Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI YA WALI
Mchele - 3 Magi
Mafuta - 1/4 kikombe
Karoti unakata refu refu - 3
Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa - 1 kikubwa
Pilipli manga - 1/2 kijicho chai
Hiliki - 1/2 kijiko chai
Karafuu ya unga - 1/4 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - 1/2 kijiko cha chai
Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji - 1 kijiko cha chai
Zabibu kavu (ukipenda) - 1/4 kikombe
Chumvi kiasi
KUPIKA WALI
Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo. Tia vitunguu kisha tia bizari zote. Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi Tia mchele upike uwive. Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda. Funika endelea kuupika hadi uwive.
MAHITAJI KWA NYAMA
Nyama - 2 Ratili (LB)
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 1/4 kikombe
Kitunguu (kata virefu virefu) - 1 Kikubwa
Pilipili mboga kubwa - 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.
Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.
KUPIKA NYAMA
Chemsha nyama hadi iwive Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu Kaanga kidogo tu kama dakika moja. Tayari kuliwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula · Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula · Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula · Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Wali
Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja
Vitunguu maji - 3
Karoti - 2
Siagi - 3 vijiko vya supu
Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando. Kwaruza karoti (grate) weka kando. Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu. Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu. Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo. Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.
Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
Kuku alokatwakatwa - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu
Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote. Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo. Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban. Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
• Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza. • Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.
• Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwakatika hali ya usafi.
• Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya nyongeza
• Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.
• Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa meno na madhara ya.
• Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mihogo kilo 1 Kidali cha kuku 1 kikubwa Nyanya 1 kubwa Kitunguu maji 1 cha wastani Swaum/tangawizi i kijiko cha chai Nazi kopo 1 curry powder 1 kijiko cha chai Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili 1 Chumvi kiasi
Matayarisho
Saga pamoja nyanya, kitunguu na swaum/ginger pamoja na vimaji kidogo. Kisha vitie kwenye sufuria isiyoshika chini na uvishemshe mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta na upike ktk moto mdogo mpaka viive.Baada ya hapo tia spice na uzipike kidogo kisha tia mihogo na kuku (kuku na mihogo vikatwe vipande vya wastani) vichanganye vizuri kisha tia nazi na vimaji kiasi,limao chumvi na pilipili na ufunike kisha punguza moto. Pika mpaka mihogo na kuku viive na ibaki rojo kidogo kisha ipua na mihogo yako itakuwa tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:34:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Muhogo - 3
Tui La Nazi - 2 vikombe
Chumvi - kiasi
Pilipili mbichi - 2
Mafuta - 1 kijiko moja
Kitunguu maji - 1 kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari. Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo. Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi. Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen veg)
Tuna (samaki/jodari) 2 kopo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 2
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 2 vijiti
Karafuu 6 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Viazi 3
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Jinsi ya kuandaa na kupika
Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20 Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu. Tia maji, yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo) Mchele (rice 1/2 kilo) Vitunguu (onion 2) Viazi (potato 2) Vitunguu swaum (garlic 3 cloves) Tangawizi (ginger) Nyanya ya kopo (tomato 1/2 ya tin) Curry powder (1/2 kijiko cha chai) Binzari nyembamba ya kusaga (cumin 1/2 kijiko cha chai) Binzari manjano (tarmaric 1/2 kijiko cha chai) Mafuta (vegetable oil) Chumvi (salt) Rangi ya chakula (food colour) Giligilani (fresh coriander) Maziwa ya mgando (yogurt kikombe 1 cha chai) Hiliki nzima (cardamon 3cloves) Karafuu (clove 3) Pilipili mtama nzima (black pepper 5) Amdalasini (cinamon stick 1)
Matayarisho
Katakata nyama kisha ioshe na uiweke kwenye sufuria kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, nyanya, curry powder, binzari zote, chumvi na maziwa ya mgando kisha bandika jikoni ichemke mpaka nyama iive na mchuzi ubakie kidogo.Baada ya hapo kaanga viazi na uweke pembeni, kisha kaanga vitunguu na mafuta mpaka viwe ya brown na kisha uvitie viazi vitunguu, na mafuta yake katika nyama. Koroga na uache uchemke kidogo kisha ipua na utie fresh coriander iliyokatwa na hapo mchuzi wako utakuwa tayari. Baada ya hapo loweka mchele wako kwa muda wa dakika 10, kisha chemsha maji yatie chumvi, hiliki, karafuu, pilipili mtama na abdalasin na mafuta. Yakisha chemka tia mchele na uache uchemke mpaka ukauke maji yakisha kauka tia rangi ya chakula na uanze kugeuza ili ichanganyike na wali wote. Baada ya hapo ufunike na uache mpaka uive. Na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.