Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Matatizo yanayotokana na ujauzito katika umri mdogo

Featured Image

Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi 20. Kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri. Viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini. Vilevile mfupa wa nyonga bado mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupitia wakati wa kuzaliwa.
Wasichana chini ya miaka 18 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo, hasa wakati wa kujifungua. Matatizo hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kuumwa uchungu kwa muda mrefu, kukwama kwa mtoto, kujifungua kwa njia ya operesheni, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Mwili huwa na mahitaji makubwa wakati wa ujauzito na kujifungua na mwili wa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 huwa haujakomaa vya kutosha kwa kazi ya kubeba mimba.
Mbali ya shida za kiafya, kuna matatizo mengine yatokanayo na kupata mimba mapema. Mara nyingi msichana na mwenzie wanakuwa bado wanasoma shule, msichana hufukuzwa shule na hata hutengwa katika jamii . Vijana mara nyingi hawana mapato ya kumlea na kumtunza mtoto, na mahali pa kuishi huwa hawana. Vilevile mvulana mara nyingi hayuko tayari kuchukua jukumu la kuwa baba. Kwa sababu hizi zote, ni vizuri zaidi mimba zitungwe baada ya msichana kufikia umri wa miaka 18.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Ni kweli kuwa daktari anaweza kufanya vipimo vya kugundua
kama mtoto aliye tumboni ni mwenye... Read More

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Karibu ndugu yangu kwenye makala hii ambao inazungumzia njia mbalimbali ambazo utaweza kutumia ku... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Habari zenu wapenzi wa Mapenzi! Kuna umuhimu mkubwa sana wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhus... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Wanawake ni vipenzi vya thamani sana katika m... Read More

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa ni ile ambayo mwanamume au mwanamke
anaozwa bila yeye mwenyewe kukubali... Read More

Je, ni muhimu kuzungumzia kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kabla ya kuingia katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuzungumzia kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kabla ya kuingia katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuzungumzia upendeleo wako wa ngono kabla ya kuingia katika uhusiano? Jibu ni ndio!... Read More

Je, ni kweli ukinywa maziwa baada ya kuvuta sigara huwezi kudhurika?

Je, ni kweli ukinywa maziwa baada ya kuvuta sigara huwezi kudhurika?

Hapana. Hii si kweli kwa sababu maziwa hayawezi kuondoa
uharibifu uliosababishwa na nikotini... Read More

Nifanyeje Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba?

Nifanyeje Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba?

Nifanyeje Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba? 🌸🌍

Read More
Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusiano wa ngono wakati wa kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusiano wa ngono wakati wa kufanya mapenzi?

Leo tutazungumzia kuhusu imani za watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusi... Read More

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia: 1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa t... Read More
Je, ni kweli kwamba mwanamke akikaa muda mrefu akiwa bikira ni shida sana kuvunja kizinda akijamiiana kwa mara ya kwanza?

Je, ni kweli kwamba mwanamke akikaa muda mrefu akiwa bikira ni shida sana kuvunja kizinda akijamiiana kwa mara ya kwanza?

Ile ngozi ndani ya uke i inabakia kuwa nyembamba na laini sana, hata mwanamke akiwa bikira katika... Read More

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu san... Read More