Stori inayogusa!!

Updated at: 2024-05-23 14:50:16 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku, mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo.
Ā
Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari. Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama. Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali. Ma doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa dk 5 angekufa. Mungu alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini Mungu atakubariki. Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. Mungu huinua vinyonge ilI kuangusha vyenye nguvu. Tuma ujumbe huu wa BARAKA kwa watu japo wanne ili kushiriki BARAKA hizi za Mungu, ujumbe huu waweza tena nitumia nami ktk kutakiana BARAKA za MUNGU WETU.
Updated at: 2024-05-23 14:50:18 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda. Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?
Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote. Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu.
Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo. Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ufanisi.
Kama umeipenda, itume kwa wengine ili nao wazinduke.
Updated at: 2024-05-23 14:50:17 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.
Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.
Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.
Badae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake 'chongo' anayemtia aibu.
Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.
Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.
Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..
Mtoto kwa hasira akamuuliza "mama umekuja kufanya nini hapa? Kama una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako"
Mama yake akasema "samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe". Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.
Baada ya siku chache kupita, yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.
Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.
Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hiviā¦
"Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee⦠Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.
Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa namiā¦.
Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongoā¦.
Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu, wewe ndiye uliyezaliwa ukiwa chongo. Ulikua na jicho moja tu. Nikaumia sana kuona mwanangu ana jicho moja, atawezaje kuishi na kukabiliana na changamoto za maisha.. Nikaomba madaktari wanitoe jicho langu moja wakupe wewe, Niliona ni heri mimi niwe chongo kwa kuwa nimeshaona mengi sana duniani kuliko wewe..
Na ulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza kuzikabili vema changamoto za dunia hii⦠Na hakika jicho langu limekusaidia kwani wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasaā¦
Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kutumia jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care of my eyeā¦
Akupendaye,
Mama"
Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.!
MORAL OF THE STORY.!
Nyuma mafanikio ya kila mwanaume yupo mwanamke. Anaweza kuwa mama yako, mke wako, dada yako au mchumba wako.. Je unatambua nafasi yake katika mafanikio yako au unampuuza tu?
Wapo wanawake ambao walijitoa sadaka ili uweze kuwa hapo ulipo. Jiulize mama yako amefanya mangapi kukufikisha hapo.
Hadithi hapo juu inatueleza juu ya mama aliyetoa jicho lake kwa mwanae.. lakini jicho ni kielelezo tu cha yale wanayofanya mama zetu.
Kuna wengine jicho lao ni vibarua alivyokua anafanya ili wewe usome.. Pengine jicho lake ni namna alivyokua akijinyima kwa kuvaa nguo moja mwaka mzima ili upate ada ya shule na mahitaji mengine.. Je umewahi kumshukuru mama yako kwa kutoa jicho lake kwa ajili yako??
Mpende sana mama yako.. Wapende wanawake wote, waheshimu, walinde, wajali. Wanapitia magumu mengi sana ili kutufanya sisi wanaume tuwe kama tulivyo.
Updated at: 2024-05-23 14:50:15 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto alifanya maamuzi ya kumpeleka baba yake ambaye alikuwa Mzee sana kwenye Makazi Maalum ya kulelea wazee ya Kanisa Katoliki iliyokuwa CHINI ya uratibu wa Padre. Alifanya hivyo Baada ya kushauriwa Na mkewe aliyekuwa akiona Ni kero kumlea baba Mkwe wake nyumbani kwao.
Ofisa katika sehemu ya mapokezi alimuomba Mzee huyo achague chumba Kama anataka chenye TV Na Kiyoyozi Au la; Mzee akasema hahitaji chumba CHOCHOTE Chenye TV wala Kiyoyozi. Mwanaye ALIPOENDA kwenye Gari kuchukua begi la baba yake; mkewe aliyekuwa muda wote kwenye Gari akasisitiza Kuwa amwambie huyo Mzee asirudi nyumbani kabisa HATA Siku Za Sikukuu Kwa sababu yeye Mke hataki usumbufu wowote wa kumhudumia.
Mtoto huyo wa pekee kwa Mzee huyo alishangaa alivyorudi Na mizigo ya baba yake alipokuta Mzee wake akizungumza Kwa bashasha Na Padre wakionekana wanafahamiana sana, maana walionekana wakiongea kwa kukumbushana mambo ya zamani ambapo Mzee alionekana mchangamfu isivyo kawaida. Mtoto akamuuliza Padre "unamfahamu baba Yangu? Maana naona mnazungumza Kwa bashasha sana Kama mnafahamiana"
Padre akajibu "Ndiyo namfahamu sana Huyu Mzee mwema; alikuja HAPA miaka 30 iliyopita tukampatia Mtoto yatima wa kiume akamlee maana Mtoto huyo hakuwa Na WAZAZI Na yeye Na mkewe hawakuwa wamebahatika kupata Mtoto"
Mabegi aliyokuwa kayashika mkononi yalidondoka, akasimama Hapo kimya bila kusema kitu ā¦ā¦
Kisa HIKI kinatoa funzo kubwa sana Kwa kila mtu kuhusu kuwajali Na kuwahudumia WAZAZI wetuā¦..
Updated at: 2024-05-23 14:50:16 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mume alirejea nyumbani na kukuta ujumbe juu ya meza umeandikwa "NIMEONDOKA" ilikuwa jioni, alienda jikoni na kukuta kukavu, aliwaita watoto na kuwauliza wakasema walimuona Mama akiondoka na begi lakini hakuwaambia anaenda wapi. Mume alichanganyikiwa, alijaribu kuchukua simu kumpigia lakini ilikuwa haipatikani, kabla hajafanya chochote mtoto wao wa mwaka mmoja alikuja akilia na kusema ana njaaa.
Ilibidi kuingia jikono na kutaka kupika huku akitukana matusi yote, kila kitu kilikuwa hakuna, hapo ndipo alipokumbuka kua asubuhi mkewe alimuomba pesa ya kununua chakula akamuambia hana afanye maarifa. "Ataondokaje ghafla namna hii, huyu mwanamke mshenzi kabisa.." Aliwaza lakini alikumbuka kuwa asubuhi hiyo hiyo baada ya kumnyima mkewe pesa ya chakula mke alilalamika kua amechoka maisha yale na yeye akamjibu "Kama umkechoka si uondoke, wanawake wako wengi ukiondoa kitu na weka kituā¦"
Akili yake iliwaza sana akakumbuka mchepuko wake, aliupigia simu uje nyumbani, lakini ulistuka kuhusu Mama watoto, akamuambia ameondoka na kamuachia watoto wote wa nne. Mchepuko ulijifanya hausikii vizuri na baada ya muda ukazima simu. Sasa alikuwa amechanganyikiwa, alitaka kupiga simu Kijijini ndipo alikumbuka kuwa hata namba ya Mama mkwe wake alikuwa hana, hakuwa na kawaida ya kuongea nao na mara chache alipoongea ni pale ambapo mkewe alipiga simu na kumuambia kuwa aongea na familia.
Alikumbuka ana namba ya rafiki wa mke wake, akampigia kumuuliza mkewe yuko wapi akasema hajui lakini mara ya mwisho alipompigia alimuambia kuwa "ANAENDA KUPUMZIKA". Alizidi tena kutukana, alitoka jikoni nakuwachukua watoto kwenda kwenye mgahawa alizunguka nao mpaka kupata sehmu ya kula, watoto walifurahi sana siku hiyo kutoka na Baba yao, waliongea na kucheka kula nnje ya nyumbani, kidogo alipata faraja na kutabasmau lakini bado alikuwa akiwaza kuhusu mkewe.
Baada ya kumaliza chakula aliwarudisha watoto nyumbani alitaka kwenda kuwalaza lakini walikataa na kutaka kuogeshwa. Kimbembe kilianza katika kuwaogesha wale wadogo. walihtaji kuoga kwa maji ya moto, alienda moja kwa moja kuwasha jiko la umeme akakuta haliwaki. Akaanza kutukana ndipo alipokumbuka miezi mitatu iliyopita liliharibika na mkewe alipomuambia alisema watumie mkaa, akaenda kwenye jiko la gesi, hata hakuwasha kwani alikumbuka kuwa siku tatu zilizopita mkewe alimuomba hela ya gesi akamtukana mwanamke gani mvivu kuwasha mkaa, anatumia tu hela wakati hana chakufanya.
Alichanganyikiwa zaidi, akaenda kuwalaza watoto kwa lazima lakini ile na yeye anapanda kitandani mtoto mdogo akaanza kulia kwa sauti ya juu, joto, alitaka kuoga, ilibidi kunyanyuka kutaka kuwasha mkaa, atauwashaje hata mafuta ya taa hajui yako wapi labda angeweka ili uwake. Ilibidi kunyanyuka kuwasha TV watoto waliangalia mpaka walipopitiwa na usingizi, hata hakuwanyanyua yeye na watoto walilala, pale pale kwenye kochi mpaka asubuhi. Wote walipitiwa, asubuhi alistuka ameichelewa kazini na watoto walitakiwa kuandaliwa kwaajili ya shule.
Kichwa kilizidi kumuuma, hakujua aanzie wapi aishie wapi, akanunue vitafunwa au apike chai lakini atapika na nini? Akawaambia siku hiyo hakuna kwenda shule, akawasha gari kwenda kununua gesi na vitu vya nyumbani. Bado mkewe alikuwa hapatikani. alinunua jiko na kuja kupika chai akawapa watoto, akaanza kumtumia meseji mkewe za kumuomba msamaha, kumuomba arejee nyumbani kwani peke yake asingeweza kuwale watoto lakini meseji hasikupokelewa.
Simu ilianza kuita, ilikuwa namba ya bosi wake, alikuwa akimhitaji kupeleka taarifa ofisini, aliamua kumtafuta mdogo wake aje akae na wanae lakini naye alikuwa bize na kazi zake. Ili bidi kuwaacha watoto nyumbani na kwenda ofisini hivyo hivyo. Alifika ofisini na kukabidhi taarifa, baada ya muda meseji simu ilipiga kelele kuashiria kuwa meseji alizomtumia mkewe ziliingia, simu ilikuwa imewashwa.
Harakaharaka alinyanyua simu na kupiga, ilipopokelewa alianza kuomba msamaha aliongea maneno mengi ya kujilaumu na kumtaka mkewe kurejea nyumbani. "Wewe ndiyo mume wake?" Upande wapili uliuliza. "Ndiyo! Ndiyo Mimi! Kuna nini kimetokea! Mke wangu kafanya nini?" Aliuliza maswali mfululizo lakini kwa utaratibu upande wapili ulisikika unasema "MImi ni nesi nipo hapa Temeke Hospital mwenye hii simu ameā¦"
Hakusubiri wala amalizie alianza kupiga kelele kulia kwa uchungu, nguvu zilimuishia na kukaa juu ya kochi la mapokezi. Wafanyakazi wenzake walimsogelea kutaka kujua ni nini, bado alikuwa ameshikilia simu, walichukua na kuongea na mtu wa upende wapili. Baada ya muda alisikia wakimuambia "Unalia nini sasa yaani baada ya ufurahi unalia, Hongera mke wako amejifungua mtoto wa kiume.." Alishtuka sana kwani alihisi ni kitu kibaya, hapo ndipo alipokumbuka kuwa mke wake alikuwa mjamzito.
Alikuwa akimuona kila siku lakini kwakuwa alikua hajali hata alikuwa hajui kuwa ujauzito wa mkewe ulikuwa na muda gani? Akili yake ilishatekwa na mchepuko kiasi cha kuisahau familia yake. Aliendelea kulia kwa uchungu uliokuwa umechanganyika na furaha, alifurahia kuwa mkewe yuko salama lakini alipata uchungu kwa ukatili wake kiasi kwamba ameshaau hata kua mkewe alikuwa amekaribia kujifungua.
Haraka haraka aliingia kwenye gari, akaenda hospitallini kumuomba mkewe msamaha,. watuwa lishangaa kumuona amepiga magoti analia kama mtoto mdogo. mkewe alimuambia nilishjakusamehe muda mrefu, naamini sasa unafahamu thamani ya familia. Alinyanyuka na kukuabli kweli sasa anafahamu maana ya familia, siku ile amejifunza mengi kuliko mambo aliyokuwa amejifunza kwa maisha yake yote. Wlikumbatiana na baada ya kuruhusiwa alirejea nyumbani kwake na mkewe, alibadili tabia na kuwa Mume na baba bora.
MWISHO
Updated at: 2024-05-23 14:50:18 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu.
Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani, baadaye tukajaliwa kuwa na watoto wa2 mmoja wa kiume Alfred na mwingine wa kike Minza. Mimi nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda mrefu ktk hospitali za wilayani karatu na Arusha mjini mpk nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu wa mwili na mambo yaliyonipata katika maisha. Mume wangu alikua ni askari polisi mpk baadaye alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti kama nitakavyoeleza baadaye hapo chini.
Tulipooana na mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na mipango mingi mizuri ya kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua tunampenda Mungu na tulikua waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda mrefu katika maisha ya ndoa na familia, baadaye maisha yalianza kuwa magumu kutokana na mishahara yetu kuwa midogo ukilinganisha na mahitaji. Mume wangu alijisikia vibaya sana zaidi yangu hasa pale alipoona wengine hasa marafiki zake wanafanikiwa lkn yeye hafanikiwi. Kuna maaskari walikua wakipandishwa vyeo haraka na kuhamishiwa mijini ikiwemo Daressalaam na Arusha- hali hiyo ilimpa shida sana akawa anaomba na kufunga kwa muda mrefu lkn hakuona mafanikio.
Wakati fulani ilitokea akakutana na rafiki yake askari mwenzie, akamualika nyumbani kwake. Mume wangu aliporudi akaja akiwa mwenye mawazo makubwa sana, sikujua ni kwanini na hukuniambia hata nilipomuuliza.
Baada ya siku kadhaa mume wangu akaacha kwenda kanisani wala huduma hakufurahia tena. Akawa ni mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Siku moja akaniambia atasafiri kikazi kwa muda wa siku tatu. Baada ya siku tatu akarudi akiwa hoi sana na mgonjwa km mtu mwenye malaria. Nikajaribu kumshawishi twende hospitali hakukubali kbs akaniambia ni uchuvo tu wa safari na kazi na atakuwa salama. Kesho yake, kweli akaamka vzr na kwenda kazini bila kuugua km hapo jana. Ikapita muda mrefu bila kujua hasa nini kinachoendelea kwa mume wangu kwani hakuniambia chochote hata nilipomuuliza.
Baada ya muda, mume wangu akapata nafasi ya kwenda masomoni Moshi. Alipomaliza masomo hayo,haikuchukua muda mrefu tukapata barua ya uhamisho wa mume wangu kikaz kuelekea Arusha mjini.
Binafsi nilifurahi sana, nikajua Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya siku nyingi. Kwa hiyo na mimi nikaanza mipango ya uhamisho. Tulipofika Arusha tukapata makazi mapya na kanisa zuri la kuabudia. Baada ya muda niligundua mume wangu hakupenda mambo ya Mungu km siku za zamani. Wakati huu mimi nilikua mjamzito nikijandaa kupata mtoto wa pili.
Tulizungumza sana na mwenzangu lkn sikujua hasa kitu gani kulikua kinamsumbua. Baada ya muda niligundua mume wangu alikua mlevi wa pombe na tabia yake ilibadilika sana hasa kuhusu mambo ya kiimani na kushirikishana mipango. Aligeuka kuwa mtu wa mambo mengi,kuamrisha na msiri sana- kutokana na aina ya kazi zao nikajua ni kawaida.
Nilipojifungua mtoto wetu wa pili akaniletea zawadi ya gari mark2-mimi nilikua miongoni mwa wanawake wachache kuendesha mark2 wakati miaka ya90 mwishoni. Tulijisikia vzr sana na mambo ni kama yalikua yananyooka.
Mwaka 2001 mume wangu alipata nafasi ya kwenda tena chuoni kusoma kwa muda mfupi huko Dar, nikabaki na familia na nikawa naendelea vzr na kazi zangu. Alipomaliza masomo akarudi na maisha yakaendelea kwa muda km kawaida. Baada ya miezi km sita kutoka chuo ni, mume wangu akaniambia anataka kuacha kazi- nilishangaa sana nikamuuliza maswali mengi lkn hukunijibu vzr. Wiki moja baadaye akaniambia ameacha kazi na ameajiriwa shirika moja kubwa la UN hapa Arusha.
Kweli akaanza kuvaa sare mpya za kazi hiyo mpya. Kazi hiyo mpya ilituletea mafanikio makubwa sana ya kifedha na kujieneza kwa mali. Wakati huo pia mimi nilipata nafasi ya kwenda kusoma chuoni muhimbili Dar kwa muda wa miaka mitano. Nikaenda Dar nikaiacha familia ikiendelea vzr kbs.
Nikiwa Dar chuoni nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi kufanya seminar ya health exhibitions (mafunzo ya maonesho)- nikiwa huko nilipigiwa simu kuwa mtoto wetu mdogo amefariki dunia. Nilichanganyikiwa nikarudi nyumbani kwa kuchelewa, nikakuta wameshamzika Alfred mwanangu sikumuona tena. Ilisemekana alifariki ghafla sana bila kujua hasa ni ugonjwa gani au alipatwa na nini mwanangu. Niliongea na madaktari, wakanieleza kuwa mwanangu alitokwa na damu nyingi sana mpk ndani ya jeneza. Uchungu mkubwa na kuchanganyikiwa vilinipata bila kujua hasa nini cha kufanya.
Niliporudi msibani nilishangaa kumkuta mume wangu akiwa na pete kubwa ya dhahabu yenye kinakshi cha tanzanite katikati mkono wa kuume. Nilipomuuliza akaniambia amenunua mjini bei ghali sana na pia ameninulia na mimi aina km hiyo ya pete. Sikujua chochote nikaipokea ile pete km zawadi nikawa naivaa. Pia akaniambia kuna kanisa jipya limeanzishwa hapa mjini ndio tutakua tunasali. Huko tulikutana na watu mbalimbali wa mataifa mengine na ibada zilikua ni za kiingereza. Tulienda kutambulishwa na mume wangu kwa mchungaji ambaye nayepia alikua amevaa pete km ya mume wangu-sikujali sana kwa siku hiyo. Nilijisikia vzr sana kwani huko nilimuona mume wangu akifurahia na kujitoa km zamani. Pia tulipata marafiki wengi akiwemo familia moja ya wakameruni waliokua karibu sana sisi. Tukahamia huko.
Baada ya muda baada ya kuipata ile pete na kurudi chuoni na kujiunga kanisa jipya huku Arusha, sikupenda tena kwenda kanisani wala kujishughulisha na mambo ya huduma kama awali. Nilijiona mwenye majukumu mengi sana na sina muda wa mambo ya kanisani na huduma. Wenzangu waliponiuliza, niliwajibu kuwa niko bize sana na masomo na shughuli za kikazi. Nikawa mzembe sana ktk mambo ya imani na huduma.
Lkn siku moja Nikiwa Dar wakati wa fellowship za chuoni, ndugu mmoja alitutembelea akahubiri kwa nguvu sana akatuambia kuna mtu amezingirwa na roho mbaya za kichawi zinazotafuta kumuangamiza na familia yake-sikuelewa hata kidogo wala hakupita mtu yeyote mbele siku hiyo. Yule muhuburi alilia sana kwa uchungu mpk mwisho wa ibada.
Baada ya kumaliza masomo mwaka 2007 nilirudi Arusha. Nikapata marafiki wengi na mitandao mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya nchi. Pesa ilikuwa nyingi mpk nikashangaa kuwa ni baraka za namna gani.
Mwaka 2009 siku moja nilishtuka na kitu kimoja pale mume wangu aliposahau pete yake (ile nyingine anayovaa mkono wa kuume sio ya ndoa) nyumbn. Mimi bila kujua nilipoiona niliihifadhi kwenye mkoba wangu nikaondoka nayo. Kumbe nyuma yangu, mume wangu alirudi nyumbn ghafla na kuitafuta sana pete akanipigia simu nikamwambia ninayo kwenye mkoba aje nilipo aichukue. Cha ajabu alipokuja ili nimpe ile pete haikuwepo tena kwenye mkoba. Nilijikagua na kuwauliza wafanyakzi wenzangu lkn pete haikuonekana. Mume wangu alichanganyikiwa na kunishambulia kwa makofi na matusi akiwa mwenye hasira kubwa- sikuwahi kumuona mume wangu akiwa mwenye hasira na ghadhabu kubwa kiasi kile. Alinidhalilisha hadharani mbele ya wafanyakazi wenzangu na kuniamrisha twende nyumbn haraka. Ofisi yao ilikua nikaribu na ofisi kwangu lkn alinipandisha gari yake na tukaelekea nyumbn bila kupitia ofisini kwao. Kwenye gari tulikua tunagombezana kwani nilijisikia kudhalilishwa kwa hali ya juu sana.
Tulipofika nyumbani, ugomvi ulikua mkubwa sana na sana mume wangu alinipiga kweli. Baadaye watu walikuja lkn hawakuweza kuingia ndani kwani kulikua kumefungwa. Mume wangu alinifungia kwenye chumba kimoja na nikamsikia akiwapigia simu watu kadhaa huku akilia km mtoto. Sikuelewa kwa kweli. Mchungaji wa kule kwenye kanisa letu alikuja na mtu mmoja ambaye alikua ni rafiki wa karibu wa familia yetu lkn foreigner.
Walipofika waliongea na mume wangu kwa muda afu wakaondoka. Mume wangu akaja akanifungulia mlango akaniambia tuongee- wakati huo alikua mpole na mkimya asiyelia tena.
Akaniambia kuwa ile pete iliyopotea ilikua ndio pete ya maisha yetu. Alipewa na huyo mchungaji na ilikua inamasharti makubwa kuwa lazima aivae yeye tu na isikae muda mrefu nje ya kidole chake. Kwa ufupi pete hiyo haikuwa ya kawaida na ile pete ilikua ni yule mtoto wetu (Alfred) aliyekufa miaka kadhaa iliyopita. Nilishtuka kujua hata ile pete niliopewa mimi haikuwepo mkononi mwangu wakati huo. Ilikua imetoweka, nikazimia kusikia maneno hayo. Nilipozinduka nilijikuta nyumbn kwa mchungaji nikiwa nimelazwa kitandani. Kumbe nilipozimia nilipelekwa hospitali na pia mume wangu akakamatwa na polisi akawekwa lokap lkn akaachiwa bady kutokana na ushawishi wake pale polisi na alipowaelezea anavyojua yeye. Alipotoka akaja hospitali wakanichukua mpk nyumbn kwa mchungaji. Nilipozinduka nikamuona mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni walikua wamevaa pete km ile ya mume wangu iliyopotea. Hawakunisemesha kitu wala hawa kuomba lkn waliondoka kule chumbani wakiniacha na mume wangu mara baada ya kupata ufahamu.
Mume wangu alinichukua mpk nyumbn, tulipofika hatukuongea kitu mpk asbh. Yeye alienda mjini baadaye akarudi akiwa bado mwenye mawazo na wasiwasi mkubwa. Siku hiyo ikapita na kesho yake. Marafiki zangu walikuja kunitembelea ili kunipa pole lkn hawakuruhusiwa. Kumbe mume wangu aliwaambia watu pamoja na ndugu zangu kuwa nimemuibia mali nyingi sana nimeficha kusikojulikana. Ndugu zangu walipokuja aliwaruhusu kwa masharti kuwa nisiwaambie ukweli. Akanitisha kuwa nikisema ukweli tutakufa wote.
Maisha yaliendelea kwa siku kadhaa, nikaendelea na kazi lkn nikiwa mwenye mawazo makubwa. Nikaomba off kazini kwa muda ili nipate ahueni. Mume wangu naye akaomba off pia tukawa tunashinda ndani tu. Nyakati za usiku nikiwa nimelala mara nyingi niliota ndoto kuwa Alfred mwanangu ananiita yuko barabarani anahangaika akiwa analia. Nikimwambia mume wangu ananiuliza ni wapi eneo gani hasa, nikimtajia eneo nilipoota ananiambia hapo ndipo pete ilipo kwa hiyo ataifuata- nakweli mara nyingi alikua anaamka anaondoka eti kuifuata hilo eneo nilipomuona mtoto wangu kwenye ndoto.
Pete ile haikuwahi kuonekana na maisha yetu yalianza kuporomoka siku hadi siku. Mume wangu hakufurahi tena. Alikua ni mtu mwenye majonzi na wasiwasi sana juu ya maisha yetu siku zijazo. Wakati huo aliwafukuza wafanyakazi wote wa nyumbn na alininyanganya simu zote na alifungia ndani nisitoke nje
Siku moja ikitokea mjini katika mizunguko yake alinijia na habari mpya akidai kuwa ndio suluhisho la tatizo letu. Aliniambia kuwa ili turejee ktk maisha yetu ya kawaida inabidi tumuue mtoto wetu Minza pia kwa siku zote za maisha yetu kuanzia siku hiyo itakua ni marufuku kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida ila tu kinyume na maumbile (yaani awe ananiingilia kinyume na maumbile ya mwanamke). Akaniambia hakuna namna nyingine ya kurejesha maisha yetu zaidi ya hivyo. Nilishtuka sana nikaogopa mno. Nilimlaumu sana mume wangu kwanini alijiingiza ktk maisha hayo- ndipo akanieleza hbr kamili kuwa mafanikio yetu yote yametokana na mfumo huo wa maisha tangu siku ile aliporudi ile safari tukiwa Karatu. Kumbe siku ile alikua ametoka kwa mganga aliyepelekwa na yule rafiki yake.
Nilimshauri mume wangu twende kwa mchungaji tukaombewe lkn akasema kuwa tukisema tu kwa watu tutakufa wote. Pia akasisitiza kuwa sisi wote tuko katika mtandao huo kwa hiyo sio rahisi kujiokoa tena. Kesho yake mume wangu alinikumbushia tena akasema ni lazima tufanye hivyo na pia sio kwa kulazimisha inatakiwa iwe kwa hiari ili tupate faida kwa haraka. Bado nilikataa, sikuwa tyr kufanya hivyo. Nilimuomba mungu usiku na mchana atusaidie. Lkn mume wangu Alinitisha sana na kunifinya mwili ili nikubali kwani alikua mwenye hasira na ghadhabu kubwa. Pia alinifungia ndani ili nisitoke nje. Pia alisisitiza nisiombe kbs. Maisha yaligeuka kuwa jehanam.
Siku km mbili zililizofuata tulipigiwa simu kutoka shuleni kwao na mtoto wetu kuwa Minza ametoweka shuleni hajulikani alipo. Tulikwenda haraka kujua hatma ya mtoto wetu. Niliogopa zaidi kwani nilijua labda ndio keshapatikana- japo mume wangu alionekana kuwa si mwenye wasiwasi ht kidogo. Nilianza kukumbuka kukemea na kuomba Mungu atusaidie lkn mume wangu alinikataza nisiombe kbs. Akanizabua kibao kikubwa mdomoni tukiwa kwenye gari mpk damu ikatoka mdomoni. Nikisikia uchungu mkubwa zaidi kwanini maisha yalikua yanaenda hivyo ghafla au nini faida ya kuishi basi.
Tulisafiri siku nzima mpk kufika shuleni kwa Minza mwanangu. Kitu cha ajabu ni kwamba tulimkuta mtoto akiwa hospitali amelzwa haongei wala hajitambui- na taarifa zinasema alikutwa chumbani(hostel) kwao mchana huo akiwa anatokwa na damu nyingi.
Siku kadhaa bdye tulipewa mtoto wetu baada ya kupata nafuu tukarudi naye nyumbn kwa matibabu zaidi. Minza aliendelea kuugua sana bila nafuu na hakuweza kuzungumza kitu alikua ni mtu wa kulala kitandani na kutazama tu.
Ilipita miezi kadhaa maisha hayo yakawa yamechukua sura ya familia yangu. Miradi kadhaa tuliyoifungua mjini ilikua imefungwa, pia kazini kwangu nilikua nakwenda kwa shida sana. Uwezo wangu wa akili na kiutendaji ulipooza sana. Nilijiingiza kwenye chama cha ulevi wa pombe km mume wangu ili kupoteza machungu na kupunguza mawazo. Lkn hai kusaidia. Lkn kule kanisani tuliendelea kwenda na mume wangu aliendelea na kazi kule UN.
Siku moja mume wangu aliniambia tunakwenda shambani kwa siku kadhaa twende wote- tulijiandaa tulikwenda pamoja. Tulipofika huko, tulijumuika pamoja na mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni. Tulifurahi na kunywa na kula mpk usiku kwa siku hiyo ya kwanza. Kesho yake asubuhi na mapema niliitwa na mume wangu kuwa kuna kikao- Cha ajabu ni kwamba asbhu hiyo mchungaji na yule mkameruni walikua wamevalia mavazi ya kitamaduni kupitiliza kawaida yao. Tulikwenda mpk vichakani zaidi kwani walisema kuna maongezi muhimu sana.
Tukiwa huko yule mchungaji alitueleza waziwazi kuwa yeye ni mtu mwenye nguvu nyingi sana na amewasaidia wengi sana. Na pia hata zile mali za kwanza na kufanikiwa kwetu ni yeye ndiye aliyetusaidia kwa nguvu zake. Na nguvu hizo ni zilitokana pete yake. Pete yake ndio inayompa nguvu na kumletea bahati na mvuto kwa watu.
Kwa kuwa tulikua tumeshindwa kutekeleza sharti la kwanza la kumuua Minza na muda ulikua umepita basi, kuna sharti lingine la mwisho
Kwa hiyo, akasema anao uwezo wa kutupatia pete nyingine lkn ndio kwa masharti. Na leo hapo yuko tyr kutusaidia tena ili tufanikiwe na tusife- kwani tulikua tumefanya makosa makubwa sana kupoteza ile pete ya awali.
Akatoa masharti ili tupate pete nyingine inabidi mimi nikubali pale niingiliwe kimwili nao wote watatu. (yaani nifanye mapenzi na wote watatu pale kichakani hadharani na mmoja baada ya mwingine akianza mume wangu). Vinginevyo mume wangu atapoteza maisha pale pale na mimi pia ningekufa siku zijazo au ningekua kichaa. Nilishtuka nikaogopa sana, nikaanza kupiga mayowe huku nilikimbia kuelekea kwa mume wangu- nililia sana kwa uchungu huku nikitaja jina la mume wangu kwa kumlaumu kwanini alijiingiza kwenye mambo hayo. Mume wangu alinisihi nikubali ili tusife kwani hakukua na namna nyingine.
Sikukubali. Nilianza kukimbia kuelekea barabarani kuhofia usalama wangu kwani niligundua mume wangu hakuwa na uwezo tena wa kunisaidia au kujiokoa. Nilpofika mahala tulipopark magari yetu sikuona gari ht moja. Nikiwa ktk hali ya kukimbia na kujiokoa huku nikipiga mayowe niliwaona yule mchungaji na yule mkameruni wamenitokea nyuma na mbele yangu. Ghafla yule mchungaji aliniwekea mkono kichwani nikaanguka chini nikapoteza fahamu.
Niliporejea fahamu zangu ni siku nilipojikuta niko katikati ya kundi la watu walinisimamia na kuniangalia kwaumakini mkubwa sana. Kumbe ilikua ni kwenye maombezi. Fahamu zangu zilinirejea na kujitambua japo nilikua nimeharibika mwili na mavazi machakavu pia nikiwa nimefungwa kwa kamba ngumu sana. Nikifanikiwa kuwatambua baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliokuwepo pale.
Kwa masaa kadhaa nilijisikia kupumbaa kama mjinga bila kujua nifanye nini. Alitokea mtu mmoja akaniambia pole. Akaniuliza kama ninajisikiaje kwa wakati huo. Nikamuelezea. Kisha nikamuhoji kuwa hapo ni wapi- akaniambia kuwa ni kituo cha maombezi na yeye ndiye mchungaji.
Inasemekana kuwa siku hiyo nilikua nimefunguliwa kutoka katika ukichaa ulionisumbua kama miaka mitatu na nusu. Katika muda wote huo niliishi msituni km mnyama. Nilitafutwa na ndugu zangu kwa muda mrefu sana bila mafanikio. Hakuna mtu alijua mimi au mume wangu tulikua wapi.
Baadaye Nilipouliza kuhusu mwanangu Minza na mume wangu, nijibiwa kuwa waliokufa miaka mitatu na nusu iliyopita. Ndipo nikakumbuka mambo magumu ya maisha yaliyonipata. Nilitunga msiba mkubwa upya kabisa. Nililia sana na kujionea huruma kama yatima asiye na msaada. Sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote. Hata uhai nilionao leo ni Mungu tu amenisaidia.
Updated at: 2024-05-23 14:50:15 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nilianza kujisikia vibaya hata kabla ya kufunga ndoa. Nakumbuka miezi mitatu kabla wakati tukiwa katika maandalizi maandalizi ya Bashiri kuja nyumbani kuleta mahari miguu ilianza kuuma kiasi cha kushindwa hata kutembea. Mama ainikanda mara kwa mara na ilikuwa ikivimba na kutoa maji kama vile jasho lakini la baridi.
Nilienda hospitali zote lakini sikugundulika na kitu chochote, nilipewa dawa tu za maumivu ambazo kusema kweli hazikusaidia chochote. Ndiyo nilikuwa nimemaliza chuo hivyo hata mchakato wa kuzunguka kutafuta kazi ilibidi niusimamishe, Bashiri alinipa moyo na kuniambia kuwa kazi nitapata tu nishughulikie afya yangu kwanza.
Nilifuata ushauri wake na mipango iliendelea huku nikipata nafuu na kuzidiwa, napata nafuu nazidiwa hivyo yani. Kutokana na hali yangu tuliamua kuchanganya sherehe zote kwamaana ya Send off na Reception, Kitchen Party ilifanyika kwa watu wachache na muda wote nilikuwa nimekaa. Siku ya sherehe niliingia ukumbini vizuri, sherehe ikaanza tukakata keki, tukala chakula lakini zawadi kule kusimama kupokea zawadi nilishindwa kabisa.
Miguu ilikuwa inawaka moto huku ikitoa jasho la baridi, sijui nini kilikuwa kikiendelea huko chini kwani viatu nilivyokuwa nimevaa vilijaa maji, niliwekewa kiti na MC akasema maharusi wakae na alipoona nimezidiwa alisema watu wacheze mziki na maharusi tuachwe wakapumzike. Watu hawakuelewa chochote kwani ingawa nilishindwa hata kunyanyuka lakini MC alikuwa mjanja.
Aliongea kua Bwana Bashiri sasa hembu mbebe mke wako kuonyesha upendo kuwa utamlinda na kubeba katika maisha yako yote. Mume wangu alininyanyua na kunibeba kunitoa nnje, nililazimisha tabasmu mpaka nilipoingia kwenye gari ambapo moja kwa moja tulielekea Muhimbili ambapo nilikaa kwa wiki mbili bila kupata nafuu yoyote. Walishindwa kwani walikuwa hawajui ni kitu gani kilikuwa kikisababisha hali ile.
Miguu ilikuwa inauma kwenye mifupa, mwanzoni ilikuwa ni mpaka magotini lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda maumiivu yalipanda mpaka kiunoni. Mbali na maumivu nilikua nikitokwa na jasho la baridi kama maji, yaani nikilalia shuka au nikivaa nguo baada ya masaa mawili nakuwa kama nimemwagiwa maji. Mwili unachemka lakini natoa jasho la baridi.
Kutokana na maumivu sikuweza kufanya chochote, hata kunyanyuka kwenda kujisaidia ilikuwa shida hivyo mume wangu alikuwa na kazi ya kunibeba kila siku mpaka chooni na kunisafisha. Anapokuwa kazini tulikuwa na mfanyakazi ambaye alikuwa akinisaidia kama kunikausha maji lakini alikuwa hawezi kuninyanyua hivyo kazi zote za kunibadilisha na kunisafisha ilikuwa juu ya mume wangu.
Mwaka uliisha nikiwa katika hali ile, mume wangu alijitahidi sana akauza na viwanja vyake alivyo nunua kipindi cha ujana na kunipeleka mpaka India lakini haikusaidia, nilipewa dawa tu kwaajili ya kukausha jasho ambazo zilisaidia kidogo lakini maumivu yalikuwa hayakomi, sanasana mwili ulikuwa unakakamaa tu.
*
Yale hayakuwa aina ya maisha ambayo nilipanga kuishi katika ndoa, kila nilichokuwa nikikiwaza kilikuwa kinyume chake, nilimuonea sana mume wangu huruma kwani badala ya kuwa mume alibadilika na kuwa nesi. Muda ulikuwa unaenda na kama mtoto wa kwanza nyumbani kwao wazazi walishakata tamaa, walihitaji mjukuu na kila siku walimsumbua kutafuta mke mwingine.
Hata mimi nilitamani aoe mke mwingina au hata atafute kimada wa kumtuliza hisia zake kwani tangu kuoana tulikuwa hatuja kutana kimwili, kamba mwaka uliisha bila mimi na mume wangu kufanya mapenzi. Siku moja uvumilivu ulinishinda na nikiwa katika maumivu makali nilimshauri kuwasikiliza ndugu zake na kutafuta hata mwanamke wa kuzaa naye tu kwani mimi sikuwa na dalili za kupona.
Aliniangalia kwa huzuni kisha akaniuliza. āUnataka kuniambia kama ni mimi ningekuwa kwenye hali hiyo na wewe ungeniacha ukatafuta mwanaume mwingine?ā Jibu lake lilikua rahisi āHapana, wewe ni mume wangu nakupenda sanaā¦ā Niliongea kwa suti ya unyonge lakini ya kumaanisha. āSasa kama ni hivyo mbona mimi unataka nikusalitiā¦ā
Nilitulia kidogo na kumuambia āLakini wewe ni mwanaume, unahisia, sisi wanawake tunaweza kuvumilia, lakini wewe ni mwanaume, wazazi wako wanataka wajukuu, mimi siwezi kupona leo wala kesho oa mwanamke mwingine hata kama hutaniacha nitafurahi kukuona unafurahaā¦ā Nilijitahidi kujibu kwa sauti ya kutetemeka na ya kukata tamaa. Bashiri aliniangalia machoni kwa muda mrefu kisha akaniuliza.
āHivi kuna fomu ambazo ulijaza kufanya maombi ya huu ugonjwa kwa Mungu?ā Aliniuliza swali ambalo sikupata jibu⦠āMimi ndiyo napaswa kukuonea huruma kutokana na maumivu uliyonayo sio wewe kunionea huruma eti nahitaji mwanamke wakutuliza hisia zangu au mtoto ili na mimi nionekane mwanaume!Kama siwezi kuvumilia hisia za mwili wangu kw asababu ya ugonjw abasi sipaswi hata kuitwa mwanaume achilia mbali mume wako!ā Aliongea maneno ambayo yalinipa faraja na kunifanya niandelee kupigana bila kukata tamaa.
Miaka miwili ilipita hali yangu ikiwa bado haijatengamaa, nilitamani kukata tamaa lakini kila siku mume wangu alinipa nguvu ya kuendelea kupambana. Tulienda kwennye maombi na kutumia dawa mbalimbali za hospitalini na za kienyeji lakini haikusaidia. Watu wengi waliamini nimelogwa lakini kutokana na imani tulimkabidhi Mungu awe muamuzi wa yote.
Siku moja mume wangu alikuja na Mzee mmoja pale nyumbani, wakati huo sikua najua alimpatia wapi lakini yule mzee alikaa nyumbani pale kwa miezi sita akiondoka mara moja moja na kukaa kama siku nne tano na kurejea. Alikuwa akija na dawa za kienyeji za kunikanda, kunichemshia na kunywa, dawa zilikuwa chungu na kusema keli ilikuwa kama adhabu kwani ilikuwa kutwa mara tatu na kukandwa tena dawa za moto.
Ukichanganya na maumivu basi ilikuwa kazi sana lakini sikua na namna nilivumilia. Kweli miezi sita ile nilianza kupata nafuu, maumivu yaliisha kabisa ingawa bado nilikuwa siwezi kunyanyuka, miguu haikuwa ikitoa maji tena wala kukakamaa niliweza kukunja lakini sikuwa na nguvu ya kusimama. Baada ya kupata nafuu ile yule mzee alituambia kuwa ameshafanya yake yaliyo ndani ya uwezo wake sasa kilichobaki ni kumuachia Mungu, alinipa dawa za kunywa na kumpa mume wangu jukumu la kunifanyisha mazoezi.
Hali yangu ilianza kutengamaa, kila siku asubuhi na jioni mume wangu alikuwa akinifanyisha mazoezi. Kwa mara yakwanza tangu kuingia kwenye ndoa, niliweza kumuangalia mume wangu na kuanza kumuona kama alivyo bila maumivu. Siku moja wakati akinifanyisha mazoezi, nilimkodolea macho, alikuwa amekonda kupita kiasi, kusema kweli kila siku nilikuwa naye lakini siku ile ndiyo niliona tofauti.
Yaani alikuwa amepungua na kuwa kama mtoto, uso wake ulionekana hauna nuru ingawa kila mara alikuwa akilazimishia tabasamu lakini alionekana kweli na mawazo. Nilijipa moyo nikiamini labda ni sababu ya ugonjwa wangu ndiyo ulikuwa unammaliza kutokana na mawazo, siku nilimuomba kuangalia picha zetu za harusi kweli alikuwa amekonda sana kuliko hata nilivyowaza awali.
Nilishindwa kuvumilia na kumuuliza nini kilikuwa kinamsumbua tofauti na hali yangu, aliishia kutabsamu na kusema hakuna kitu ni maisha tu nikipona na yeye atakuwa sawa. Lakini ukweli mume wangu hakuja kuwa sawa tena. Sikumoja mume wangu aliingia chumbani, nilishaanza kupata nafuu ingawa bado nilikuwa siwezi kunyanyuka wala kufanya chochote.
Alionekana kuwa na huzuni kuliko kawaida yake, ingawa alijaribu kutabasmau lakini nilimuona kabisa akilengwa lengwa na machozi. Aliongea na kunikalisha kitandani kisha nayeye akakaa pembeni yangu na kuniambia. āMke wangu kuna kitu naomba unisaidie, yaani uniahidi kukifanya, nakuomba sana unahidi kitu hicho na hata iweje usijekubadilisha mawazo, naomba sanaā¦ā
Aliongea huku akilengwa lengwa kwa machozi, nilimuambia hakuna hata haja ya kuuliza nilikuwa tayari kufanya kitu chochote. Alisisitiza niahidi kufanya na mimi niliahidi huku nikinyanyua mikono yangu kumkumbatia. āMke wangu naomba nikifa uolewe tena na kama Mungu akikujalia mtoto basi kama ni wakiume umpe jina langu na kama ni wakike basi jina la kati liwe la kwanguā¦ā
Aliongea machozi yakimtoka, sikutaka kumsikiliza kwanini anaongelea kufa nilijaribu kumtuliza lakini aliniomba ni muahidi hicho kitu. Alirudia zaidi ya mara kumi ndipo nilipomuahidi kua nitafanya hivyo. Baada ya kumuahidi aliniambia kuwa yeye hawezi ishi mdua mrefu, aliamua kunificha lakini anajua hana muda hivyo kuamua kuniambia. Mwaka mmoja uliopita aligundulika kuwa ana kansa na ilikuwa katika hatua mbaya.
Hakutaka kuniambia kutokana na ugonjwa wangu lakini Daktari aliyekuwa anamhudumia alimuambia kuwa hana zaidi ya mwaka ila mpaka wakati ananiambia ilikua ni karibu miaka mwili kitu ambacho ilikuwa ni kama miujiza. Aliniambia hajisikii vizuri na kaamua kuniambia kwani hata nguvu ya kunihudumia hana tena. Kweli mume wangu alikuwa amechoka na hali yake ilikuwa mbaya.
Sijui nilipata wapi nguvu lakini nilijikuta nasimama, ingawa sikusimama kwa muda mrefu lakini sikutaka kulia, nilijitahidi kuzuia machozi na kumkumbatia mume wangu. Ilikuwa ni karibu miaka mitatu tangu tuoane na katika muda wote huo tulikuwa hata hatujakutana kimwili, alivumilia ugonjwa wangu tangu siku ya kwanza ya ndoa yetu na mimi nilimuomba Mungu anipe nguvu hata niwezie kumhudumia lanini haikutokea. Sikuweza kusimama tena mpaka sasa wakati naaandika hapa.
Ingawa nimeweza kupona lakini magoti yangu hayana nguvu kuubeba mwili wangu hivyo nalazimika kutumia kiti cha magurudumu. Mume wangu alifariki mwezi mmoja baada tu ya kunipa zile taarifa na kila siku katika mwezi huo alisisitiza niolewe ili niwe na furaha. Ni mwaka wa pili sasa, sijaolewa na sidhani kama nitakuja kuwa na furaha, naweza kufanya kazi zangu lakini sijui kama nitaweza kuufungua moyo wangu tena.
**
Kila siku maneno ya mume wangu hunijia, najua alitaka niwe na furaha na kila siku na muomba anipe mwanaume wa kunipa furaha. Natamani sana nimzalie mtoto ili tu abebe jina lake, nadhani hicho ndiyo kitu ambacho kinanipa nguvu mpaka sasa. Mungu alinipa Mume akanipa na Nesi. Alijitoa kwaajili yangu akiwa mzima na hata baada ya kugundua kuwa ni mgonjwa aliweka ugonjwa wangu mbele na kunihudumia mimi kwanza.
Natamani kuandika mengi ila leo niishie hapa. Lengo la kuandika kisa changu hiki nikuwaasa tu nyie mlioko katika ndoa kuwa msipoteze muda wenu katika kunyanyasana na kuudhiana, katika kugombana, kuna muda mchache sana wa kupendana na kila siku utakua ukijuta kama hukumpenda mwenza wako ipasavyo. Mapenzi ni furaha, ingawa ndoa yangu yote ilikuwa ya mateso lakini yalikuwa ni mateso ya ugonjwa, ilikua ni ndoa ya amani na mume wangu kila siku alihakikisha natabasmau.
Alifanya kila kitu ili kuhakikisha kuwa nina furaha hakuchoka kunifanya nitabasamu hata nikiwa katikati ya maumivu makali. Nakumbuka alijua napenda sana kuvaa viatu virefu hivyo karibu kila mwezi aliniletea zawadi ya viatu na kila viatu vipya vilipotoka alikuwa akiniletea. Alivipanga ndani na kuniambia hakutaka fasheni inipite hivyo nikipona nita vaavvyote. Mpaka sasa sijaweza kuvvaa kwani bado sijaweza kutembea ila naamini ipo siku Mungu atanisimamisha na nitaweza kutembea na nitavivaa vyote kwaajili yake.
Naomba nimalizie hapa, samahanini kwa stori ndefu nitafurahi sana kama utatumia sekunde chache kushea stori yangu. Lengo langu ni kwa yule anayesoma awe mwanamke au mwanaume kumpenda sana mtu aliyenaye na kumuonyesha mapenzi ya kweli kwani siku akiondoka utatafuta mtu wa kumuonyesha mapenzi itashindikana. Mimi nina mambo mengi ya kumkumbuka Mume wangu, hembu jiulize wewe ukiondoka leo mume au mke wako atakukumbuka kwa nini? Atakukumbuka kwa mazuri au mateso uliyompa?
Ahsante sana kaka, huwa natumia muda wangu mwingi kwenye ukurasa wako nikisoma unachoandika kuhusu mapenzi. Watu wengi wanachezea upendo wanaoonyeshwa leo kwakuwa wanadhani labda hautakoma, siku ukikoma ndipo watajuta. Mungu awabariki wote na awasaidie msije kujuta kwa mnayowafanyia wapenzi wenu bali muwatengenezee kumbukumbu nzuri na kuwapa faraja kila siku.
Kumbuka kuna siku utatamani kumuambia mko au mumeo unampenda lakini hatakuwepo kukusikia, kuna siku utatamani kumnunulia zawadi na kumpa tabasamu, kuna siku utatamani kutoka na familia nzima kufurahia maisha lakini mwenza wako hatakuwepo. Kwanini unatumia muda wko mwingi kutengeneza ugomvi, chuki na manyanyaso kwa mwenza wako. Ahsante sana kaka Iddi kwa kukubali kukiandika kisa changu na kunisikiliza, Mungu awabariki wote mliosoma kis ahiki na kitumieni kusambaza upendo.
Updated at: 2024-05-23 14:50:19 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dada mmoja aliyejulikana kwa jina
la Angel, alikuwa anafanya
biashara ya kujiuza ili aweze
kuweka kitu tumboni mwake.
dada huyo alikuwa na wateja
wamaana na mapedeshee wengi
sana kwa hiyo kwa siku yeye
kuondoka na laki 4 au 5
ilikuwa ni kawaida sana.
Siku moja dada Angel aliamua aende
hospitali ili akatoe mimba
aliyokuwa nayo tumboni mwake,
alifanikiwa na kutoa mimba ile
lakini baada ya kumaliza utoaji wa
miamba alimuomba daktari atoe
kizazi kabisa ili asipate tabu ya
kuja kutoa mimba kila mara!
Daktari alifanya kama
alivyoambiwa.
Dada Angel alirudi mtaani na
kuendelea na biashara ya kujiuza.
Siku moja ilikuwa jumapili Angel
alikutana na rafiki yake wa muda
mrefu waliyekuwa wanaishi wote
enzi za utoto wao, rafiki yake
huyo alimwambia Angel waende
kanisani, ili kuficha aibu ya
biashara aliyokuwa anafanya;
dada Angel alikubari na
wakaamua kwenda wote
kanisani.
Siku hiyo Angel alilielewa sana neno la Mungu kutoka kwa mchungaji na akaahidi
kuwa jumapili ijayo ataenda, basi
ikawa tabia mpya ya dada Angel
akawa kila siku anafanya biashara
zake za kujiuza na jumapili
anaenda kanisani..
Kadri siku
zinavyozidi kwenda dada Angel
akaanza kupunguza biashara ya
kujiuza na kumgeukia Muumba
mpaka akaacha kabisa tabia ya
kujiuza na kuanza kufanya
shughuli nyingine zilizokuwa
zinamuingizia kipato.
Siku moja Angel alienda kanisani
na alipokuwa ameketi mchungaji
alimfuata na kumwambia
"nimeoteshwa kuwa ww ndiyo
utakuwa mke wangu wa kufa na
kuzikana" dada Angel alishtuka
na alimtazama mchungaji na
kumwambia "mchungaji
umekurupuka mimi kamwe
siwezi kuwa mke wa mtu na
kamwe siwezi kuzaa" alimaliza
Angel na kuondoka kanisani.
Kila wiki aliyokuwa anaenda kanisani
dada Angel alikutana na maneno
yale yale kwa mchungaji na
mchungaji alimwambia "nimeota
umepata ujauzito na umenizalia
watoto wanne" Angel
alimuangalia mchungaji na
kusimama na msimamo wake
ulele ule.
Siku zilizidi kwenda lakini
kutokana na mchungaji
kuendelea kusema maneno yale
yale basi ilibidi dada Angel
akubali na akakubali kuolewa na
mchungaji na wakafunga ndoa na
ndoa yao ilikuwa ya furaha sana.
Kadri siku zilivyozidi kwenda dada
angel alianza kuona mabadiliko
mwilini mwake na kuamua
kwenda katika ile hospitali
aliyowahi kwenda mwanzo kutoa
mimba na kumkuta daktari
aliyemfanyanyia utoaji wa
mimba siku za nyuma, baada ya
daktari kumona Angel akajua
amekuja kwa shida nyingine
ikabidi amuulize "Dada Angel
nikusaidie nini tena dada yangu"
Angel alijibu kuwa anahisi
anadalili za ujauzito, Daktari
alicheka sana baada ya kuambiwa
hayo majibu kutoka kwa angel
na daktari alimwambia "Dada
Angel naona umechanganyikiwa enh dada yangu?? mimi ndiye
nilitoa kizazi chako leo iweje uwe
na mimba acha kuchekesha
walionuna"
Angel alimwambia daktari
chukua vipimo kapime, kweli
daktari alifanya hivyo na baadae
akarudi mikono inamtetemeka na
kumwambia angel "Dada
angel nipeleke na mimi kwa
huyo uneyebuabudu nami niweze
kumuabudu maana ni mkweli na
anasaidia wanyonge,
Dada
Angel wewe ni mjamzito wa miezi
miwili". Angel alilia huku
akiamini kuwa Mungu ashindwi
na kitu chochote Duniani.
Daktari wiki ilifata naye alienda
kanisani na kuanza kumtukuza
Munguā¦
Ndugu yangu hata kama upo
katika wakati mgumu kiasi gani
lakini kumbuka yupo anaweza
kufanya ugumu wa mambo yako
kuwa mepesi kama unatafuna
karanga.
hakuna kinachoshindikana kwa
Mungu,comment AMINA kama unaamini
hakuna kinachoshindika na kwa
jina lake yeye muumba na kama
unaamini magumu yako yote
yenaweza kuwa mepesi
kupindukia