Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Featured Image

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama “sukari ya kahawia”.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni i kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ualbino husababishwa na nini?

Ualbino husababishwa na nini?

Watu wenye ualbino hawana uwezo kabisa au wana uwezo mdogo wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele... Read More
Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake... Read More

Je, Ni Lazima Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Marafiki au Shinikizo za Kisiasa?

Je, Ni Lazima Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Marafiki au Shinikizo za Kisiasa?

Je, ni lazima kufanya ngono kwa sababu ya marafiki au shinikizo za kisiasa? 🤔

Ndugu vij... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Kila mtu anataka kuwa na mvuto wa kipekee kwa msichana. Lakini je, unajua jinsi ya kuwa na mvuto ... Read More

Je, kuna tofauti za kitabia katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kitabia katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kitabia katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna! Ili kufurahi na kufikia kil... Read More

Ubikira ni nini?

Ubikira ni nini?

Maana halisi ya neno “bikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj... Read More

Njia za Kujenga Ushirikiano na Msichana katika Malengo ya Pamoja

Njia za Kujenga Ushirikiano na Msichana katika Malengo ya Pamoja

Kuwashirikisha wasichana katika malengo ya pamoja ni jambo muhimu sana katika jamii yetu. Wasicha... Read More

Je, uume una urefu kiasi gani? Ni kweli kwamba wanaume warefu wana uume mkubwa na wale wafupi wana uume mdogo?

Je, uume una urefu kiasi gani? Ni kweli kwamba wanaume warefu wana uume mkubwa na wale wafupi wana uume mdogo?

Kwa kawaida urefu wa uume ambao haujasisimuka kwa wastani ni kati ya sentimeta 7 na 10, na uume ... Read More

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Watu huogopa kujaribu vitu au mambo ambayo hawajayazoea
au yale ambayo yapo tofauti. Jinsi u... Read More

Watu wanaamini kuwa Albino wana joto katika mapenzi kuliko watu weusi, Je, hiyo ni kweli?

Watu wanaamini kuwa Albino wana joto katika mapenzi kuliko watu weusi, Je, hiyo ni kweli?

Hii siyo kweli,
tofauti
baina ya Albino
na mtu a s i
ekuwa na ualbino
i ... Read More

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Habari za leo wapenzi wangu! Nami nina furaha sana kuwa hapa leo kuongelea kuhusu swala la ngono ... Read More

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More