Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Updated at: 2024-05-25 18:07:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji "unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki", Mchungaji akasema "ungewaacha kwanza nichukue sadaka…!
Updated at: 2024-05-25 17:09:25 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili 😂😂😂hapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Ungekua wewe ndio mama wa huyu mtoto ungemfanyaje?
Updated at: 2024-05-25 17:11:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna mtoto mmoja aliamka kutoka usingizini alipokuwa kalala na mama yake na kupiga kelele "mamaa" mama yake akaamka na kumwambia nin mwnangu mtoto akajibu "mama nimeota ndoto mbaya sana" ndoto gani hyo mwanangu mtoto akajibu "nimeota tumefungua shule"
Updated at: 2024-05-25 18:12:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata 'Laki Moja' ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:13:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtoto…Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasa…..
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!