Updated at: 2024-05-25 17:04:59 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.ππ
Dogo alivyomchomea dada wa kazi kwa mama yake kuhusu baba
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Updated at: 2024-05-25 18:06:07 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.
Updated at: 2024-05-25 17:09:46 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema hataki tena kujiunga fb!
ππππππππππππππ Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Updated at: 2024-05-25 17:12:24 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama PADRI: Haya JAMAA: Niliiba kamba PADRI: Kamba? JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng'ombe PADRI: Kwa hiyo uliiba ng'ombe? JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng'ombe PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa
Angalia huyu boyfriend alivyomuweza huyu msichana wake
Siku moja msichana alikuwa anapita maeneo ya A.T.M gafla
akamuona boyfriend wake anatoa pesa kwenye A.T.M binti
akaamua kujificha na kumtumia boyfriend wake sms ya
kimahaba
Updated at: 2023-04-29 22:53:12 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Siku moja msichana alikuwa anapita maeneo ya A.T.M gafla
akamuona boyfriend wake anatoa pesa kwenye A.T.M binti
akaamua kujificha na kumtumia boyfriend wake sms ya
kimahaba
"Honey kama upo nyumbani umelala naomba unitumie ndoto
zako,
Kama unakula nitumie chakula, Kama unacheka nitumie kicheko
chako,
Kama unalia nitumie machozi yako,Kama unatoa pesa kwenye
A.T.M nitumie pesa." Boyfriend akajibu "NIKO CHOONI LABDA
NIKUTUMIE KINYESI MPENZI!!