Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Featured Image

Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.





Yafuatayo ni mambo yakufanya ili kumvutia mwanamke.





1. Kuonyesha kuwa unamjali





Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.





2. Kuonyesha kuwa karibu na kupatikana unapohitajika





Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.





3. Kumsifia na kumuonyesha kuwa ni bora





Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.







[products columns="2" ids="30827"]





4. Kupewa kipaumbele





Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.





5. Usafi binafsi





Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.





6. Anavutiwa na mwanamme anayejiamini





Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.





7. Malengo ya maisha





Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.





8. Anayeweza kujitetea





Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.





9. Anayemtosheleza tendo la ndoa





Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.







Ili kufahamu mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu wanawake, Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Kuwa msaada katika safari ya kiroho ya mke wako ni jambo muhimu katika kujenga uhusiano wa kiroho na... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Uwiano na Kustawisha Maendeleo ya Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Uwiano na Kustawisha Maendeleo ya Familia

Kuweka kipaumbele cha kuishi kwa uwiano na kustawisha maendeleo ya familia ni jambo muhimu sana k... Read More

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwasaidia Watoto Kufanikiwa Shuleni na Maisha

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwasaidia Watoto Kufanikiwa Shuleni na Maisha

Karibu kwenye makala hii ambayo itakupa mwongozo wa jinsi ya kuunda mazingira ya kuwasaidia watot... Read More

Je, watu wanpendelea kutumia njia za asili za kupanga uzazi?

Je, watu wanpendelea kutumia njia za asili za kupanga uzazi?

Karibu kwenye makala hii kuhusu kwa nini watu wanapendelea njia za asili za kupanga uzazi. Kupang... Read More

Jinsi ya Kujenga Mawazo chanya na Matumaini katika Familia

Jinsi ya Kujenga Mawazo chanya na Matumaini katika Familia

Kujenga mawazo chanya na matumaini katika familia ni muhimu sana. Ni muhimu kwa sababu inasaidia ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya burudani na likizo

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya burudani na likizo

Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya burudani na likizo ni njia nzuri ya... Read More
Jinsi ya Kuanzisha Mazungumzo ya Wazi kuhusu Kufanya Mapenzi na Mapenzi

Jinsi ya Kuanzisha Mazungumzo ya Wazi kuhusu Kufanya Mapenzi na Mapenzi

Kufanya mapenzi ni kitu ambacho wengi wetu tunakifurahia. Hata hivyo, ni muhimu kujadili kwa wazi... Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika Kujenga Ustawi wa Kihisia na mke wako

Jinsi ya Kusaidiana katika Kujenga Ustawi wa Kihisia na mke wako

Kusaidiana katika kujenga ustawi wa kihisia na mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu na... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu uwekezaji na mipango ya fedha ya baadaye

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu uwekezaji na mipango ya fedha ya baadaye

Mahusiano ya kimapenzi huwa yanahitaji ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya kuweza kufanikiwa. Ni m... Read More

Jinsi ya Kushughulikia Uaminifu na Udanganyifu wa mke wako

Jinsi ya Kushughulikia Uaminifu na Udanganyifu wa mke wako

Kushughulikia uaminifu na udanganyifu katika ndoa ni suala nyeti na linalohitaji mchakato wa kina. H... Read More
Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Unapokwenda kwenye tarehe ya kwanza na msichana, ni muhimu sana kufikiria njia za kufanya tarehe ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na Msichana kwa Ujasiri na Uhakika

Jinsi ya Kuwasiliana na Msichana kwa Ujasiri na Uhakika

Kila mtu anapenda kuwasiliana na mtu mwingine kwa ujasiri na uhakika, hasa wanapojaribu kuwasilia... Read More