Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga

Featured Image

Vipimo Vya Ugali:

Unga wa mahindi/sembe - 4

Maji - 6 takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chota unga kidogo katika kibakuli uchanganye na maji kidogo .
Weka maji mengineyo katika sufuria kwenye moto.
Changanya na mchanganyiko mdogo ufanya kama uji.
Kisha kidogo kidogo unaongeza sembe huku unakoroga na kuusonga ugali hadi uive.

Vipimo Vya Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi

Samaki nguru - 5 vipande

Pilipili mbichi ilosagwa

Kitunguu maji kilosagwa - 1 kimoja

Nyanya ilosagwa - 2

Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ¼ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Ndimu - 2 kamua

Tui la nazi zito - 2 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Baada ya kumuosha samaki, weka katika sufuria.
Tia chumvi, ndimu, pilipili mbichi ilosagwa.
Tia vitunguu na nyanya zilosagwa
Mkaushe kwa hivyo viungo, akianza kukauka tia tui la nazi.
Acha kidogo tu katika moto tui liwive mchuzi ukiwa tayari.

Vipimo Vya Bamia

Bamia - ½ kilo takriban

Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai

Methi/uwatu/fenugreek seeds ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Dania/corriander ilosagwa - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Mafuta - 1 kikombe cha kahawa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata bamia kwa urefu.
Weka mafuta katika karai, kisha tia bizari zote na nyanya kopo, kaanga kidogo.
Tia bamia endelea kukaanga, kisha acha katika moto mdogomdogo ufunike.
Kila baada ya muda funua karai ukaange bamia hadi ziwive zikiwa tayari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

1. Chakula

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimb... Read More

Mapishi ya tambi za mayai

Mapishi ya tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina... Read More

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Kama mzazi au mlezi, mara nyingi... Read More

Mapishi ya Chicken Curry

Mapishi ya Chicken Curry

Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).

Mahitaji

... Read More
Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mahitaji

Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe

Kuku

Vitunguu - 3

Nyany... Read More

Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Viamba upishi

Unga wa ngano 1 Kilo

Siagi ¼ kilo

Mayai 2

Kastadi (custa... Read More

Mapishi ya Maharage na spinach

Mapishi ya Maharage na spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji ... Read More

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)

VIAMBAUPISHI

Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe... Read More

Mapishi ya Pilau Ya Sosi Ya Soya Na Mboga

Mapishi ya Pilau Ya Sosi Ya Soya Na Mboga

Viambaupishi

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) 3 magi

<... Read More
Mapishi ya Kidheri - Makande

Mapishi ya Kidheri - Makande

Mahitaji

Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo

Maharage - 3 vikombe

Mahin... Read More

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Vipimo vya Wali:

Mchele basmati - 3 magi (kikombe kikubwa)

Mchanganyiko wa mboga za... Read More

Mapishi ya Ndizi na samaki

Mapishi ya Ndizi na samaki

Mahitaji

Ndizi laini (Matoke 6)
Viazi mbatata (potato 3)
Samaki wabichi wa wast... Read More