Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
Dalili
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
· Kushindwa kupumua vizuri
· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
· Kucha kuwa dhaifu
· Kusikia hasira na kuhamasika haraka
· Kuchoka sana kuliko kawaida
· Maumivu makali ya kichwa
· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
· Uchovu wa mara kwa mara
Matibabu.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Tafadhali soma na uwapelekee wengine.
Dr. Chriss Mosby wa Tanzania amegundua kensa mpya kwa...
Read More
Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini i...
Read More
Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha n...
Read More
Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.
Ukipatw...
Read More
Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafut...
Read More
Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchuk...
Read More
Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubong...
Read More
Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ...
Read More
Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids....
Read More
Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:...
Read More
Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika du...
Read More
Tunda asili yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linaj...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!