NDOA sio kichaka cha kujificha kukimbia matatizo. NDOA sio mahali pa kutolea mkosi. Wala sio mahali pa kupunguzia shida. Ndoa sio mbadala wa elimu na michakato ya kimaisha. Huolewi ili kupunguza adha za maisha. NDOA ni jukumu zito kuliko hata kusoma masters degree ya Neuro-surgeon. Wengi hamjaweza kumudu maisha yenu binafsi na bado mnalilia Mungu kuwaongezea jukumu la kumeneji maisha ya mtu mwingine.
Updated at: 2024-07-16 11:49:46 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
NDOA sio kichaka cha kujificha kukimbia matatizo. NDOA sio mahali pa kutolea mkosi. Wala sio mahali pa kupunguzia shida. Ndoa sio mbadala wa elimu na michakato ya kimaisha. Huolewi ili kupunguza adha za maisha. NDOA ni jukumu zito kuliko hata kusoma masters degree ya Neuro-surgeon. Wengi hamjaweza kumudu maisha yenu binafsi na bado mnalilia Mungu kuwaongezea jukumu la kumeneji maisha ya mtu mwingine.
Kama huwezi hata kujitafutia hela ya kusuka nywele zako utawezaje kuendesha maisha ya familia. Maana unaweza kuolewa na mwanaume mwenye pesa lakini akapitia mithihani pesa zikatoweka utafanyaje kama huna akili ya kujiongeza? Ndio maana wengi mnawakataa watu wenye Ndoto lakini hawanapesa kwa sasa kwa sababu ya akili ya utegemezi. Unataka mwanaume mwenye kila kitu, sababu kubwa ni uvivu na uzembe. Hutaki kujitafutia vya kwako. Ukisoma MITHALI 31 inaeleza habari za MKE MWEMA.
Hapo ndio pa kujipima je unakidhi hivyo viwango? Mke mwema sio tegemezi ila ni mwanamke mwenye uhuru wa kifedha (Financial Freedom). JIULIZE TU KAMA IKITOKEA HUJAOLEWA MIAKA MITANO IJAYO UTAKUWAJE? MAISHA YAKO YATAKUWAJE? UTAKUWA NA HALI GANI? Maswali kama haya yatakusaidia kujiongeza. Tafuta kitu cha kufanya hata kama Ndoa isipotokea leo isiwe mwisho wa maisha, Ndoto na maono yako. Siku hizi wanaume hawaulizi ukoo wanauliza UNAFANYA NINI?
Mtu anapiga hesabu akikuoa mkaunganisha nguvu mtafanya nini kwenye maisha. Sasa wewe kalia kubandika kope na kuchora kucha kutwa nzima huna shughuli ya kufanya huku ukingoja kuombewa upate Mume. Watu hawaoi mapambo wanataka Wake watakao tengeneza nao hatma zao. Pambo ni kwaajili ya Starehe lakini MKE ni kwaajili ya maisha. Sikupondi wala sio nia yangu kukuvunja moyo, nataka utoke hapo ulipo ujiongeze ili hata ukiingia kwenye Ndoa isijae visa na kuonewa. Pesa itakupa heshima, pesa inakupa sauti, hata Wakwe zako hawawezi kukunyanyasa ukiwa na pesa kwani wanajua watakosa vitenge.
Nataka nikwambie kweli, ukiwa na hela utachagua mwanaume wa kukuoa kwani wapo wengi ila kama umefulia, tegemezi kweli utaona wanaume ni wachache. Pata kitu cha kufanya, tengeneza milango ya kipato. Badala ya kukesha unaomba Mungu akupe Mume anza kuomba Mungu akupe uhuru wa kifedha, kama itakubidi kurudi shule rudi tu. Jiongeze usibaki hapo ulipo. Ni Yesu peke yake asiyebadilika (Hebrania 13) Lakini wanadamu wote lazima tubadilike kila kukicha tukihama hatua moja kwenda nyingine.
Mungu akufungue macho kuona kiini cha ujumbe huu na lengoF lake na wala usichukuliwe na upepo wa adui upindishao maana katika jumbe zenye kubadilisha maisha kama hii.
Kuolewa sio mwisho wa maisha, Mungu kwanza achukue nafasi kwenye maisha yako na akupe utoshelevu katika moyo wako kiasi kwamba uone hata bila Mume unaweza kuishi.
Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kutubu na kumgeukia Mungu katika wongofu wa moyo?
Moyo wangu unaruka kwa furaha kila ninaposikia kuhusu ujumbe wa Kanisa Katoliki kuhusu kutubu na kumgeukia Mungu. Ni wazi kuwa wongofu wa moyo ni muhimu sana katika kuimarisha uhusiano wetu na Mungu na katika kivuli cha kanisa hili, tunaweza kujifunza mambo mengi yanayotuhusu.
Updated at: 2024-07-16 11:49:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kutubu na kumgeukia Mungu katika wongofu wa moyo?
Ndio! Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kutubu na kumgeukia Mungu katika wongofu wa moyo. Kutubu ni kutambua makosa yetu, kujuta na kuahidi kubadili tabia zetu kwa kufuata kanuni za Mungu. Kimsingi, toba ni kuanza upya kwa njia ya Mungu.
Kanisa Katoliki linasisitiza kuhusu umuhimu wa toba kwa sababu inampendeza Mungu na inaleta amani na furaha kwa wanaotubu. Biblia inatuambia katika Luka 15:10 kwamba mbinguni kuna furaha kubwa miongoni mwa malaika wa Mungu wanapompokea mwenye dhambi anayetubu.
Kanisa linatueleza kuwa toba inahitaji kujutia dhambi zetu na kujitakasa. Inasema kwamba kutubu ni kujikana, kujinyenyekeza na kumwomba Mungu msamaha kwa unyenyekevu. Kuna haja ya kutambua kuwa dhambi zetu zinamuumiza Mungu na kuanza kutafuta njia ya kumpendeza.
Kanisa Katoliki linatufundisha pia juu ya umuhimu wa sakramenti ya toba. Sakramenti hii inasaidia katika wongofu wa moyo kwa kupata msamaha wa Mungu na kijito cha uzima katika Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, sakramenti hii ni muhimu katika kujenga uhusiano wetu na Mungu.
Kwa mujibu wa Catechism of the Catholic Church, toba ni muhimu kwa sababu inaponya na kurejesha uhusiano wetu na Mungu. Inaelezea kuwa kutubu kunatufanya kuwa wapya kwa sababu inatutoa katika hali ya dhambi na kutufanya watakatifu. Catechism pia inasisitiza umuhimu wa toba kama njia ya kuungana na Mungu na kufikia utakatifu.
Kwa hiyo, tunaweza kusikia kwa ufasaha kwamba Kanisa Katoliki linasisitiza umuhimu wa toba na kumgeukia Mungu katika wongofu wa moyo. Tunatakiwa kujifunza kwa kina juu ya toba na kujitahidi kutenda kulingana na kanuni za Mungu. Mwisho wa siku, toba inatuleta karibu na Mungu na inatuwezesha kuishi kwa furaha kama wana wa Mungu.