Sheria kuhusu utoaji mimba

Sheria kuhusu utoaji
mimba zinatofautiana
kati ya nchi na nchi. Hapa
Tanzania utoaji mimba
ni kosa la jinai.5 Kosa la
jinai linamchukulia mtu
hatua aliyetoa mimba na
yule aliyemtoa au
kumsaidia kutoa mimba.
Hata hivyo hapa Tanzania
unaruhusiwa kutoa mimba
pale tu inapokwepo sababu
za kuokoa maisha ya mama
mjamzito kama kuna
matatizo ya kiafya au
pale mimba inatokana na
kubakwa.6 Utoaji mimba hufanyika kwa siri.
Ni hatari iwapo utoaji mimba utafanyika bila ya utaalamu. Yule
anayesaidia kutoa mimba anawajibishwa kisheria. Iwapo utoaji
mimba umefanywa na mtu asiye na ujuzi, kwa mama mwenyewe,
au kifaa kilichotumika ni kichafu, au majani au dawa zimewekwa
ukeni, zinaweza kuhatarisha maisha ya mama.
Ni muhimu hata hivyo kujua kuwa wahudumu wengine hutoa
huduma baada ya mimba kuharibika kwa wale wanaohitaji
msichana au mama, kutokana na matatizo ya utoaji mimba au
kuharibika kwa mimba

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Siyo haki kwa mtoa huduma wa afya kukataa kumtibu.
Kama kijana, una haki sawa ya kutibiwa kama vile mtu yoyote.
Iwapo mtoa huduma anakataa kukutibu wewe, jaribu kuzungumza
naye kuhusu jambo hilo na umuulize sababu za kukataa kukutibu.
Iwapo yeye anashikilia uamuzi wa kutokutibu basi amua ama
unatafuta mhudumu mwingine au zungumza na mkubwa wake
kuhusu tatizo lako. Ni jambo la maana kuzungumza na rafiki
yako au mwone mtu unayemwamini akusaidie kutatua tatizo
lako.

Vituo vingi vya Umma na vya binafsi vya huduma za afya
vinajitahidi kutoa huduma rafiki kwa vijana. Tafuta kituo cha
karibu au shirika linalotoa huduma za afya ya uzazi. Kumbuka,
haki ya afya ambayo pia inabeba haki ya huduma ya afya ya
uzazi, Kimataifa inatambuliwa kupitia ICESCR4 na pia imetiwa
saini na kuridhiwa hapa Tanzania. Hivyo usisite kuulizia huduma
kama hii.

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?

Kujamiiana ni uamuzi wa mtu binafsi. Ni uamuzi wako na hakuna
mtu yeyote mwenye haki ya kukuamulia. Lakini unapoamua
kujamiiana hakikisha kwamba ni maamuzi uliojulishwa na kwamba
unaelewa matokeo ya kujamiiana. Usisahau kuchukua hadhari
muhimu. kumbuka kutumia kondomu kujikinga wewe na mwenzi
wako kutokana na mimba usizotarajia na magonjwa kama vile
Virusi vya UKIMWI. Madhari mwili wako unaendelea kukua,
kujamiiana bila ya kondomu ni hatari zaidi kuliko mtu mzima,
kwa sababu maambukizo mengine haswa kwa vijana yanaweza
kukuletea matatizo kama vile ugumba baadaye katika maisha.
Pia jiulize mwenyewe kwa uangalifu kama kweli unataka
kujamiiana. Ni muhimu pia kujadiliana na mwenzi wako na kuwa
na hakika kama wote wawili mnataka kujamiiana. Usijamiiane
kwa sababu tu unafikiria kwamba watu wengine wanajamiiana
au unajitosa kwa kuwa unashawishiwa na marafiki au watu
wazima.

Ni umri gani ambapo vijana wanapaswa kuelezwa juu ya afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Vijana balehe wote wana haki ya kupata habari juu ya mambo yote
wanayoyapenda. Watoto wanavyokuwa, wanapitia mabadiliko ya
kimwili, hisia na ya kisaikolojia katika maisha yao. Watu wazima,
hasa wale wanaowasimamia watoto wanapaswa kuwapa habari
juu ya mabadiliko na jinsi yanavyoshawishi ukuaji wa kimwili na
hisia. Hii ni muhimu ifanyike muda wote na katika kila rika.
Vijana wana mahitaji mbalimbali kutegemea umri wao, katika
hatua ya ukuaji na mazingira, mvulana wa umri wa miaka 11 au
kijana wa miaka 18 watakuwa na shauku tofauti. Pi wavulana au
wasichana wana haja tofauti na hata vijana wawili wenye umri
na jinsia moja wanaweza kukua kwa kasi na njia tofauti.
Tofauti hizi zinahitaji
kutambuliwa na kushughulikiwa.
Ni muhimu
pia kutambua
kwamba mahitaji
haya yatabadilika
kadiri ya muda unavyoenda
na pia kuweza
kubadilika kwa
haraka sana. Kwa
mfano mtu anapokuwa
na mhemuko wa
kujisikia kujamiiana.
Kwa njia yoyote, watoto
wana haja ya
kupata habari juu ya
uzazi kabla au mara
tu wapaoingia katika
ujana. Pia mada juu ya wajibu wa wavulana na wasichana katika
jamii, uhusiano na marafiki, na wazazi, uhusiano wa kijinsia na
matatizo yanayotokana na unyanyasaji wa kijinsia / ujinsia ni
muhimu yajadiliwe.
Iwapo vijana hawapati habari za kutosha juu ya mabadiliko ya
miili yao wanaweza kuingizwa katika matatizo ya kimaisha, ya
kijinsia na mimba yasiyotarajiwa au magonjwa yatokanayo na
kujamiiana pamoja na Virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo wasichana
na wavulana wanahitaji kupata elimu ya ujinsia wanapokuwa vijana
wadogo. Hii ni pamoja na habari ya jinsi ya kujilinda wenyewe.
Siyo kweli kwamba elimu ya ujinsia inahimiza vijana wajamiiane.
Kinyume chake, wale vijana waliopata habari sahihi wanakuwa
na mwelekeo mzuri na wana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi
. kama vile kuamua kuahirisha kujamiiana mpaka baadaye na
pia wanajilinda mara wanapoanza kujamiiana. Elimu ya Afya ya
Uzazi na Ujinsia ina habari juu ya uzuiaji wa mimba na kondomu.
Kabla ya kuanza kujamiiana inatakiwa vijana waelezwe kuhusu
njia za uzazi wa mpango na hasa jinsi ya kutumia kondomu kwa
sababu kondomu huzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI
na magonjwa yatokanayo na kujamiiana. Jambo la busara ni
kwenda kliniki kwa ushauri katika suala zima la njia za uzazi wa
mpango mara tu ukiamua kuanza kujamiiana.

Haki za uzazi ni zipi?

Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na
asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa
haki ya kupata heshima kama
binadamu. Mara mtu azaliwapo
mume au mke hupata
haki hizi. Haki hizi
zinatambuliwa kimataifa
na zina usawa kwa watu
wote. Nchi mbalimbali
zimetia saini na kuidhinisha
haki hizi za kimataifa
na kufanya ni sehemu
ya sheria zao
pamoja na kuweka sera
zinazolinda haki hizi.

Haki za uzazi zina misingi yake katika haki za binadamu na pia
zinahusiana na haki za mtu mmojammoja.

Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya
ya uzazi.

Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na
kuwajibika, kama unataka kujamiaana lini na nani.
Uhuru wa maamuzi.

Kuamua kwa hiari na kuwajibika juu ya idadi na muda wa
kupishana katika kupata watoto.

Kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi.

Haki za kufanya maamuzi kuhusu afya ya uzazi, kwa
uhuru, bila kunyanyaswa, kulazimishwa, bila kutumia
nguvu pamoja na maamuzi nani wa kufunga naye ndoa.

Kujilinda kutokana na mila zenye madhara kama vile
ukeketaji wa wanawake.

Haki hizi zimerekebishwa tangu mkutano uliofanyika Cairo mwaka
19941.

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via
vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi inahusiana na mambo
yote yanayojumuisha uzazi na ujinsia. Ina maana kuwa watu
wana uwezo wa kukidhi mapenzi na usalama katika maisha
yao, kwamba watu wana uwezo wa kuwa na watoto na pia wana
uhuru wa kuamua, kama lini na kwa muda gani wapate watoto.
Yaliyomo humu yanampa haki mwanamume na mwanamke kupewa
habari au kuelekezwa na kufikiwa na njia za uzazi wa mpango
ambazo ni salama, zinazofanya kazi, anazomudu kulipia na njia
zinazokubalika za uzazi wa mpango alizochagua na haki ya kuwa
na huduma za afya zinazofaa ambazo zitawawezesha wanawake
kuwa salama wakati wa ujazito na kujifungua.

Ukweli kuhusu albino

  1. Je, ualbino unaambukiza? ……….. Hapana
  2. Ualbino ni ugonjwa? ………..Hapana
  3. Ualbino ni laana? ………..Hapana
  4. Ualbino ni kitu cha kawaida? ………..Hapana
  5. Ualbino unawapata tu watu weusi?……….. Hapana
  6. Watu wanaoishi na ualbino wana macho mekundu?……….. Hapana
  7. Albino ni watu wenye imani za ushirikina? ………..Hapana
  8. Albino wana nguvu za giza? ………..Hapana
  9. Je, Albino hawana akili? ………..Hapana
  10. Je, ni kosa la mwanamke anayezaa mtoto Albino? ………..Hapana
  11. Je, jamii ibadili mtazamo hasi iliyo nao kuhusu Albino?……….. NDIYO

Je, kuna madhara gani yatokanayo na uvutaji sigara kwa vijana hasa kijana Albino?

Kuna madhara mengi ambayo hutokana na uvutaji sigara.
Madhara mengi yanampata mvutaji kwani moshi unaingia
kwenye mapafu na kuendelea kuleta madhara mengine sehemu
nyingine za mwili.

Unaweza pia kupata madhara kwa kukaa karibu na mtu
anayevuta (hii inaitwa mvutaji baki). Uvutaji unafanya mwili
wako kunyonya sumu ijulikanayo kama nikotini. Nikotini ndio
chanzo kikubwa cha matatizo yatokanayo na uvutaji.
Uvutaji sigara unahusishwa na magonjwa mengi. Kiungo cha
mwili kinachoathirika kwanza ni mapafu. Uvutaji husababisha
kukohoakohoa, vichomi na kulipuka kwa kifua kikuu (TB) na
hatimaye saratani ya mapafu. Uvutaji pia unaathiri ngozi.
Ngozi ya mvutaji inakuwa nyepesi kwani inaathiri mishipa ya
damu iliyopo karibu chini ya ngozi. Hali hii inaifanya ngozi
kushindwa kujitengeneza upya (regenerate). Kwa vile Albino
tayari wana matatizo ya ngozi ni vizuri kama hawatavuta na
kwa wale wanaovuta basi waache kuvuta.

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Athari za pombe kwa mtu anayeishi na ualbino ni sawa na zile
zinazowapata watu wengine.
Mtu akiwa katika hali ya ulevi anaweza kuzembea katika
kufanya uamuzi sahihi kwa mfano kuhatarisha maisha yake
kwa kuendesha baiskeli yake kimchoromchoro, kujamiiana
bila kuvaa kondomu na kadhalika. Mbali na hayo, watu wenye
matatizo ya kunywa pombe husahau kujiweka katika hali nzuri
kwa maana hawajali kula chakula. Tabia hii inamuweka katika
hatari ya kuandamwa na maradhi.
Pombe zinaweza pia kuingiliana na maisha/uhusiano wa kimwili.
Mwanzo kabisa pombe inaweza kukusisimua na kukufanya
mchangamfu (kutoona aibu), lakini kadiri unavyoendelea
kunywa unaanza kusinzia na kwa upande wa wanaume wengine,
uume kukosa nguvu. Unaweza kushawishika kutoa aibu uliyo
nayo kwa kunywa pombe lakini mara nyingi hii haileti mvuto
kutoka kwa wenzi wako.

Kunywa pombe pia kunaleta uharibifu wa kudumu kwenye ubongo
ambao unamfanya mtu kupata matatizo ya kumbukumbu.
Pombe imewekwa kwenye kundi la vilevi tegemezi. Mwili
ukishazoea pombe, ni rahisi sana watu kutumia pesa zote
kwa ajili ya pombe na kusahau kufanya mambo mengine
yatakayomletea maendeleo katika maisha yake.

Watu wanaoishi na ulemavu wanapewa huduma za upasuaji hasa wakati wa kujifungua?

Upasuaji unafanyika kwa wanawake wote ambao wamegundulika
kuwa na tatizo la kujifungua kwa njia ya kawaida. Hii inafanyika
bila kujali hali yao kwa maana kwa watu wenye ulemavu na
wasio na ulemavu. Kila mwanamke atapata huduma hiyo kama
itakuwepo sehemu anapoishi.
Tatizo lililopo hapa Tanzania kwa sasa hivi hasa sehemu
zilizojitenga ni umbali wa kufikia huduma hii. Umbali huu
unamfanya mama aliyeanza uchungu wa kujifungua kushindwa
kuweza kufika kwa muda unaotakiwa.

Haki za ujinsia na afya ya uzazi zinamhusu pia mtu anayeishi na ualbino?

Haki za msingi; hasa zile zinazohusiana na kuthaminiwa na
kuheshimiwa kama binadamu zinawahusu binadamu wote
kuanzia siku unayozaliwa. Mataifa yote Ulimwenguni yameridhia
mikataba ya Kimataifa inayokubaliana na matamko haya ya
haki. Haki hizi ziko dhahiri katika sheria za nchi husika. Haki
muhimu za ujinsia na afya ya uzazi ni hizi:
β€’ Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya ya
uzazi.
β€’ Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na kuwajibika,
kama anataka kujamiiana lini na mtu gani.

β€’ Kuamua idadi ya watoto anaotaka kuzaa na hao watoto
wapishane miaka mingapi.
β€’ Kupata huduma za afya ya uzazi.
β€’ Kuamua bila kulazimishwa nani wa kufunga naye ndoa.
β€’ Kulindwa dhidi ya mila zenye madhara kama vile ukeketaji
wa wanawake.
Watu wote wakiwemo wale wanaoishi na ualbino au ulemavu
wa aina yoyote wanalindwa na haki za binadamu. Changamoto
iliyopo ni kwa wale watu wanaoishi na ualbino kutoa sauti katika
kutetea na kuhamasisha jamii juu ya haki zao.

Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?

Ndiyo msichana anaweza kupata mimba kwa kujamiiana mara
moja tu bila kujali ana rangi gani ya ngozi. Wasichana weupe,
weusi na wanaoishi na ualbino au wasio na ulemavu wa ngozi
wanafanana wote inapokuja kwenye suala la uwezekano wa
kupata mimba. Kinachobainisha/ kinachosababisha upatikanaji
wa mimba ni wakati tendo la kujamiiana linapofanywa na hatua
ya mzunguko wa hedhi. Kama yai lililopevuka kwa ajili ya
kurutubishwa litakuwa tayari basi ujauzito utatokea mara tu
baada ya mbegu ya mwanaume kuingia, (wakati wa kujamiiana).
Ujauzito unaweza kutokea hata kama msichana alikuwa bado
bikira na ni mara yake ya kwanza kujamiiana.

Je, wazazi ambao wote ni Albino wanaweza kupata mtoto ambaye siyo Albino?

Kwa kawaida, wazazi wote wakiwa Albino watazaa mtoto
Albino. Kwa maana hiyo basi, iwapo watu wawili wanaoishi na
ualbino wataamua kuunda familia itakuwa vizuri wafikirie kwa
makini kama wangependa kuzaa pamoja wakizingatia matatizo
ambayo wamewahi kupitia wao wenyewe kama Albino ndani ya
jamii. Ualbino ni hali ya kurithi na inabidi mtoto Albino abebe
vinasaba kutoka kwa wazazi pande zote ili aweze kuonyesha
ualbino. Hata hivyo, kuna aina zaidi ya moja ya ualbino na
pia aina tofauti za vinasaba, kama wazazi watakuwa na aina
tofauti ya ualbino na aina tofauti katika vinasaba, uwezekano
wa kupata mtoto asiyekuwa na ulemavu wa ngozi unakuwepo.
Lakini matukio kama haya yamejitokeza mara chache sana
ulimwenguni.

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Ni kweli kuwa daktari anaweza kufanya vipimo vya kugundua
kama mtoto aliye tumboni ni mwenye ulemavu au la. Baadhi ya
vipimo hivi ni β€œultra sound” ambacho kinawezesha kuona picha ya
umbo la mtoto akiwa bado tumboni. Vipimo vingine vinaangalia
damu. Lakini ualbino hauwezi kugundulika kwa vipimo hivi.
Pia baada ya kuzaliwa daktari ana uwezo wa kutambua kama
mtoto ana ulemavu / hitilafu kama vile moyo, kwenye damu
kama vile β€œsickle cell”. Ualbino unaweza kugundulika mara tu
mtoto anapozaliwa au baada ya wiki chache.

Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa?

Kama umebakwa au kulazimishwa kujamiiana unaweza kupata
huduma katika hospitali, kituo cha afya , zahanati au kutoka
kwa mhudumu wa afya ambaye atakupatia vidonge vya dharura
vya kuzuia mimba. Hivi ni vidonge ambavyo vinatumika ili
kupunguza uwezekano wa kupata mimba kama ulijamiiana bila
kinga, au umesahau kutumia njia yako ya uzazi wa mpango au
ulilazimishwa kujamiiana.

Ili ufanye kazi, njia hii ya dharura ya kuzuia mimba inatakiwa
itumiwe ndani ya saa 120 (ndani ya siku tano) baada ya tukio.
Inakuwa vizuri zaidi kama njia hii ya dharura itatumika punde
bila kusubiri kwani kwa kufanya hivyo, ufanisi wake unakuwa
wa kuaminika zaidi.

Hii njia ya dharura inazuia tu mimba kutungwa, haiwezi kusababisha
kutoka kwa mimba pindi mimba ikishatunga. Utakapotafuta
msaada wa kupata huduma ya vidonge vya dharura
vya kuzuia mimba hasa kwa wale waliobakwa au kulazimishwa ,
mwombe mhudumu akusaidie kupata huduma ya kuzuia maambukizo
ya UKIMWI. (Post exposure prophylasis). Unaweza
kupata taarifa zaidi kwa mtoa huduma wa uzazi wa mpango
kwenye kliniki za serikali, kliniki za UMATI, kliniki za Marie
Stopes au sehemu yoyote wanapotoa njia za kisasa za uzazi
wa mpango.

Kuna athari gani za mimba za utotoni hasa kwa kijana Albino?

Katika masuala ya athari za mimba katika umri mdogo ni
kwamba vijana Albino hawana tofauti na vijana wengine . Bado
inashauriwa na kutiliwa mkazo umuhimu wa msichana kutopata
mimba akiwa na umri chini ya miaka 18.

Sababu kubwa ikiwa ni
kuwa mwili wa msichana
ambaye umri wake ni chini
ya miaka 18 haujakomaa
vya kutosha kuweza
kuhimili ujauzito bila
matatizo. Katika umri huu
mdogo, uwezekano mkubwa
wa kupata matatizo
yanayotokana na ujauzito,
hasa wakati wa kujifungua.
Uzoefu umeonyesha
kuwa mara nyingi wakati
wa kujifungua mtoto
anashindwa kutoka na
inabidi mama afanyiwe
upasuaji. Pia katika
umri huu uwezekano ni
mkubwa mtoto kuzaliwa
njiti (hajafikia muda wa
kuzaliwa).
Tatizo jingine linaweza kutokea pale ambapo kichwa cha mtoto
ni kikubwa au mama anakuwa na uchungu wa muda mrefu na
kusababishwa kuchanika kwenye mfumo wa uzazi kwenye njia
ya haja ndogo au hata na njia ya haja kubwa na mama kupata
fistula. Hali hii ikitokea itamfanya mama hatimaye awe anavuja
ama haja ndogo au haja kubwa au vyote viwili kupitia njia ya
ukeni.

Mbali na madhara haya ya kiafya, msichana anaweza kupata
matatizo mengine ya kijamii kama vile kufukuzwa shule,
kusababisha ugomvi ndani ya familia na jamii. Kwa mantiki hii,
ni muhimu kwa vijana kusubiri hadi kufikia miaka 18 wakiwa
tayari kuchukua / kubeba majukumu kama wazazi.

Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Hakuna kipimo rahisi cha kuwezesha kuonyesha kama mama
mjamzito amebeba kinasaba cha ualbino. Lakini uwezekano upo,
kama wazazi watakuwa wamepata mtoto Albino. Uwezekano wa
kujua kama mimba inayofuatia kichanga kitakuwa na ualbino kwa
kutumia kipimo maalamu kinachovuta maji yaliyo kwenye mji wa
mimba na kupima hayo majimaji kuona kama kuna kinasaba cha
Albino. Hata hivyo, vipimo hivi ni vya gharama kubwa na kwa
kiasi kikubwa kwa sasa vinapatikana, katika hospitali kubwa
maalumu za nchi zilizoendelea (Ulaya, Marekani na kadhalika).

Shopping Cart
17
    17
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About