Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Kama mwanamke, unapambana na changamoto nyingi katika maisha yako ambazo zinaweza kukuzuia kufany... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na mitazamo ya kisiasa na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na mitazamo ya kisiasa na mpenzi wako

Kuna kitu kimoja kinachotenganisha watu wengi kwa ujumla, na hasa wapenzi, kitu hiki ni tofauti z... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

  1. Kujenga ushir... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Mara nyingi, kama wanaume, tunataka kuonye... Read More

Jinsi ya Kuvunja Tabia Mbaya na Kujenga Mazingira ya Mabadiliko katika Familia

Jinsi ya Kuvunja Tabia Mbaya na Kujenga Mazingira ya Mabadiliko katika Familia

Kwa kila familia, tabia mbaya zinaweza kuwa tatizo kubwa. Hata hivyo, kutokuwa na mazingira mazur... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Kama wapenzi, tunahitaji kuwa na uhusiano mzuri na kudumisha stadi za mawasiliano ili kuboresha u... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Leo tutaongelea kuhusu umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono au kufanya ... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Mahusiano ya mbali ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi, haswa katika ulimwengu wa leo ambapo ... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Mahusiano ... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu na Kujenga Imani katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu na Kujenga Imani katika Familia

Katika familia, ushirikiano wenye uaminifu na imani ni muhimu sana kwa ustawi wa kila mmoja. Ni m... Read More

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakua na kujifunza maadili y... Read More

Kufikia Kilele: Umuhimu wa Ushirikiano wa Kufikia Kilele katika Kufanya Mapenzi

Kufikia Kilele: Umuhimu wa Ushirikiano wa Kufikia Kilele katika Kufanya Mapenzi

Mapenzi ni hisia za moyoni ambazo zinaweza kumfanya mtu kufikia kilele cha furaha na utimilifu wa... Read More