Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.


Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.


Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.


Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”


Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.


FUNZO:


Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.


Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.


1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.


2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.


3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.


Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.


Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.


*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.


Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa na maji... Read More

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

  1. Kujenga mahusiano mazuri ya familia ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtu an... Read More

Ndoa sio utani. Soma stori hii

Ndoa sio utani. Soma stori hii

"Mkeo amefariki. Rudi nyumbani kwako haraka sana" Hezron alimwambia Daniel katika simu.

"Mk... Read More

Jinsi ya Kufanya Familia kuwa Mazingira ya Kujifunza na Kubadilisha Maisha

Jinsi ya Kufanya Familia kuwa Mazingira ya Kujifunza na Kubadilisha Maisha

  1. Familia ni moja ya mazingira ya kujifunza na kubadilisha maisha. Kwa hivyo, ni muhimu k... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia muda mwingi katika mchezo wa hatua wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia muda mwingi katika mchezo wa hatua wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki, leo tutajadili kuhusu swali linaloulizwa sana kuhusu watu kwa nini wanapendel... Read More

Jinsi ya Kuwa na Siku ya Kumbukumbu ya Kipekee na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Siku ya Kumbukumbu ya Kipekee na Msichana

Kumbukumbu zetu ni muhimu sana katika maisha yetu. Siku ya kumbukumbu ni siku muhimu sana kwa sab... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kusimamia Fedha katika Mahusiano

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kusimamia Fedha katika Mahusiano

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kusimamia Fedha katika Mahusiano

Karibu katika makal... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Kusudi na Kuunga Mkono Malengo ya Kibinafsi katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wenye Kusudi na Kuunga Mkono Malengo ya Kibinafsi katika Mahusiano

Kujenga ushirikiano wenye kusudi na kuunga mkono malengo ya kibinafsi katika mahusiano ni muhimu ... Read More

Jinsi ya Kukuza Utatuzi wa Mizozo na Ushirikiano katika Familia Yako

Jinsi ya Kukuza Utatuzi wa Mizozo na Ushirikiano katika Familia Yako

Familia ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Hata hivyo, tofauti za kifikra, tabia, na mengine... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Uwiano na Kuhamasisha Uadilifu katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Uwiano na Kuhamasisha Uadilifu katika Familia

Kujenga Ushirikiano Wenye Uwiano na Kuhamasisha Uadilifu katika Familia

Familia ni moja ya... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo yenye Matokeo Matarajio na Wanafamilia

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo yenye Matokeo Matarajio na Wanafamilia

Mazungumzo ni sehemu muhimu sana ya uhusiano wa familia. Hata hivyo, kama si kwa ustadi, mazungum... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kijamii na kujitolea

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kijamii na kujitolea

Mawasiliano ndio msingi wa mahusiano yoyote ya kimapenzi. Kuwa na uwezo wa kuzungumza na mpenzi w... Read More