Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Kuna madhara mengi ambayo hutokana na uvutaji sigara.
Madhara mengi yanampata mvutaji kwani ...
Read More
Kama umebakwa au kulazimishwa kujamiiana unaweza kupata
huduma katika hospitali, kituo cha a...
Read More
Watoto wengi wanaozaliwa na ualbino, wazazi wao wana rangi
ya ngozi, nywele na macho inayafa...
Read More
Siyo rahisi kusema ni nani anayestarehe zaidi ya mwenziwe, kwa sababu starehe inayotokana na mwan...
Read More
Ndiyo. Hapa Tanzania kuna kitengo maalumu kinachojishughulisha
na masuala ya akili. Wataalam...
Read More
Jinsi ya Kuepuka Kupotoshwa kuhusu Ngono na Mitandao ya Kijamii π±ππ
Karibu vijana...
Read More
Leo hii tutazungumzia kuhusu masuala ya kutafuta tarehe ya muda mrefu na msichana. Inawezekana um...
Read More
Wakati wa kutumia kondomu ya kiume ni muhimu kufuata hatua zifuatazo. Hakikisha kwamba pakiti ina...
Read More
Kujenga ukaribu wa kiroho na msichana katika uhusiano ni jambo muhimu sana. Uhusiano wa kimapenzi...
Read More
Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati wa kumnyonyesha?
Ndiyo, mama mwenye vi...
Read More
Habari yako rafiki yangu? Leo nataka kuzungumzia suala ambalo limekuwa likiwasumbua wengi kwa mud...
Read More
Jinsi ya Kuheshimu Maamuzi ya Mwenzi Wako kuhusu Ngono π
Karibu kwenye makala hii nzuri...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!