Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ujasiri na kujiamini

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ujasiri na kujiamini

Kuwa na ujasiri na kujiamini ni muhimu katika mahusiano, lakini mara nyingine tunaweza kukosa uja... Read More

Jinsi ya Kuunda Amani na Furaha katika Familia Yako

Jinsi ya Kuunda Amani na Furaha katika Familia Yako

Kuunda amani na furaha katika familia yako ni muhimu sana. Familia ni eneo la usalama, upendo na ... Read More

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio! Kuna tofauti kubwa sana kati ya wa... Read More

Kukuza Urafiki na Upendo katika Familia Yako ili Iwe na Amani na Furaha

Kukuza Urafiki na Upendo katika Familia Yako ili Iwe na Amani na Furaha

Kufanya familia yako kuwa na upendo na amani inahitaji jitihada kutoka kwa kila mmoja. Ni muhimu ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na wafanyakazi wenzake

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na wafanyakazi wenzake

Wakati mwingine, inaweza kuwa changamoto kupata njia ya kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga ... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Uimara na Uthabiti wa Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Uimara na Uthabiti wa Ndoa na mke wako

Kuimarisha uimara na uthabiti wa ndoa na mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano wa ndoa wenye ... Read More
Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Kama wapenzi wapya au wapenzi wa muda mrefu, ni muhimu sana kujadili matarajio ya ngono/kufanya m... Read More

Mazungumzo ya Wazi kuhusu Fedha: Ujenzi wa Ustawi wa Familia

Mazungumzo ya Wazi kuhusu Fedha: Ujenzi wa Ustawi wa Familia

Mazungumzo ya wazi kuhusu fedha ni hatua muhimu kuelekea ustawi wa familia. Hii ni kwa sababu, ka... Read More

Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Kila familia inahitaji kuwa na uhusiano thabiti na wa upendo ili iweze kukua na kuwa bora. Ni muh... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kifedha na matumizi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kifedha na matumizi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kifedha na matumizi ni muhimu katika kujenga uelewano n... Read More
Jinsi ya kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi

Jinsi ya kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi

Kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi ni jambo muhimu katika kujenga ndoa yenye furaha na afy... Read More
Jinsi ya kuimarisha uhusiano wa kijamii na mke wako

Jinsi ya kuimarisha uhusiano wa kijamii na mke wako

Kuimarisha uhusiano wa kijamii na mke wako ni muhimu katika kujenga ndoa imara na yenye furaha. Hapa... Read More