Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

Featured Image

BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANGU

Duna Lawrence (78) ni raia wa Togo ambaye alijitosa kwenda nchini Ujerumani kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya 80. Baada ya kufika huko, alipata kazi, akawa muaminifu kwa Bosi wake ili aweze kupata mafanikio.

Baada ya miaka mingi kupita, Duna alirudi nchini mwake kwa mara ya kwanza na akaoa, kisha kurejea tena Ujerumani. Bwana Duna aliendelea kufanya kazi kwa bidii huku mafanikio yake kimaisha yakizidi
kushuka chini, akaomba kuongezewa mshahara ili kukidhi mahitaji yake, lakini hiyo haikumpa unafuu.

Jamaa huyu bado hakuona mafanikio yoyote, kazi zikaendelea kuwa nyingi, familia yake nayo ikawa kwenye wakati mgumu. Bwana Duna umri ulizidi kumtupa mkono, huku akijiona hana chochote cha kujivunia katika kazi anayofanya.

Duna akawa mzee, nguvu nazo zikamuisha, ufanisi kazini ukapungua na magonjwa ya kiutu uzima yakaanza kumwandama, akamweleza Bosi wake hali halisi ya kiafya, akaomba alipwe stahiki zake ili arudi nyumbani. Bosi wake alimwonea huruma Mzee Duna, ila hakuwa na namna nyingine ya kumsaidia zaidi ya kumpa stahiki zake zote. Mzee Duna alirejea nchini Togo.

Mzee Duna akiwa anapekua begi lake wakati wa usiku, alikutana na barua ikiwa na dola 2000 na kuandikwa maneno haya:

"… Duna umefanya kazi kwa muda mrefu lakini ulishindwa kuniuliza jinsi ya kuwa tajiri kama mimi, hilo hukuliona kuwa na maana kwako, ukang'ang'ania kuongezwa mshahara na kudai malimbikizo yako, halikuwa jambo baya, ni haki yako. Ulikuwa kama mfungwa kwangu kwa sababu ya kufanya kazi ukitegemea kupata pesa, uliitumikia pesa kwa muda mrefu na haikuweza kukuondolea umasikini. Ninachokushauri, licha ya umri kuwa mkubwa ila anza kujali mambo yako, Mind Your Own Business, Not Another One's. Tumia pesa niliyokupatia kujali mambo yako, umejali mambo yangu kwa muda mrefu sana, jifunze kujali shughuli zako… "

Mzee Duna alisikitika sana, akatoa machozi kwa uchungu, hakujali suala la umri kumtupa mkono, akajitosa kutafuta fursa mbalimbali ndani ya nchi yake akiwa na mtizamo tofauti kuhusu pesa. Mzee Duna alifungua mgahawa, akaajiri vijana kadhaa kwa ajili ya kumsaidia kuwahudumia wateja. Biashara ikawa nzuri, akazidi kutanua biashara yake, akaongeza eneo ili kuwahudumia wateja wengi zaidi. Mzee Duna alipata maeneo kadhaa, akafungua migahawa mikubwa na kuipa jina la "MIND YOUR OWN BUSINESS RESTAURANT".

Nini tunajifunza?

Ifikie wakati kila mtu aanze kujali mambo yake katika kuamua hatima ya maisha yake kiuchumi. Kuendelea kuomba nyongeza ya mshahara, malipo ya ziada, na malupulupu mbalimbali hayatakufanya ujitegemee kiuchumi, bali kuwa tegemezi. Una miaka zaidi ya kumi kazini lakini bado huna uchumi imara, jaribu kujiuliza unamtajirisha nani, nani ananufaika kupitia jasho lako. Lazima ukumbuke kuwa maisha yako yote hayataishia kwenye kazi tu, kuna kipindi hutaweza kufanya kazi kabisa. Je, utaishi kwa njia gani? Anza kufikiria kuhusu maisha yako, timiza ndoto yako na si ya mtu mwingine. Anza kutengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya kujiajiri, usiache kazi kwa papara.

1.Tafadhali fuata hatua makini ili uanze kujali mambo yako.

2.Usifikiri kile wanachofikiri wengi ndicho sahihi.
Fikiri kile kinachokunufaisha wewe ndicho sahihi.

2.Jua maana ya mafanikio!Je, ni kumiliki pesa, vipi kuhusu afya?

Je, mafanikio ni afya, kula vizuri, kuvaa na kula vizuri?Vipi kuhusu mahusiano mazuri ya kijamii na Mungu wako?

Je, maisha ni mahusiano mazuri na Jamii na Mungu?Vipi kuhusu ubinafsi uchoyo na fitna moyoni mwako?

Penda wenzako kwa dhati!Mjue Mwenyezi Mungu wa kweli, Simama imara katika matendo na akili yako.Heshimu na waheshimu wenye mamlaka ama amali za kijamii.

Furahi, ona mbali,fanya kazi, zingatia afya, Mjue Mungu wa Kweli. pumzika vizuri!

Mungu akubariki!

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa k... Read More

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hu... Read More

Una thamani gani?

Una thamani gani?

Kazi au shughuli unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?unawasaidia au unawaumiza??
Biasha... Read More

Kukataliwa ni mtaji

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali y... Read More

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utaku... Read More

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho... Read More

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Sikiliza, hakuna haja ya kuketi chini ili kuelewa ujumbe huu: Ukweli unabak... Read More

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana... Read More

Jaribu kufikiria haya

Jaribu kufikiria haya

1. Uelekeo ni muhimu kuliko kasi. Ni heri kwenda taratibu katika Uelekeo sahihi, kuliko kwenda kw... Read More

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitu... Read More

UKWELI KUHUSU MSHAHARA

UKWELI KUHUSU MSHAHARA

1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku uta... Read More