Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kulevya hurahisisha kupata na kuenea kwa magonjwa haya. Dawa hizi hudhoofisha mwili na kinga ya mwili. Hivyo basi hurahisisha virusi vya magonjwa kuingia mwilini mwa mtumiaji kiurahisi.

Matumizi ya dawa za kulevya huwafanya watumiaji kusahau hatari za kuwa na wapenzi wengi pamoja na kufanya ngono na watu usiofahamu hali za afya zao. Hujisahau kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu. Vilevile husahau majukumu yao kama vile mke, watoto na familia nzima kwa ujumla.
Dawa za kulevya zinazoingia mwilini kwa njia ya sindano husababisha uwezekano mkubwa wa kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU) kwa watumiaji pindi wanapochangia sindano kujidungia dawa hizo mwilini. Pia dawa za kulevya huchangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa kuwa watumiaji hujii ngiza katika biashara ya ngono i ili kuweza kujipatia fedha za kununulia dawa hizo.

Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?

Kitu muhimu ni kwamba, kweli uwe umedhamiria kuacha. Hatua ya kwanza ni kujiuliza kwa nini unatumia dawa za kulevya. Pale utakapojua ni nini ulikuwa unahitaji katika dawa za kulevya ni rahisi kutimiza malengo hayo kwa njia za kiafya zaidi. Jaribu kupunguza taratibu kiasi na muda wa kutumia dawa za kulevya. Pia tumia vitamini na madini kuimarisha afya yako. Jitenge na watumiaji wengine wa dawa za kulevya na sehemu ulizokuwa ukienda kupata dawa za kulevya. Kama hutofanikiwa katika hatua ya kwanza usikate tamaa! Watu hushindwa kuacha katika jaribio la kwanza! Jaribu tena!

Kuacha dawa za kulevya ni sawasawa na kupata nafuu ya ugonjwa, ni rahisi zaidi kufanikiwa kama utapata ushirikiano zaidi kutoka kwa marafiki au wanafamilia. Unaweza vilevile kuomba ushauri kutoka kwa watoa nasaha au madaktari. Msaada wa kitabibu ni muhimu kwa wale waliozoea kutumia hiroini na pombe, kwani mara nyingi hupata madhara yatishiayo maisha pale wanapojaribu kuacha dawa za kulevya.
Ni vigumu kusema utachukua muda gani kuacha kutumia dawa za kulevya, kwa sababu i natofautiana kati ya mtu na mtu.

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Hii ndio hasa sababu kwa nini dawa za kulevya ni hatari! Mara unapozizoea unakuwa na ugumu wa kuendesha maisha yako bila dawa za kulevya. Kwa dawa nyingi za kulevya ubongo huzoea kuwepo kwake kwenye damu na dawa zaidi na zaidi huhitajika i ili kuendeleza hali hiyo. Hii i ii ina maana kadri muda unavyoenda ndivyo unavyoongeza kiasi cha dawa za kulevya unachokihitaji.
Pale utakapojaribu kupunguza kiasi cha matumizi ya dawa za kulevya au kuacha kabisa unaweza kupata hali ya kimaumbile au kiakili i i itokeayo kutokana na kuacha kitu ulichozoea. Hali hii inaweza i isiwe ya kufurahisha, yenye kuumiza na pengine hatari kwa maisha yako. Mara mtu anapozizoea dawa za kulevya haiwi tu tabia bali ugonjwa. Watu wengi wanaotegemea dawa za kulevya hawazitumii kwa kujifurahisha bali kuzuia maumivu yasababishwayo na kuacha kitu ulichozoea. Njia nzuri ya kuzuia hali hii ni rahisi: kuwa jasiri na sema HAPANA. Usijaribu dawa za kulevya.

Je, ni kweli kwamba kuvuta bangi kunaongeza akili na uwezo wa kufikiri?

Hapana, hii si kweli! Vijana wanaoamini kwamba wana uwezo wa kufikiri baada ya kuvuta bangi kwa sababu inawapa hisia ya kuzoea mihemko ya kusikia vizuri au kufahamu kwa haraka. Lakini ni kawaida kwamba uvutaji wa bangi unaathiri shule, kazi na shughuli nyingine kinyume na matarajio ya mafanikio. Siku zote vijana wavutaji bangi wanapoteza ari shuleni au mafunzoni. Wanashindwa kuweka malengo ya maisha yao ya baadaye.

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Bangi hupunguza mawazo kwa muda mfupi kwani huleta hisia za furaha na utulivu. Lakini hata hivyo matatizo hubakia palepale na mara nyingi huongezeka hapo baadaye. Watu wanaovuta bangi huikimbia dunia halisi na huingia dunia ya ndoto kwa muda mfupi. Mara hisia zilizoletwa na bangi zinapoondoka, aghalabu matatizo huwa mabaya zaidi kuliko mwanzo. Matumizi ya bangi huahirisha na kuchelewesha tu utatuzi wa matatizo.

Nini matokeo ya unusaji/uvutaji wa petroli kwa vijana?

Kama kijana akinusa au kuvuta petroli kupitia puani au mdomoni, petroli hiyo huingia kwenye mapafu na sehemu zote mwilini.
Madhara ya unusaji au uvutaji petroli ni sawa kabisa na pombe. Baada ya kunusa/kuvuta petroli mtuamiaji hujisikia kizunguzungu na kulewa. Wengine huhisi kama kwamba wanaota na kujisikia furaha. Lakini wengine hujisikia kuumwa na kusinzia.
Unusaji/uvutaji wa petroli ni hatari sana na hata huweza kusababisha vifo kwani petroli humfanya mtu apoteze fahamu, huharibu mapafu na wengine hufa kwenye ajali. Hii hutokana na kushindwa kutoa uamuzi ufaao wanapokabiliwa na hali zinazoweza kusababisha ajali, hasa barabarani.
Matumizi ya muda mrefu ya petroli huweza kumsababishia madhara mtumiaji kama kutokwa na damu puani, kupoteza hamu ya kula, kuwa dhaifu, kupata matatizo ya mtindio wa ubongo, kupatwa na magonjwa ya figo, moyo, mapafu na kuharibika maini.

Je, inawezekana kuwa ni hatari kutumia Valium au Klorokwini au dawa nyingine ambazo zinapatikana katika maduka ya dawa?

Ndiyo! Dawa yoyote i itakayotumiwa pasipo mahitaji sahihi au kwa kipimo zaidi ya kinachopendekezwa i inaweza kuwa hatari na pengine husababisa kifo. Mara zote sikiliza kwa makini maelekezo yatolewayo na madaktari au wauzaji wa dawa. Usichanganye dawa na pombe au dawa nyingine kwani kwa hakika kufanya hivyo ni hatari.

Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Ni vigumu sana kujibu swali hili kwa sababu muda wa madhara hutegemea sababu mbalimbali kama vile aina za dawa za kulevya, njia za utumiaji, hali ya mtu na mazingira anapozitumia dawa hizo za kulevya. Mtu anaweza kuanza kutumia dawa za kulevya mara kwa mara i ili kukidhi kile anachokihitaji. Kwa baadhi ya dawa za kulevya, na baadhi ya watu, matumizi ya mara kwa mara kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili ni kipimo tosha cha kumfanya aishi kwa kutegemea dawa za kulevya.

Dawa gani za kulevya ni hatari zaidi?

Kwa ujumla dawa zote za kulevya zinaweza kuwa ni za hatari. Kati ya dawa zilizohalalishwa kisheria nikotini, ambayo i ipo kwenye sigara, ndiyo hasa ya hatari. Inawezekana kuwa umeshakuwa tegemezi kwa sigara. Hii i ii ina maana ubongo wako utaizoea nikotini na utahitaji nikotini zaidi na zaidi i i ili kuendelea kuwa na hali nzuri. Nikotini pia ni hatari zaidi kwa sababu vijana mara nyingi huanza kutumia sigara kabla ya kuanza kutumia dawa kali zaidi.

Miongoni mwa dawa zisizoruhusiwa kisheria nchini Tanzania, heroini ndiyo labda yenye kusababisha utegemezi. Vilevile inahusishwa na makosa mengi ya jinai. Utumiaji wa heroini ni hatari hasa katika maambukizi ya UKIMWI. Watu wanaposhirikiana katika kutumia sindano za kujidungia heroini wanajiweka katika hatari na uwezekano mkubwa sana wa kuambukizana virusi vya UKIMWI. Hili hutokea pia pale watumiaji wa heroini wanapojiuza mii li yao katika ngono i ili wapate dawa za kulevya au fedha za kununulia dawa hizo.
Uvutaji bangi husaidia kuondoa aibu na vizuizi. Hii i ii inamaanisha kuwa wavuta bangi wanaweza wakasahau kufanya ngono salama na hivyo kuwa katika hatari zaidi ya kupata au kueneza UKIMWI. Matumizi mabaya ya dawa huweza kuwa hatari sana na pengine kusababisha kifo pale zitakapotumiwa kupita kipimo ama zitakapochanganywa na dawa nyngine au pombe.

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Sababu mojawapo ni kuwa bangi hulimwa hapa nchini na
hivyo hupatikana kwa urahisi. Bangi huuzwa kwa bei
nafuu kuliko dawa nyingine za kulevya. Vilevile, vijana
wengi huwaona wakubwa wao wakitumia na hii huwafanya waone kuvuta bangi ni kitu halali.

Sababu nyingine ni i i imani potofu kwamba ukivuta bangi unaweza kuwa jasiri wa kufanya kazi na kusoma sana. Lakini yote haya ni uzushi na si kweli kwani watu husahau madhara ya muda mrefu yasababishwayo na uvutaji bangi.
Sababu nyingine i inayowafanya Watanzania watumie bangi ni utegemezi wa kisaikolojia, kwani baada ya kuvuta bangi kwa muda, mtu huanza kujisikia hawezi i kuhimili msukumo wa kawaida wa maisha na kuishi bila bangi. Kwa maana hiyo muathirika huendelea na uvutaji bangi.

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika viungo vya
ndani ya mwili kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Watu wengi hufa katika ajali pale wanapokuwa wana kiasi kikubwa cha kilevi katika damu, kwani wanashindwa kutambua mazingira ya hatari.
Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza akafa ghafla kwa kile kinachoitwa kuzidisha dawa, pale mtu atakapotumia dawa za kulevya zaidi ya uwezo wa mwili. Kifo cha ghafla kinaweza kutokea au kutokana na matumizi ya kokaini na vifukishi kama petroli bila hata ya kuzidisha kiwango. Watumiaji wa vifukishi kama petroli mara nyingi hutumia mifuko ya plastiki i i ili kuongeza kiwango cha mvuke wanaovuta. Katika mazingira haya ni rahisi kupoteza fahamu kutokana na kukoseshwa hewa na mifuko hiyo. Kuchanganya baadhi ya dawa za kulevya kama vile heroini na dawa zingine hasa dawa za kutuliza maumivu (mfano valium) au pombe pia huweza kusababisha kifo.

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kidogo kunaweza kusilete madhara i ila mpaka tu pale utakapoyazoea. Mara nyingi watu huanza kuhitaji dawa zaidi pale wanapozizoea na kupata madhara. Hii i ii inaweza kusababishia mtu kutawaliwa na dawa za kulevya. Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza kuwa mtegemezi wa dawa hizo bila ya kujijua. Kujaribu dawa za kulevya kunaweza kukawa na madhara kama “utaishia pabaya”. “Kuishia pabaya” ni jambo la kutisha na si la kufurahisha hata kidogo! Hali hiyo inaweza kutokea mara ya kwanza unapoanza kutumia bangi.

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali na huwezi ukasema kwa uhakika jinsi zitakavyokuathiri. Madhara ya dawa za kulevya yanategemea aina, kiwango na jinsi zitakavyotumika. Vilevile inategemea na umri, afya ya mwili na ukomavu wa akili, na pia mazoea ya matumizi ya dawa hizo.
Madhara ya muda hutokea mara tu baada ya dawa za kulevya kutumika, wakati madhara ya muda mrefu huonekana baada ya muda kupita, na mara nyingi husababisha uharibifu wa kudumu kwenye mapafu na ubongo.

Kwa mfano, bangi, husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, matatizo ya kumbukumbu ya muda mfupi, pamoja na umakini, kujifunza, kufikiri na kutatua matatizo. Pia inaweza ikasababisha kasoro kwenye utaratibu wa viungo vya mwili. Mara kwa mara wavuta bangi huwa na macho mekundu. Na vijana wengine hupata mihemuko mbalimbali kama uoga na hofu baada ya matumizi ya bangi.
Dawa za kulevya za vichangamsho, kama mirungi na kokaini, inasemekana kuwa huwafanya watumiaji kuwa macho, kujiona wana nguvu na kujiamini. Vichangamsho vikitumika kwa wingi, humfanya mtumaji kujihisi kuwa na wasiwasi au hofu. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya akili au hata kifo i iwapo yatatumika kwa kiwango cha juu.
Dawa za kulevya zinazokufanya upooze kama heroini au dawa nyingine zinazoagizwa na daktari, husababisha kujisikia umetulia, una amani na furaha. Ukizidisha vipimo husababisha usingizi, upungufu wa umakini na uwezo wa kuona, kizunguzungu, kutapika na kutokwa jasho. Vilevile kipimo kingi kinaweza kusababisha usingizi wa muda mrefu, kuzimia na hata kifo.

Pombe za kienyeji kama gongo ni hatari kwa afya na zinaweza kusababisha upofu na hata kifo.
Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa vijana kuhimili na kutatua matatizo yao ya kijamii na kiakili. Hii husababisha vijana kuwa wepesi kujihusisha na ujambazi na mambo ya ngono na ugomvi, mabadiliko hayo ya tabia husababisha ugomvi katika familia na kuvunjika kwa urafiki. Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo sababu kubwa ya ajali za barabarani, kujiua na maambukizo mbalimbali.

Tofauti ya VVU na UKIMWI

Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii ngereza ni HIV yaani “Human Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa Kii ngereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni “Acquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, i ikii manisha kuwa mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi haya huitwa UKIMWI.

Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu anayeumwa UKIMWI i itakuwa tayari i i imepungua. Mwili wake utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.

Sababu za matumizi ya dawa za kulevya

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watu kutumia dawa za kulevya, nazo ni kama zifuatazo:
Watu wengi hutumia dawa wakitumaini kusahau matatizo yanayowakabili, wengine hutumia kama viburudisho na wanataka kujionyesha kwamba ni watu wazima na wenye nguvu. Wengine pia huanza kutumia dawa kiutani na hatimaye hushindwa kujizuia kuzitumia. Wengine hutumia kutokana na msukumo wa rika au kutokana na kushawishiwa na watu wengine kwamba dawa za kulevya huwapa raha. Wengine hutumia kutokana na ukali wa maisha, uchovu pamoja na upweke. Kimsingi, dawa za kulevya hazimpatii mtu ufumbuzi wa matatizo, bali humwongezea matatizo mtumiaji.

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama “sukari ya kahawia”.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni i kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.

Shopping Cart
17
    17
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About