Updated at: 2024-05-25 16:58:28 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jumapili baada ya kutoka KANISANI, Pastor akaona simu yangu niliyonunua LAKI 5,akaniuliza hiyo simu umenunua Bei gani?
Kwakuwa natoaga sadaka kidogo,na ZAKA ndo sijawahi kutoa,Nikamjibu nimenunua JANA,ELFU 50, akanipa LAKI MOJA,nikanunue mbili,yake na ya mke wake. Sa najaribu kumuuliza Mungu,kwanini kaamua kuniadhibu mbele ya mchungaji bila hata kunionya!
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Updated at: 2024-05-25 17:10:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo kampigia simu baba yake; DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti? DOGO : Lakini baba BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona ntakachofanya. DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda shilingi milioni 3 BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua haraka mwanangu mpenzi…
Updated at: 2024-05-25 17:46:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MADENGE HAKOSI VISA
baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake. BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa. MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. 😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:55:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule "Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny" anakuuliza "pckt mny" ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha "pocket money" af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Updated at: 2024-05-25 17:57:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!