Kuhusu Ubatizo, Haya ndiyo mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu

Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?
Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Updated at: 2024-05-27 06:44:48 (11 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?
Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
โNami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenuโ (Ez 36:26-27).
โKisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kungโaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwanakondooโ (Ufu 22:1).
Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu lini?
Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha waamini walivyotekeleza agizo hilo katika mazingira mbalimbali, sio tu yalipopatikana maji mengi. Hivyo Paulo alipokuwa ndani ya nyumba โakasimama akabatizwaโ (Mdo 9:18).
Kumbe Yohane Mbatizaji hakusogea mbali na mto Yordani, akisubiri watu wamuendee kutoka maeneo yote ya nchi ile kame.
โAlikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji teleโ (Yoh 3:23).
Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?
Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote.
โKweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa motoโ (Math 3:11).
Paulo aliuliza watu, โโMlibatizwa kwa ubatizo gani?โ Wakasema, โKwa ubatizo wa Yohaneโ. Paulo akasema, โYohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesuโ. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesuโ (Mdo 19:3-5).
Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni zipi?
Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti inategemea imani kwa Kristo na kutushirikisha kifo na ufufuko wake.
โMaana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristoโ (Gal 3:27).
Ndivyo inavyoondolea dhambi zote na kuingiza katika uzima wa Utatu Mtakatifu. Kwa sababu hiyo Yesu aliagiza tubatizeย โkwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifuโ (Math 28:19).
Maneno hayo ndiyo muhimu zaidi katika sakramenti hiyo. Maji peke yake, hasa yakiwa mengi, yanaweza kuosha mwili, lakini si roho. Kumbe ubatizo unaotuokoa
โsiyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Munguโ (1Pet 3:21).
Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?
Ndiyo, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwakeย โalichukizwa sana, akawaambia, โWaacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisaโ (Mk 10:14-15).
Yeremia aliambiwa,
Yeremia aliambiwa,
โKabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifaโ (Yer 1:5).
Yohane Mbatizaji alitabiriwa โatajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamayeโ (Lk 1:15).
Mitume walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu.
Walibatizwa โyeye na nyumba yakeโ,ย โyeye na watu wake woteโย (Mdo 16:15,33);
โwatu wa nyumbani mwa Stefanaโ (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.
Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?
Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani.
โVinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvuโ (Zab 8:2).
โElisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu,ย kitoto kichangaย kikaruka ndani ya tumbo lakeโฆ kwa shangweโ (Lk 1:41,44).
โNakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zakoโ (Math 11:25-26).
Je, watu wazima wanaweza kuelewa sakramenti kwa dhati?
Hapana, watu wazima hawawezi kuelewa sakramenti kwa dhati, kwa kuwa zote ni mafumbo yanayotuzidi. Basi, kama Petro alipooshwa miguu, tumuachie Bwana atufanyie kazi anavyojua yeye.
โNifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadayeโ (Yoh 13:7).
Kisha kuoshwa tuzidi kuchimba mafumbo hayo kwa mwanga wa Neno na wa Roho Mtakatifu.
โJe, mmeelewa na hayo niliyowatendea?โฆ Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyoโ (Yoh 13:12,15).
Je, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto?
Ndiyo, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto kama wengine pia.
Walimletea Yesu โmtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanneโฆ Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, โMwanangu, umesamehewa dhambi zakoโ (Mk 2:5).
Yesu aliiona imani yao akamponya. Imani ya watu wengine ndio ilivyopelekea kuponywa kwa huyu mtu. Vivyo hivyo Imani ya Mzazi inaweza kumsaidia mtoto.
Kwa ubatizo watoto wanaunganishwa naye na kuanza kuponywa madonda ya dhambi ya asili.
โTazama, mimi naliumbwa kati hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatianiโ (Zab 51:5).
โIkiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristoโ (Rom 5:19).
Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?
Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.
โHata zilipotimia siku nane za kumtahiri,ย aliitwa jina lake Yesuโย (Lk 2:21).
Watu wa mataifa walipoongokea dini hiyo, walioshwa na kutahiriwa pamoja na watoto wao. Mitume pia walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu. Walibatizwa โyeye na nyumba yakeโ, โyeye na watu wake woteโ (Mdo 16:15,33); โwatu wa nyumbani mwa Stefanaโ (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.
Kwa Kanisa Katoliki, ubatizo sio ukamilifu wa kuwa Mkristo. Ubatizo ni Sakramenti ya kwanza ambayo inakamilishwa na Sakramenti ya Kipaimara ambayo humfanya Mkristo kuwa mkamilifu kwa kukiri na kuahidi mwenyewe kuwa Mfuasi wa Yesu Kristu kwa kumkataa Shetani na Mambo yake yote. Kwa maana hiyo, watoto wanapobatizwa wazazi wanamtoa au wanamwalika mtoto katika Imani ya Kikristu wakiahidi kumtumza na kumwelekeza katika njia ya Imani kwa Yesu Kristu mpaka atakapokua mkubwa na kuwa na ufahamu na Elimu ya kutosha kuhusu Imani yake ndipo na yeye atakiri na kuahidi mwenyewe wakati wa Sakramenti ya Kipaimara.
Je, ubatizo tuu unatosha?
Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula.
Sakramenti hizo tatu kwa pamoja ni msingi wa maisha ya Wakristo wote, kumbe nyingine zinahitajika tu katika hali na nafasi maalumu. Mitume waliwaendea Wasamaria
โwakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifuโ (Mdo 8:15-16).
โAmin, amin, nawaambieni: Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndaniyenuโ (Yoh 6:53).
Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?
Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake.
โWaliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yaoโ (Mdo 19:5-6).
Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste, ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia Mitume Roho Mtakatifu, ambaye siku hamsini baadaye akawajia kama
โupepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yoteโ (Mdo 2:2).
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.
Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapotulisha na kutunywesha Mwili na Damu yake ili tushiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi.
โAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimiโ (Yoh 6:56-57).
Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani mwetu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.
Sakramenti ya ubatizo ni nini?
Sakramenti ya Ubatizo ni Sakramenti yenye kuondoa dhambi ya asili pamoja na dhambi nyingine zote tulizotenda, kufufua roho zetu kwa kututia uzima wa Mungu, Kutuandika Wakristu Watoto wateule wa Mungu na wa Kanisa.
Ubatizo ni nini?
Ubatizo ni Sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho Mtakatifu, ni mlango (Kiingilio) kwa Sakramenti nyingine zote na ni ufunguo wa uzima wa milele. (Yoh 3:3, Mt28:19)
Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?
Sakramenti ya Ubatizo yatuletea;
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13)
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13)
Kuna Ubatizo wa namna ngapi?
Kuna Ubatizo wa namna tatu;
1. Ubatizo wa maji - Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa - Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu - Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa
1. Ubatizo wa maji - Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa - Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu - Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa
Nani aweza kubatiza?
Mwenye mamlaka ya kubatiza kwa kawaida ni yule mwenye dataja takatifu katika Kanisa, lakini katika hatari ya kufa kila mtu anaweza kubatiza.
Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?
Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu
Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?
Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo
Anayebatizwa yampasa nini?
Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo
Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni kumwagia maji katika panda la uso na kutamka maneno "Fulani (jina lake linatajwa) nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" (Mt 28:19)
Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?
Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;
1. Kutoa mfano mzuri wa maisha ya Kikristo
2. Kumuongoza mbatizwa katika maisha ya Ukristo
3. Kumuombea mbatizwa
4. Kushirikiana na wazazi katika malezi
2. Kumuongoza mbatizwa katika maisha ya Ukristo
3. Kumuombea mbatizwa
4. Kushirikiana na wazazi katika malezi