Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Nyama
Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo
Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari mchanganyiko/garama masala - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Wali
Mchele - 4 glass
Mbatata/viazi menya katakata - 3 kubwa
Vitunguu katakata - 5
Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) - 1 kijiko cha supu
Hiliki ya unga - 1 kijiko cha chai
Bizari nzima ya pilau/cumin - 1 mti
Samli au mafuta - 2 Vijiko vya supu
Karoti zilokatwakatwa nyembamba - 6-7
Zabibu - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake. kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele. Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto. Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo. Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo. Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive. Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu. Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kupika tambi ni kama ifuatavyo
VIAMBA UPISHI
Tambi pakti moja
Sukari ¾ kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Iliki kiasi
Maji 3 Vikombe vya chai
Vanilla / Arki rose 1-2 Tone
Zabibu Kiasi (Ukipenda)
JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO
1. Zichambue tambi ziwe moja moja.
2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.
3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.
4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto. 5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.
6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa
Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.
Updated at: 2024-05-25 10:23:09 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi
Siagi - ¼ Kikombe cha chai
Baking powder - 2 Vijiko vya chai
Pistachio/ lozi - 2 vikombe vya chai
Mafuta - ½ Kikombe
VIAMBAUPISHI VYA SHIRA
Sukari - 2 Vikombe vya chai
Maji - 2 ½ Vikombe vya chai
ndimu - ½ kijiko cha chai
JINSI YA KUANDAA
Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili) Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta. Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na lozi. Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki. Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana) Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki. Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
ANGALIZO
Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika. Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:35 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 3 vikombe
Samaki Nguru (king fish) - 5 vipande
Vitunguu - 2
Nyanya/tungule - 4
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Pilipili mbichi - 5-7
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7-9 chembe
Kotmiri - 1 msongo (bunch)
Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 2-3
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha samaki, kata vipande kiasi weka kando. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo sana (crush) . Katakata kotmiri weka kando. Saga pamoja, pilipili mbichi, kitunguu thomu, ndimu na chumvi. Changanya pamoja na bizari ya samaki kisha paka katika vipande vya samaki acha kidogo vikolee. Weka mafuta katika sufuria au karai, kaanga vitunguu kidogo tu kisha tia nyanya/tungule endelea kukaanga hadi vilainike na kupondeka. Tia kikombe kimoja na nusu cha tui la nazi, kisha tia vipande vya samaki na masala yake, acha mchuzi uchemke samaki aive. Ongeza chumvi, ndimu, pilipili ikihitajika. Ongezea tui lilobakia acha motoni kwa daika chache tu. Epua mwagia kotmiri mchuzi ukiwa tayari.
Pika wali wa maji/mweupe kama kawaida utolee na mchuzi.
Jinsi ya kuishi maisha marefu (Mambo ya kuzingatia ili uishi maisha marefu)
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuishi ukiwa na afya na kuishi maisha marefu kunawezekana kwa kubadili hali ya maisha unayoishi inayoharibu afya yako mfano uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,kutokufanya mazoezi na kutokula matunda na mbogamboga.
Mambo yanayoweza kukusaidia kuishi maisha marefu ni kama yafuatayo
Kuuandaa mwili kwa maisha marefu kwa kufanya mazoezi
Kuwa makini kutambua na kutibu matatizo ya kiafya
Kuepuka mazingira na kufanya kazi kwa namna au kazi zinazoweza kudhuru maisha yako. Mfano kuendesha gari bila kufuata utaratibu, kutokuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kazi
Epuka vitu vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya yako na kukuletea matatizo ya kiafya kama dawa za mimea na mifugo, zitumie kama inavyotakiwa
Usinywe pombe, usivute sigara wala kutumia dawa za kulevya
Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama isiyokuwa na mifupa - 1 ½ Lb(ratili) Mchele wa Basmati (rowanisha) - 3 Magi Vitunguu maji - 2 Mchanganyiko wa mboga za barafu - 1 Magi (karoti, mahindi, njegere) Pilipili Mbichi - 3 Pilipili mboga kijani na nyekundu - 1 Pilipili manga - ½ kijiko cha chai Chumvi - Kiasi Sosi ya soya (soy sauce) - 5 Vijiko vya supu Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu Mchanganyiko wa bizari (garam masala) - 1 Kijiko cha supu Kotmiri iliyokatwa - ½ Kikombe Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutaarisha
Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi. Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke. Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando. Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama. Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350° kwa muda wa dakika 20 hivi. Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage (beans 2 vikombe vya chai) Nazi (coconut milk kiasi) Vitunguu maji (onion 1kikubwa) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai) Chumvi (salt kiasi) Curry powder 1 kijiko cha chai Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa