Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kushirikiana na mpenzi wako majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha

Jinsi ya Kushirikiana na mpenzi wako majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha

Kushirikiana na mpenzi wako katika majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha ni muhimu katika kuje... Read More
Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kuwa na heshima na uwiano ka... Read More

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Uli... Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika Kujenga Ustawi wa Kihisia na mke wako

Jinsi ya Kusaidiana katika Kujenga Ustawi wa Kihisia na mke wako

Kusaidiana katika kujenga ustawi wa kihisia na mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu na... Read More
Jinsi ya kushirikiana kifedha na Mke wako

Jinsi ya kushirikiana kifedha na Mke wako

Kushirikiana kifedha na mke wako ni muhimu katika kujenga uhusiano imara na kuendeleza maelewano kat... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimaadili na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimaadili na mpenzi wako

Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimaadili na mpenzi wako ni muhimu katika kujenga uhusiano wenye... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi ni muhimu katika kujeng... Read More
Kuweka Nafasi ya Kujifunza na Kukuza katika Mahusiano yako

Kuweka Nafasi ya Kujifunza na Kukuza katika Mahusiano yako

Kuweka nafasi ya kujifunza na kukuza katika mahusiano yako ni muhimu sana. Mahusiano ni kitu kizu... Read More

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

  1. Kujenga mahusiano mazuri ya familia ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtu an... Read More

Njia za Kuimarisha Uaminifu na Uwazi katika Mahusiano yako

Njia za Kuimarisha Uaminifu na Uwazi katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha ya mtu yeyote. Mahusiano yanaweza kuwa ya kimapenzi,... Read More

Njia Rahisi za Kuifanya Familia Yako Iwe na Amani na Furaha

Njia Rahisi za Kuifanya Familia Yako Iwe na Amani na Furaha

Kuwa na familia yenye amani na furaha ni ndoto ya kila mzazi. Hata hivyo, mara nyingi, hali ya ms... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Wakati mwingine haifai kuwa mzaha kuhusu kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo b... Read More