
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 1
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 1 vijiti
Karafuu - 3 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Maji - 2 Β½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele. Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive. Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu. Tia mboga ya barafu (frozen vegetables) Tia maji, kidonge cha supu. Yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:35:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO
Unga wa mchele 500g
Samli 250g
Sukari 250g
Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai
Baking powder 1 kijiko cha chai
Mayai 4
Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA
1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo) Yai (egg 1) Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai) Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai) Maji kiasi Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari
Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo andaa kachumbali kwa kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.