Updated at: 2024-05-25 17:05:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, "naomba leseni yako." Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2 Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu! Haya nenda Ulevi sio mzuri ππππ
Updated at: 2024-05-25 17:57:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.
Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Updated at: 2024-05-25 17:10:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo kampigia simu baba yake; DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti? DOGO : Lakini baba BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona ntakachofanya. DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda shilingi milioni 3 BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua haraka mwanangu mpenziβ¦