Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Mahusiano ya kimapenzi kati ya msichana mwenye umri mdogo na watu wazima

Featured Image

Inawezekana kwa msichana mdogo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwenye umri mkubwa. Hata hivyo uzoefu umeonyesha kwamba uhusiano kama huo mara nyingi unakuwa mgumu. Kwanza kabisa ni suala la upevu wa akili na uwiano wa jinsi ya kufurahia maisha.

Kwa mfano, vijana ambao hawajapishana sana umri (miaka ishirini na zaidi) wanaweza kuongea, kujadiliana na kuelimishana kuhusu mambo yao. Lakini inapotokea umri umepishana sana, mvuto wao wa maisha unakuwa tofauti vilevile. Kwa kuongezea, mzunguko wao wa watu wa rika utakuwa wa umri tofauti na watakuwa na mambo machache sana ambayo yatawafurahisha wote wawili kwa pamoja. Mara nyingi, hili linaweza kuleta mtafaruku kati ya msichana na mume wake na kusababisha kuwa na uhusiano wa juujuu.

Pili, kuna shaka kidogo kuhusu kulea watoto. Kumlea mtoto mpaka afikie umri mkubwa wa kuweza kujitegemea na kufanya maamuzi yake mwenyewe, kunahitaji nguvu nyingi. Sasa iwapo mume naye amezeeka na anahitaji kutunzwa itamuwia vigumu sana mwanamke kutekeleza majukumu yote mawili kwa ufanisi, ili kuhakikisha kuwepo kwa maendeleo mazuri ya familia.

Kwa kuongezea mwanaume mzee anaweza kupungua nguvu na hamu ya kutaka kujamiiana wakati msichana hamu yake iko juu. Hili linaweza kuleta ugomvi mkubwa kati yao.

Pia ni muhimu kukumbuka kuwa wanaume wenye umri mkubwa tayari watakuwa wamekuwa na wapenzi wengi kabla yako. Kwa hiyo ni muhimu kwako kumtaka aende kupima virusi vya UKIMWI kabla ya kuanza uhusiano wa kimwili.

Unapofikiria uhusiano na mwanaume mwenye umri unaozidi umri wako sana, fikiria hoja zilizoandikwa hapo juu na angalia hali yako. Mara nyingi ni rahisi kudumisha uhusiano, ukiolewa na mtu ambaye mnalingana umri.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kwa nini watu wanakuwa wagomvi na wakali wanapokuwa wamelewa?

Kwa nini watu wanakuwa wagomvi na wakali wanapokuwa wamelewa?

Madhara ya pombe husababisha watu walioolewa kugombana.
Kutokana na ushawishi wa pombe watu ... Read More

Nini kifanyike ili kurekebisha matatizo ya macho ya Albino?

Nini kifanyike ili kurekebisha matatizo ya macho ya Albino?

Kuishi kwa kushindwa kuona sawasawa ni changamoto ya
msingi waliyonayo Albino, inaathiri eli... Read More

Nini maana ya neno Albino?

Nini maana ya neno Albino?

Neno Albino linamaanisha mtu mweupe, linatokana na neno la lugha ya Kilatini - albus-linamaanisha β€... Read More
Je, unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara na kunywa pombe?

Je, unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara na kunywa pombe?

Ndiyo. Unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara au kunywa
pombe. Lakini pale tu utakapozidisha... Read More

Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?

Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?

Hapa Tanzania matumizi, umilikaji, usafirishaji na kuhusika katika dawa za kulevya kama vile bang... Read More

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Kila mwanaume anatamani kumpata m... Read More

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Kuna magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana ni kisonono, kaswende, klamdi... Read More
Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugum... Read More

Je, inafaa kuzungumzia kuhusu historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano?

Je, inafaa kuzungumzia kuhusu historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano?

Je, kuna haja ya kuzungumzia historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano? Jib... Read More

Je, nini imani ya watu katika kutumia mawasiliano ya kimwili kama ishara ya mapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kutumia mawasiliano ya kimwili kama ishara ya mapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kutumia mawasiliano ya kimwili kama ishara ya mapenzi wakati wa ngo... Read More

Msichana akijamiiana mara moja tu anaweza akapata mimba?

Msichana akijamiiana mara moja tu anaweza akapata mimba?

Msichana anaweza kupata mimba akijamii ana mara moja tu. Inategemea na mzunguko wa hedhi. Kama nd... Read More

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Sababu mojawapo ni kuwa bangi hulimwa hapa nchini na
hivyo hupatikana kwa urahisi. Bangi huu... Read More